"Tumepewa taarifa rasmi kwamba haturuhusiwi kuwa na mashabiki uwanjani kwa hiyo mchezo utachezwa bila mashabiki na wale wanaopenda kufuatilia mpira, mashabiki wetu na mashabiki kwa ujumla watafuatilia kupitia Azam TV ambayo itakuwa live kutokea uwanjani."
Kauli ya Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Azam FC, Thabith Zakaria 'Zaka Za Kazi', kuelekea mchezo wetu wa raundi ya awali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Horseed ya Somalia, utakaofanyika Uwanja wa Azam Complex kesho Jumamosi saa 1.00 usiku.
JUST IN| Gavana wa Rivers United, Nyesom Wike amethibitisha kuwa “hawategemei kuona mashabiki katika mchezo wao wa Jumapili dhidi ya Yanga.”View attachment 1931318
Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Ummy Mwalimu amesema Serikali inakusudia kuandaa mfumo wa kielektoniki wa alama za vidole kwa ajili ya kuhakiki mahudhurio ya Walimu kwenye shule mbalimbali za Tanzania.
Ummy amesema mpango huo ni kwa Shule zote za Msingi na Sekondari katika Halmashauri zote nchini ili kudhibiti mahudhurio ya Walimu Mashuleni, ametoa kauli hii wakati akifungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi Tawi la Tume ya Utumishi wa Walimu Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI Ummy Mwalimu amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Asajile Lucas Mwambambale ili kwenda kujibu tuhuma zinazomkabili katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa za wizi wa mabati.
Waziri Ummy mwalimu pia amemuagiza Katibu Mkuu TAMISEMI kupeleka timu huru ya kuchunguza kwa kina suala la aliyekuwa DED wa Halmashauri hiyo.
Ummy amewakumbusha Watumishi wote wa Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kufanya kazi kwa weledi, kuwa waadilifu na makini katika utendaji kazi wao wa kila siku.
Siku kama ya leo September 10 ya kila mwaka ni siku ya kuzuia kujiua Duniani ambapo ilianzishwa ili Watu wapate uelewa na wachukue hatua madhubuti za kuzuia Watu kujiua hata pale wanapokutana na changamoto maishani.
Kila inapofika tarehe hii Watu hufanya shughuli mbalimbali Duniani za namna ya kuzuia vifo vitokanavyo na kujiua na hii imeanza tangu mwaka 2003.
Inakadiriwa kuwa Watu milioni 1 hujiua kila mwaka na Mtu mmoja kati ya Watu elfu 1 hujiua kila mwaka idadi ambayo ni wastani wa 1.4% ya vifo vyote duniani.
Mwanamke wa Urusi aliyekuwa anaitwa Fagilu Mukhametzyanov alifariki kwa presha akiwa kwenye msiba wake mwenyewe, ni kwamba akiwa Hospitali Daktari alisema ameshafariki hivyo shughuli za mazishi zikaandaliwa lakini kumbe Daktari alikosea kwani Fagilu alikua hai.
Siku ya kuzika akiwa kwenye Jeneza alipata fahamu na kushangaa kukuta umati nyumbani kwao Ndugu, Jamaa na Marafiki wakilia kwa uchungu alipouliza akaambiwa wanajua sababu waliambiwa yeye amefariki hapohapo presha ikapanda kwa mshtuko na akafariki kweli.
Utafiti wa AIIMS wa Nchini India umeeleza kuwa katika kipindi cha miaka 10 iliyopita Watu 330 wamefariki wakati wakiwa wanapiga picha kwenye maeneo hatari kama kwenye majengo marefu, Barabarani n.k kwa lengo la kupost kwenye mitandao yao ya kijamii.
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imeishauri Chadema kuweka picha ya Rais katika ofisi za viongozi wa chama hicho kwa sababu hiyo ni taasisi ya umma.
Ushauri huo umetolewa leo Ijumaa Septemba 10, 2021 na Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza wakati wakifanya ukaguzi wa chama hicho katika utekelezaji wa Sheria ya Vyama vya Siasa na Sheria ya Gharama za Uchaguzi.
Amesema ofisi za vyama vya siasa ni ofisi za umma hivyo ni vizuri wakaendeleza utamaduni wa kuwa na picha ya Rais kwenye taasisi za umma.
"Hii ni ofisi ya umma, ni vizuri kukawa na picha ya Rais ukutani, siyo unaweka picha ya katibu mkuu. Huu ni ushauri tumewapa, tutapita Januari kuona kama wamelifanyia kazi," amesema Nyahoza.
Akizungumzia suala hilo, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema - Zanzibar, Salum Mwalimu amesema Msajili amekuta mambo yamekaa vizuri ndiyo maana akagundua hakuna picha ya Rais.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.