Makapuku Forum

Makapuku Forum

Watu wawili wamefariki kwa kunywa sumu katika Kitongoji cha Mlandizi kata ya Mlandizi Tarafa ya Mlandizi Wilaya ya kipolisi Mlandizi Mkoani Pwani.

“Tarehe 5 September 2021 asubuhi huko Mlandizi Watu wawili wanaodaiwa kuwa ni Wapenzi walikutwa wamefariki katika makazi yao baada ya kunywa ya kitu kinachodhaniwa ni sumu, Watu hao ni Godfrey Pius Mandai (48) ambaye alikuwa ni Dereva wa Kampuni na veronica Gerald ( 42) Mfanyabiashara na mkazi wa Mtwara ambaye alisafiri kutoka Mtwara na kumfuata Mpenzi wake huyo Mlandizi.

“Mwanaume yule alitengeneza juisi ambayo ndani yake ilikuwa na sumu akampa Veronica akanywa na kufariki, Mwanaume alipoona Mpenzi wake amefariki na yeye akanywa na akafariki”

“Chanzo ni wivu wa kimapenzi ambapo Mwanaume alikuwa anamtuhumu Veronica kuwa anafanya usaliti, kwenye eneo la tukio tumekuta chupa yenye masalia ya sumu na tumekuta pia karatasi ambayo inadhaniwa imeandikwa na mmoja wao na imeandikwa ‘HUU NI USALITI TU’” ——— asema Kamanda wa polisi Mkoa wa Pwani Wankyo Nyigesa.
Screenshot_20210911-130430_Instagram.jpg
 
Uongozi wa Klabu ya Yanga umepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mjumbe wa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji TFF na Kiongozi wa Simba Sc, ndugu, Zacharia Hans Pope.

Tunatoa pole kwa Uongozi wa TFF, Simba Sc, Familia, Washabiki, Ndugu, Jamaa na Wanamichezo wote.
Screenshot_20210911-131726_Instagram.jpg
 
Waoka Mitake, Azam FC wanataanza kuchanga karata zao hii Leo kwenye dimba la Chamazi, Complex dhidi ya Horseed kutoka Somalia

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa bila ya mashabiki maelekezo kutoka CAF kuendelea kuchukua tahadhari ya Covid
Screenshot_20210911-131932_Instagram.jpg
 
“Ninamfahamu kwa miaka mingi akiwa ni Mwana Simba mahiri , mwenye msimamo na ukweli. Ni mtu aliependa umoja na kupata mafanikio kwa jumla.

Siku zote alikubali kutumikia klabu kwa moyo wake wote , bila kujali muda wake, mali au hasara”- Mwenyekiti wa klabu, Murtaza Mangungu akimzungumzia marehemu Zakaria Hans Poppe.
Screenshot_20210911-132030_Instagram.jpg
 
“Nimefanya kazi na wewe kwa miaka mingi, na kila siku uliweka maslahi ya Simba mbele. Kaka yangu ulikua na wema wa kipekee, na ulikua wa kwanza na ulinyooka linapokuja suala la kuilinda Simba, hukuwa na maslahi binafsi.

Ulikua rafiki wa marafiki wa Simba, na ulikua tofauti na wasioitakia mema Simba.”- Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Mohammed Dewji kufuatia kifo cha Zakaria Hans Poppe.
Screenshot_20210911-132146_Instagram.jpg
 
Klabu ya Yanga imethibitisha kupokea taarifa rasmi kutoka Shirikisho la Mpira Afrika (CAF) kwamba mashabiki hawataruhusiwa kuingia uwanjani kushuhudia mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Rivers United FC ya Nigeria.

Yanga itacheza na Rivers United siku ya Jumapili Septemba 12, 2021 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.
Screenshot_20210911-132401_Instagram.jpg
 
Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu “Gomes anaendelea na kozi ya UEFA Pro ambayo anasoma online, baada ya CAF kubadilisha masharti ya leseni, Gomes alirudi kusoma.
.
Anaendelea kufanya kozi online kwenye ukanda huu ambayo kituo chake kipo Rwanda. Atafanya mitihani na akihitimu atakuwa na vigezo ambavyo CAF inahitaji. Ni wiki sita anakuwa amehitimu, hivyo kwenye mechi yetu ya kimataifa tutakuwa naye.”
.
Gomes kwa sasa ana leseni ya UEFA A diploma na kwa mujibu wa Salum Madadi, kozi ya UEFA Pro hadi kuhitimu inachukua wiki tano, lakini anasema wakati wao wanasoma hadi kuhitimu ilikuwa ni mwezi mmoja haikuzidi hapo.
.
Simba itaanzia raundi ya pili kati ya Oktoba 22 hadi 24 na mshindi kati ya Jwaneng Galaxy ya Botswana na DFC Beme ya Afrika ya Kati.
Screenshot_20210911-132609_Instagram.jpg
 
Matajiri wawapa mzuka mastaa Yanga, kuvuna milioni 500
.
Mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu Bara, Yanga, kesho jioni wanashuka uwanjani ili kuwakabili Rivers United ya Nigeria, huku mastaa wa Jangwani wakiwa wamejazwa upepo baada ya bilionea wa klabu hiyo kuwawekea mzigo wa maana mezani ili kuhakikisha wanalikamilisha jambo lao la kufika hatua ya makundi.
.
Ipo hivi. Jana jioni mabosi wa Yanga walikutana na mastaa wa timu hiyo kwenye kambi yao ya Avic, Kigamboni jijini Dar es Salaam na matajiri hao wakatoa tamko zito la kufika makundi msimu huu, kwa kuwahakikishia kuwa kwamba wamedhamilia kufanya kweli, basi watachukua si chini ya Sh milioni 500 wakiwatoa Rivers United.
.
Fedha hizo ni kama bonasi tu ambapo Yanga wanataka kuhakikisha wachezaji wao wanahamasika na kushinda.
Screenshot_20210911-132731_Instagram.jpg
 
BANDA AJIBU WANAOBEZA KURUDI NYUMBANI
.
Beki Abdi Banda ujiunga kwake Mtibwa Sugar kumezua maneno mengi akionekana kama amefulia, hivyo anajipanga kuwajibu watu kwa mguu wake ili watambue amerejea Tanzania kujipanga upya kisha akakipige nje.
.
Alisema kabla ya kukubaliana na Mtibwa Sugar, alipata ofa za timu zinazotamaniwa na wachezaji wengi, ila alichagua kulinda kipaji badala ya kutanguliza tamaa.
.
“Sio kila wakati mchezaji atatanguliza pesa mbele, hasa mwenye malengo ya kufanya makubwa. Kuna kipindi cha kulinda kipaji chake, kupata timu ya kucheza mechi nyingi za kumjengea ufiti,” alisema Banda.
.
“Nahitaji kucheza mechi nyingi zaidi kwani sijacheza kwa muda mrefu baada ya kutoka nje. Nimechagua Mtibwa Sugar ili huduma yangu iwafae kwa kuonyesha madini ya mguu wangu.”
Screenshot_20210911-132844_Instagram.jpg
 
PSG YAMVIZIA RUDIGER WA BURE
.
Antonio Rudiger, 28, alikuwa mmoja wa mastaa waliokuwa wakihusishwa sana na mpango wa kuhama Chelsea kwenye dirisha lililopita la uhamisho wa majira ya kiangazi.
.
Na sasa mkataba wake huko Stamford Bridge hauzidi mwaka mmoja, hivyo ataendelea kuwa gumzo kwenye mchakato wa kuhama labda kama tu atasaini dili jipya.
.
The Blues walionyesha dhamira ya dhati ya kutaka kumsajili beki wa kati wa Sevilla, Jules Kounde kwenye dirisha lililopita la uhamisho wa majira ya kiangazi.
.
PSG ishaweka mipango yake ya kumnasa bure Rudiger mwakani kama ilivyofanya kwa wakali Lionel Messi, Georginio Wijnaldum, Gianluigi Donnarumma na Sergio Ramos kwenye dirisha lililopita.
Screenshot_20210911-133252_Instagram.jpg
 
Katika maisha fanya kile kinachokupa furaha bwana na amani

Maana ukipatia utasemwa ukikosea utasemwa vilevile

Mimi najijua mwenyewe siangalii flani atasema nini hiyo ni juu yake nafanya vile vinavyonipa furaha na amani roho yangu iridhike tu hata babe wangu analifahamu hilo
 
EPL| RONALDO IS BACK HOME

Nyieee sikilizeni, sisi tunajua wote nyie ni Mashabiki wa Manchester United, sijui Mimi nipo Chelsea, nipo Liverpool, nipo Arsenal ila namkubali tu Ronaldo hiyo sio kweli

HAPANA, huwezi kusema napenda mchuzi ila sili nyama

HT: UNITED 1-0 NEWCASTLE

RONALDO
Screenshot_20210911-180434_Instagram.jpg
Screenshot_20210911-180455_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom