Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20210813-082656_Opera%20Mini.jpg
Screenshot_20210813-082711_Opera%20Mini.jpg
 
Mwanzilishi wa Makampuni ya ASAS, Alhaj Faraj Ahmed Abri (Mzee ASAS) amefariki dunia leo August 13, 2021 Jijini Dar es salaam, Mzee Asas atazikwa makaburi ya Kisutu baadaye leo, Familia imeomba Waombolezaji kutoenda nyumbani kwenye msiba.

RIPMzeeASAS
Screenshot_20210813-110901_GBInsta.jpg
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezungumza na Wakuu wa Mikoa kwa njia ya mtandao (Video Conference) ambapo amesema Rais Samia Suluhu Hassan ametoa fedha nyingi tangu ameingia madarakani na hivyo kuwataka Wakuu wa Mikoa kuzisimamia fedha zinazotumwa kutoka TAMISEMI na Mamlaka ya Elimu nchini (TEA) ili kuhakikisha kuwa zinafanya kazi katika muda uliopangwa.

“Fedha ikija haipaswi kukaa zaidi ya wiki, ni lazima ziende kwenye maeneo ya utekelezaji”———Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

Waziri Mkuu amewataka pia Wakuu wa Mikoa waendelee kusimamia mazao ya kimkakati kama alizeti, chikichi, parachichi na sasa tunaimarisha mazao ya ufuta, kokoa, Zabibu katika maeneo yao.

Kuhusu ulinzi na usalama, Waziri Mkuu amesema viongozi wanapaswa kuhakikisha kunakuwa na utulivu wa kutosha nchini ili watu waweze kufanya kazi kwa amani———-“Pakiwepo usalama baina koo na koo, kijiji na kijiji, itasaidia kufanya kazi na kuongeza uzalishaji”
Screenshot_20210813-111104_GBInsta.jpg
 
Kaimu Afisa habari wa Simba SC Ezekiel Kamwaga amethibitisha kuwa Kiungo wa kimataifa wa Zambia Cloutous Chama (30) amejiunga na Club ya RS Berkane ya Morocco akisaini mkataba wa miaka mitatu.

Chama amesaini mkataba huo unaotajwa kuwa umeigharimu RS Berkane ada ya uhamisho ya Tsh Bilioni 1.5 kwenda Simba SC na kuongezewa mshahara mara nne ya aliokuwa analipwa Simba SC.

Chama ambae ameonekana kwenye mazoezi ya RS Berkane akiwa na Tuisila Kisinda wa Yanga, alijiunga na Simba SC mwaka 2018 akitokea Lusaka Dynamos ya Zambia.
Screenshot_20210813-111212_GBInsta.jpg
 
Wachezaji nyota wa Simba, Luis Miquissone na Clatous Chama hawatakuwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo msimu ujao.

Kutokana na majina yao kuimbwa sana msimu uliopita kwenye michuano yote, Je Simba itaendeleza moto wao uleule au itaanza upya ili wachezaji wapya wazoeane na wa zamani?
Screenshot_20210813-111729_GBInsta.jpg
 
Wananchi Yanga wameshindwa kujizuia na wachache wameamua kupiga kambi Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kuwasubiri wachezaji wao wawili wa kigeni raia wa DR Congo beki Djuma Shaban na winga Jesus Moloko ambao wametua nchini alfajiri ya leo kujiandaa kwenda Morocco kambini.
Screenshot_20210813-111918_GBInsta.jpg
 
Leo, Agosti 13, dunia inaadhimisha siku ya watu wanaotumia mkono wa kushoto. Watu hao ni asilimia 7 hadi10 ya idadi ya watu duniani. Ukiwa unatumia mkono wa kushoto hongera kwa kuwa unakuwa sehemu ya kundi la viongozi bora kama Barack Obama, Albert Einstein na Sachin Tendulkar na wengine kama Oprah Winfrey.

Kwa mujibu wa wanasayansi wa Chuo Kikuu cha Oxford, ubongo wa mashoto hufanya kazi vizuri zaidi ya wengine na sehemu mbili za akili hufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na ndio huw ana stadi nzuri. Kwa wanamichezo, kutumia mguu au mkono wa kushoto humnufaisha sana mashoto na hii ni kwa sababu wachezaji wengi hutumia mikono au miguu ya kulia na hivyo kupata shida kupambana na mchezaji kama Luis Miquisson.

Pia mashoto ni wapiganaji wenye mafanikio. Sifa nyingine, kwa mujibu wa wanasayansi, mashoto ni wazuri katika kuwasiliana kwa maneno.
Screenshot_20210813-112541_GBInsta.jpg
 
Waziri wa TAMISEMI Ummy Mwalimu amemshukuru Rais Samia Suluhu kwa kuonesha kwa vitendo dhamira yake ya kujenga barabara Vijijini kwa kuongeza bajeti kutoka Tshs bilioni 273 mwaka 2020/21 hadi kufikia shilingi bilioni 966.43 mwaka huu wa fedha 2021/22.

Itakumbukwa jana Waziri Ummy alizindua Mpango Mkakati wa Pili wa Miaka Mitano wa Wakala wa Barabara Vijiji na Mjini(TARURA) na kaulimbiu isemayo 'TARURA tunakufungulia barabara, kufika kusipofikika'.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo Waziri Ummy alisema———“Kauli mbiu hii isiwe kwenye makaratasi na mwaka huu ndio wa kuwapima, matarajio ya Serikali na Watanzania kwa TARURA ni makubwa sana tunaomba msituangushe mkafungue Barabara za mijini na vijijini."

Ummy alisema Rais Samia Suluhu Hassan amedhamiria kutatua changamoto za barabara mijini na vijijini kupitia ongezeko la bajeti.

“Mmeniambia kupitia mpango huu wenu wa miaka mitano mtaongeza Kilomita 73,242 za Barabara kiwango cha changarawe, hii itakuwa ni hatua kubwa na mmesema mnahitaji Tsh.Trilioni 3.6, niwatoe hofu tu kama Rais Samia ameweza kutenga Tsh. Bilioni 966.43 mwaka huu sidhani kama atashindwa kutoa hiyo fedha kwa kipindi cha miaka mitano”———Ummy
Screenshot_20210813-144524_GBInsta.jpg
 
Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Patrice Motsepe amewasili leo Agosti 13, 2021 Jijini Dodoma na kupokelewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Innocent Bashungwa, Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Ally Possi na Rais wa Shirikisho la Soka Nchini, Wallace Karia.
Screenshot_20210813-144742_GBInsta.jpg
Screenshot_20210813-144759_GBInsta.jpg
Screenshot_20210813-144814_GBInsta.jpg
Screenshot_20210813-144838_GBInsta.jpg
 
Mmoja wa wafuasi wa Chadema akidhibitiwa na akasri polisi waliokuwa wakilinda usalama katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.

Leo Ijumaa Agosti 13, 2021, kesi ya Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Freeman Mbowe ilikuwa ikitajwa.
Screenshot_20210813-145211_GBInsta.jpg
Screenshot_20210813-145230_GBInsta.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom