Makapuku Forum

Makapuku Forum

Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu uchumi maarufu kama Mahakama ya Mafisadi Elinaza Luvanda amejitoa kusikiliza kesi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na wenzake.

Jaji huyo amejitoa baada ya Freeman Mbowe kumuomba ajitoe kwa madai kwamba kuna taarifa kuwa Jaji huyo amewekwa kimkakati hivyo hatomtendea haki.
Screenshot_20210906-174317_Instagram.jpg
 
Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma ambaye alihukumiwa kifungo cha miezi 15 jela baada ya kukaidi agizo la Mahakama kuhusu kesi ya rushwa dhidi yake, ameruhusiwa kumaliza kifungo chake akiwa nyumbani kutokana na kuumwa kwake.

Idara ya Magereza imetangaza msamaha huo wa kiafya miezi miwili tu tangu Zuma (79) aanze kutumikia kifungo hicho ambapo amelazwa katika hospitali moja nje ya Mahakama hiyo tangu August 6.

August 14 alifanyiwa upasuaji ambao hadi sasa hIjaelezwa ulikua wa nini ila Idara ya Magereza imesema kwamba uamuzi huu mpya ulitokana na ripoti ya kiafya waliyopata kuhusu Zuma, hata hivyo wamesema atahitajika kufuata masharti atakayopewa na watamfuatilia kuhakikisha anamaliza kifungo chake.
Screenshot_20210906-175017_Instagram.jpg
 
Mtoto wa Rais wa zamani wa Libya Muammar Ghadafi aitwae Al-Saadi Gadhafi ameachiwa huru kutoka gerezani alikowekwa kwa zaidi ya miaka saba Tripoli, Libya.

Kaimu Waziri Mkuu wa Libya Abdul Hamid Dbeibah ametangaza kuachiliwa huru kwa Al-Saadi kutokana na agizo la awali la Mahakama.

Msemaji wa Serikali ya mpito ya Libya Mohamed Hamouda amesema Al-Saadi alikua amefungwa kwenye gereza la al-Hadaba ambako Maafisa wengi wa uliokuwa utawala wa zamani nchini humo wamefungwa.
Screenshot_20210906-175134_Instagram.jpg
 
Siku moja baada ya tukio la kitengo maalum cha jeshi la Guinea kutangaza kuupindua utawala wa Rais Alpha Conde na kumshikilia Rais huyo, Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika, Marekani, Ufaransa na jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za magharibi mwa Afrika (ECOWAS) zimeshutumu vikali mapinduzi hayo na kutaka Rais Conde aachiliwe huru mara moja.

Taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi pamoja na Mkuu wa Kamisheni ya Umoja huo Moussa Faki Mahamat, imelitaka Baraza la Usalama nchini Guinea kufanya kikao cha dharura ili kutathmini hali ilivyo na lichukue hatua muafaka.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres pia ameshutumu vikali hatua hiyo ya jeshi kuchukua madaraka kwa nguvu, kupitia ukurasa wa Twitter, Guterres ametaka Rais Conde kuachiliwa huru mara moja.

Vikosi maalum vya jeshi nchini humo vilidai kuupindua utawala wa Rais Alpha Conde ambaye ametawala Nchi hiyo kwa muda mrefu na kusema wanamshikilia Rais huyo.

Wakuu wa Mapinduzi hayo wametangaza marufuku ya Watu kutoka nje nchini kote hadi watakapotoa maelezo zaidi, pia wamesema nafasi za magavana sasa zimechukuliwa na wanajeshi na kusisitiza kuwa Conde yuko salama na hajajeruhiwa.
Screenshot_20210906-175502_Instagram.jpg
Screenshot_20210906-175527_Instagram.jpg
 
Wakati Yanga wakienda na nyota 28 watani wao Simba imepeleka majina ya wachezaji 31 CAF.
Makipa wanne ambao ni chaguo lao la kwanza Aishi Manula, Benno Kakolanya, Jeremiah Kisubi na Ally Salim katika orodha hiyo.

Safu ya ulinzi ina mabeki tisa ambao ni; Erasto Nyoni, Mohammed Hussein, Gadiel Michael, Henock Inonga ‘Varane’, Israel Mwenda, Joash Onyango, Pascal Wawa, Kennedy Juma na Shomari Kapombe, huku eneo la kiungo likiwa na watu 12 ambao ni Abdulswamad Kassim, Bernard Morrison, Duncan Nyoni, Hassan Dilunga, Jimmyson Mwanuke, Jonas Mkude, Mzamiru Yassin na Pape Ousmane Sakho.

Wengine ni Peter Banda, Rally Bwalya, Sadio Kanoute na Thadeo Lwanga, huku kwenye ushambuliaji kuna nahodha John Bocco, Meddie Kagere, Chriss Mugalu, Yusuph Mhilu, Ibrahim Ajibu na Kibu Denis.
Screenshot_20210906-175812_Instagram.jpg
 
Yanga inajipanga na mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya awali wakikutana na Rivers United ya Nigeria na uhakika pale makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) upande wa Idara ya Mashindano yamefika majina 28 tu,
Orodha ya uhakika ambayo Mwanaspoti imeipata ni kwamba jina la mwisho kukamilishwa katika usajili huo ni kiungo Khalid Aucho ambaye Waarabu wa Lel Makkasa inayoshiriki Ligi Kuu Misri walikuwa wanadengua kutoa uhamisho wake wa kimataifa lakini baadaye wakaachia wenyewe.

Orodha ambayo Yanga imewasilisha inawajumuisha makipa 3 ambao ni Diarra Djigui, Erick Johola na Ramadhan Kabwili huku mabeki wakiwa 9 ambao ni Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Yannick Bangala, Dickson Job, Bakari Mwammnyeto.

Wengine ni Kibwana Shomari, Djuma Shaban, David Bryson, Adeyun Saleh na Paul Godfrey ‘Boxer’ watakaosimamia uimara wa Yanga katika safu ya ulinzi ya timu hiyo.

Yanga imewajumuisha viungo 6 ambao Mukoko Tonombe, Aucho, Feisal Salum, Zawadi Mauya, Deus Kaseke, Jesus Muloko, Farid Mussa, huku kwenye eneo la ushambuliaji itakuwa na watu 5 ambao ni Fiston Mayele, Heritier Makambo, Yacouba Songne, Said Ntibazonkiza na Yusuf Athuman.




Screenshot_20210906-180045_Instagram.jpg
 
Wanigeria wa Yanga watua
.
Wapinzani wa Yanga kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, Rivers United tayari wametua nchini kwa mchezo wao wa raundi ya awali.
.
Rivers watavaana na Yanga Jumapili hii kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, kabla ya kurudiana nao katika mchezo wa kuamua nani avuke kuingia raundi ya kwanza Septemba 19, mechi itakayopigwa katika Uwanja wa Adokiye Amiesimaka uliopo mjini Port Harcourt
Screenshot_20210906-180813_Instagram.jpg
 
Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh akanusha tetesi za kiungo Mukoko Tonombe kufukuzwa timu ya taifa ya DR Congo:

“Mukoko hakuwa fiti ndio maana wamemuondoa kwenye programu za timu yake ya taifa, ataungana na hawa wengine ambao walikuwa na majeraha.”
.
Hafidh ameongeza kuwa Balama Mapinduzi, Yassin Mustafa na Tonombe Mukoko kwasasa wanafanya programu maalum.
Screenshot_20210906-181138_Instagram.jpg
 
Yanga kutesti tena na KMC
.
Imesalia wiki moja tu kabla ya Yanga kukata utepe kwenye mechi ya kimataifa kwa kuvaana na Rivers United ya Nigeria, huku Kocha Nasreddine Nabi akikuna kichwa ili awape raha mashabiki wa klabu hiyo na leo anatesti tena mitambo jijini Dar es Salaam.
.
Kocha Nabi hajaridhika kabisa na maandalizi ya awali aliyoyafanya nchini Morocco na sasa anawafua vijana wake kinoma kambini Avic Kigamboni, ili kuona wanaiva tayari kwa vita ya msimu mpya.
.
Meneja wa timu hiyo, Hafidh Saleh amesema kwamba tayari uongozi umeyafanyia kazi mahitaji ya kocha kwa kutafuta mechi za kirafiki na tayari wameipata ya kesho dhidi ya KMC kabla ya kuangalia wanapata nyingine wakiwasubiri Wanigeria Septemba 12
Screenshot_20210906-181521_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom