Makapuku Forum

Makapuku Forum

Mashemasi 13 wa Jimbo Katoliki la Moshi wakiwa wamelala kifudifudi wakati wakila kiapo cha daraja la upadri kama ishara ya kujitolea maisha yao kwa Mungu.
Ibada ya upadirisho imeongozwa na Askofu wa Jimbo Katoliki la Moshi, Askofu Ludovick Minde akiongozana na mapadri wa Jimbo hilo. Picha na Janeth Joseph.
Screenshot_20210812-165320_GBInsta.jpg
 
Zimbabwe imeanza kufungua makanisa, ambapo ni waumini waliopata chanjo ya corona ndio watakaoruhusiwa kushiriki ibada.

Mwezi uliopita mwanzoni mwa wimbi la tatu la janga la Covid-19 nchi hiyo ilipiga marufuku mikusanyiko ya watu ambayo ilihusisha huduma za ibada makanisani, mamlaka zilisema hali ilikuwa mbaya zaidi tangu mlipuko wa ugonjwa huo uanze mwaka jana.

Serikali ya Rais Emmerson Mnangagwa pia imejaribu kuongeza matumizi ya chanjo za Covid-19 kwa kuondoa posho kwa wafanyakazi wa umma ambao hawajachanjwa na kuwazuia kutumia usafiri wa bure kwenda kazini.
Screenshot_20210812-165546_GBInsta.jpg
 
Mbawakau ni moja kati ya wadudu wa muhimu sana katika Hifadhi, wadudu hawa hula kinyesi cha wanyama na wengi wao hupendelea kinyesi cha Tembo na Nyumbu kwa Hifadhini.

Mbawakau ana uwezo wa kusukuma kinyesi chenye uzito mkubwa zaidi yake baada ya kukitengeneza kama mpira na kwenda kuuzika eneo alilochagua.

Mara nyingi dume husukuma baada ya kutengeneza mpira huo kwa kutumia miguu ya nyuma. Jike hutaga mayai katika mpira huo kisha wanauzika ili viwavi wanapoanguliwa waweze kula kinyesi hicho wakiwa chini ya ardhi Watafiti wanasema kuna zaidi ya aina 100 ya mbawakau upande wa kusini mwa Serengeti.
Screenshot_20210812-165754_GBInsta.jpg
 
Rais wa Malawi, Lazarus Chakwera (pichani) amewafukuza kazi waziri wa nishati na katibu mkuu wa wizara hiyo, ambao wote wanakabiliwa na tuhuma za rushwa.

Wawili hao walikamatwa Agosti 10, 2021, wanadaiwa kuingilia utaratibu wa utoaji wa mikataba ya kusambaza mafuta.
Screenshot_20210812-165920_GBInsta.jpg
 
Spika wa Bunge Job Ndugai, ametoa kauli kuwa subira yavuta kheri hivyo tuendelee kungoja huenda zipo hatua zitakazochukuliwa na Bunge hilo kwa wabunge ambao wametoa kauli zao hadharani kwamba hawako tayari kuchoma chanjo dhidi ya Virusi vya Corona.
Screenshot_20210812-170025_GBInsta.jpg
 
Carlos Rodriguez ni mwanaume anayeishi bila ubongo. Carlos alizaliwa akiwa mzima hana matatizo ya aina yoyote katika mwili wake, wakati wa ujana wake alijiingiza katika matumizi ya mihadarati iliyompelekea kuwa na tabia za uhalifu.

Carlos Rodriguez alipokua na miaka 14 aliba gari, wakati anaendesha, gari likapata ajali na kurushwa nje ya gari na kupiga kichwa chake kwenye lami na kupelekea kuwa na matatizo kwenye ubongo ili kuokoa maisha yake madaktari ilibidi watoe ubongo wake awe bila ubongo, chakushangaza ni kwamba hata baada ya kutolewa ubongo bado hakua amepoteza kumbukumbu kitu ambacho wanasayansi hawakupata jibu kwa nini bado hakupoteza kumbukumbu?

lakini kutoka na nadharia mbalimbali za wanasayansi ni kwamba miishio ya neva iliyoko tumboni inayo unganisha ubongo na tumbo ilikua inamsaidia kuwa na kumbukumbu.
Screenshot_20210812-170127_GBInsta.jpg
 
Nchini Burkina Faso kuna kijiji kinaitwa Bazoule, kijiji pekee ambacho mamba huishi na binadamu kwa Amani na muda mwingine wanakijiji hukaa juu ya mamba hao bila hofu, mamba hawafanyi chochote kwa mtu yeyote.

Vipi na wewe ukiambiwa ukae juu ya mamba utakubali!!??
Screenshot_20210812-170435_GBInsta.jpg
Screenshot_20210812-170501_GBInsta.jpg
Screenshot_20210812-170518_GBInsta.jpg
 
LIONEL MESSI NA ARGENTINA CLAUSE|

Kwenye mkataba wa Lionel Messi na PSG, Kuna kipengele kinaitwa ARGENTINA

Kipengele hiki kinasema:

-Messi ataruhusiwa kujiunga na timu yake ya taifa, iwe mechi ya kirafiki au mashindano ila akiitwa klabu hapaswi kumzuia

-Messi pia amehitaji Maofisa wa soka wa Argentina wawe na uhuru wa kutembelea PSG, kuingia mazoezini au popote pale

Messi hataki utani na taifa lake.
Screenshot_20210812-171000_GBInsta.jpg
 
Asilimia 90% ya aina zote za ndege wanakuwa na mke"Mpenzi" mmoja lakini ku - cheat (kuchepuka) ni kawaida.

Hivi ni Kiumbe gani duniani hakiwezi kuchepuka!!?View attachment 1889703
Mimi peke yangu ndio huwa sichepuki , kwani inahusika hata kama huwa siingizi yote naweka kichwa tu?

Huwa wanasema njiwa wa kufugwa hachepuki lakini sina hakika na hilo.
 
Kuna Mtoto wa Lionel Messi, anaitwa Mateo huyu wa chini karibu na Mama yake, huyu anapenda kupinga kila kitu cha Baba yake

Mfano anaweza kukosa penati ila yeye akashangilia, anaweza kuwa timu nyingine na yeye akawa timu nyingine

Ajabu hapo wapo PSG ila yeye ipo siku atashabikia Lyon, yani ni mpingaji tu

Mwenyewe Messi anasema bado ni Mtoto haelewi kitu
Screenshot_20210812-171209_GBInsta.jpg
 
Pluijm afunguka kuwapeleka Yanga FIFA
.
Aliyekuwa kocha wa Yanga, Mholanzi Hans Van Der Pluijm amethibitisha kuwa amejipanga kuwafungulia mashitaka klabu ya Yanga kwa Shirikisho la Soka Duniani FIFA kuhusiana na madai ya stahiki zake.
.
Pluijm amesema: "Taarifa za za mimi kuwa kwenye mpango wa kuwapeleka Yanga FlFA ni za kweli, lakini nisingependa kuzungumza sana kuhusu suala la kesi hii kwa sasa, kwakuwa kuna wawakilishi wangu ambao wako Dar es Salaam kwa sasa wanashughulikia kesi hii."
.
Inaripotiwa kuwa kocha huyo anawadai dola 50,000 (Sh milioni 115).
.
Screenshot_20210812-171925_GBInsta.jpg
 
HISIA ZA EDO KUMWEMBE: ONGEZEKO LA WAKONGO LIGI KUU
.
Wachezaji kutoka DR Congo wana maarifa uwanjani. Kifupi ni kwamba wana vipaji. Lakini hata sisi si tuna vipaji? Ndio, tena vikubwa. Wachezaji karibu wote wa Tanzania wana vipaji. Tofauti ni kwamba juu ya vipaji vya wachezaji wetu Wakongo wao wameongeza matumizi ya nguvu. Ni kitu ambacho kitawatofautisha wachezaji wetu na wale wa nje kwa muda mrefu.
.
Sijui tunakosea wapi lakini ukweli ni kwamba licha ya ubishoo wao nje ya uwanja lakini wachezaji wa DR Congo wana matumizi makubwa ya nguvu na wanapania wanapocheza soka. Congo haina wachezaji legelege.
.
Nje ya uwanja wachezaji wa DR Congo ni mabishoo. Wanapenda kuvaa hereni, kusuka nywele, kuongeza rangi katika miili yao na mengineyo. Wakiingia uwanjani wanapiga kazi kuliko wachezaji wetu ambao wengi wao ni legelege. Sielewi tatizo linaanzia wapi. Ndivyo tulivyozaliwa? Hapana. Zamani tulikuwa na kizazi cha kina Athuman China na wengineo. Walikuwa wana vipaji vikubwa vya mpira lakini matumizi yao ya nguvu pia yalikuwa juu.
.
Leo wachezaji wenye matumizi ya nguvu nchini wamepotea. Wengi wamebakiza vipaji tu.
.
Mnakubaliana na LEGEND wazawa wamezidi kuwa legelege __!!
Screenshot_20210812-172932_GBInsta.jpg
 
“Moloko ni mchezaji mzuri sana, mashabiki wala wasidhani kuna kitu kitapungua ataendeleza pale nilipoishia namjua vizuri nimecheza naye tukiwa Vita naona klabu imepata mtu sahihi sana.”
.
“Timu ya Yanga sasa wamefanya usajili mzuri sana,kabla sijaondoka nilikutana na bosi mkubwa wa GSM akaniambia anataka kutengeneza timu bora sana kwa msimu ujao na sasa naona kutakuwa na moto pale.”
.
- Tuisila Kisinda.
Screenshot_20210812-173256_GBInsta.jpg
 
Zlatan Ibrahimovic:

"PSG haikumsajili Messi, Messi ameisajili PSG, angalia tu Mataji aliyoshinda Messi na ulinganishe na PSG, hiyo inakuambia mengi kuwa Messi ni mkubwa mara 10 kuliko hiyo klabu. ”
.
Unakubali na Zlatan? Ndio au Hapana __?
Screenshot_20210812-173422_GBInsta.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom