Makapuku Forum

Makapuku Forum

Wazazi wa watoto wanaosoma Shule ya Msingi Imanga katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, wamezuka shuleni hapo kwa madai ya kuhoji sababu za wanafunzi kupewa chanjo dhidi ya corona bila kupewa taarifa.

Hata hivyo, Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Carlos Mabula amesema leo Jumatano Agosti 11 kuwa wazazi hao waliandamana na kufika shuleni hapo huku wakiwa na hasira ya kudhani ugeni uliofika shuleni hapo ni kwa ajili ya kuchoma chanjo wanafunzi wa shule hiyo.


Screenshot_20210811-150327_GBInsta.jpg
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemkutana kesi ya kujibu aliyekuwa mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), Dickson Maimu na wenzake wanne na hivyo wanatakiwa kuanza kujitetea.

Maimu na wenzake wanne wanakabiliwa na mashtaka 55 yakiwemo ya kutakatisha fedha na kuisababishia Serikali hasara ya Sh1.175 bilioni.
Screenshot_20210811-150910_GBInsta.jpg
 
Ukistaajabu ya Mussa utajaona ya Firauni msemo huu unajihirisha baada ya kauli ya Onesmo Mbasha ambaye ni mmoja wa vijana wanaouza bidhaa mbalimbali zitokanazo na wanyama zikiwemo sehemu za uzazi za ng'ombe dume zinazojumuisha uume na korodani.
Screenshot_20210811-151118_GBInsta.jpg
 
Mpaka sasa Barcelona wapo kwenye 95% ya mishahara, wanapambana kuona namna gani wataliingiza jina la Memphis Depay kwenye mfumo maana mshahara unaweza kuvuka hizo 5% zilizosalia

Rais Joan Laporta, alikuwa na mipango kadhaa kuokoa jahazi

-European Super League, imesalitiwa na waoga, wamebaki wao watatu tu

-Dili la mkopo wa CVC Media Partners halina maslahi litaiweka klabu kwenye hasara ya muda mrefu

Zimesalia njia mbili pekee hatarishi ambazo tunasubiri atachukua ipi

Mosi, kuuza sehemu ya haki za La Masia na majengo kadhaa ya klabu ili kubalance vitabu

Pili, kuuza baadhi ya wachezaji tegemezi ili kutunisha mfuko ambao ni Pedri, Frank De Jong yoyote kati yao, japo hii ni ngumu sana kufanyika

Tatu, ni Wachezaji kukubali kuendelea kupunguza mishahara yao ili kuisaidia klabu! Hii ndio njia inayojadiliwa zaidi mpaka sasa

Bado mapambano yanaendelea wakati LA LIGA inakaribia kuanza

BARCELONA wana hali ngumu sana
Screenshot_20210811-151559_GBInsta.jpg
 
MBAPPE NA REAL MADRID| MADRID, SPAIN

Hakuna maelewano mazuri kati ya Viongozi wa Real Madrid na PSG mpaka sasa, PSG wakiwashutumu Madrid kumlaghai kijana na ndio sababu amegoma kusaini mpaka sasa

Taarifa za leo asubuhi ni kuwa, msimamo wa Mbappe upo palepale licha ya Messi kusainiwa ila yeye anahitaji kuondoka kujiunga na Real Madrid

Mbappe yupo wazi kuwa hawezi kusaini mkataba mpya, kama hauzwi basi ataondoka bure mwishoni mwa msimu

Mpaka sasa Madrid hawana presha yoyote, PSG waamue wao wachukue pesa au Madrid wachukue mtu wao bure
Screenshot_20210811-151846_GBInsta.jpg
 
Soka la Hispania lipo chini ya Shirikisho lao la soka RFEF, ambao wao wana LA LIGA kama chombo huru kinachosimamia Ligi kuu na Daraja la kwanza

Sasa kutokana na uhuru huo LA LIGA chini ya Javier Tebas wana mambo mengi wanafanya kinyume na mitazamo ya wengi, huku wakisema ni kibiashara zaidi

Uliwahi kutokea mgogoro wa kwanza kati ya Shirikisho na LA LIGA kuhusu kuweka mechi siku za juma, kama Jumatatu na Ijumaa, wakafikishana mpaka Baraza la michezo la Hispania

Sasa mgogoro wa sasa ni mkataba wa LA LIGA ana CVC Media Partners, ambapo La Liga wanataka kuwauzia 10% ya hisa ili wasimamie haki za kurusha ligi yao, huku wakitoa pesa nyingi

Bahati mbaya sana Rais Perez wa Real Madrid alikuwa wa kwanza kushtukia mpango huo kuwa hauna faida kwa klabu! Kwakuwa wakiuza haki zao wataingiza hasara ya Euro 800 Million kwa miaka 50 ijayo

LA LIGA wao wanasema ni mpango wa kusaidia klabu kujikwamua kiuchumi ila klabu kama Real Madrid na Barcelona wamegoma, wanasema ni mpango wa muda mfupi kiuchumi ila hasara ya muda mrefu

Kwa pamoja Real Madrid na Barcelona wamegoma kuubariki mkataba huo na wamesema ikitokea wamesaini LA LIGA basi wao wataondoa rasmi mechi zao kurushwa kwenye TV

Na leo taarifa rasmi kutoka Shirikisho la soka Hispania limesema mkataba huo ni batili na hawautambui! Hivyo Madrid na Barcelona wana support ya Shirikisho la soka
Screenshot_20210811-152023_GBInsta.jpg
 
Sawa mpo busy na Messi lakini haibadilishi ukweli kuwa beki mwenye kombe la dunia, RAPHAEL VARANE yupo Manchester United

Mkimalizana na issue za Messi njooni mna msala wenu huku wakina Werner, Auba Mane
Screenshot_20210811-152142_GBInsta.jpg
 
LIONEL MESSI| PARIS, FRANCE

Ilipotimu saa sita usiku jana kwa saa za Afrika Mashariki, PSG waliweka jezi ya Messi kwenye website na tayari kuiuza online

Ilipofika saa saba usiku kwa saa za Afrika Mashariki, tayari wameuza jezi 250,000 ndani ya saa moja tu

Nilinunua jezi Paris ya PSG mwaka juzi, kwa EURO 100 hapo hesabu nyepesi zaidi ni kuwa wameingiza EURO MILLION 24 ndani ya saa moja tu
Screenshot_20210811-152319_GBInsta.jpg
 
LIONEL MESSI| PARIS, FRANCE

Baada ya Lionel Messi kutambulishwa kama Mchezaji mpya wa PSG, ile account rasmi ya Twitter ya LIGUE 1, imeongezeka followers zaidi ya 11,405 ndani ya masaa machache sana

Admn akapost kuwakaribisha Followers wapya na kujipongeza
Screenshot_20210811-152427_GBInsta.jpg
 
Wachezaji wa Manchester United siku ya jana walihudhuria hafla ya chakula cha pamoja kwenye hotel ya IVY jijini Manchester

Pichani ni baadhi ya wachezaji wakati wanawasili, Jadon Sancho, Paul Pogba na Donny Van de Beek

Pogba kwenye masuala ya kuvaa na camera tena, mbona mtachoka nyinyi ndugu yetu kutoka Guinea hapo
Screenshot_20210811-152554_GBInsta.jpg
Screenshot_20210811-152615_GBInsta.jpg
Screenshot_20210811-152632_GBInsta.jpg
 
SPORTS TOURISM| Huu ndio utalii kupitia michezo wenzetu hapo Rwanda wameweka pesa pale PSG na Arsenal pia

Tazama Lionel Messi amevaa jezi yenye VISIT RWANDA, Mbappe huwa anavaa, Neymar na Mastaa wengine wengi

Mileage kwa Rwanda, ni wazi kila mtu atahitaji kujua RWANDA ni nini, ipo wapi na kuna nini? Ndipo hapo watu husafiri, Exploring and expedition

Bingo hii, mileage kali sana hii
Screenshot_20210811-152851_GBInsta.jpg
 
Wakati nyota wa NBA, Stephen Curry alipotembelea Paris mwaka juzi alipiga picha na uzi wa PSG ukiwa na namba 30 mgongoni ambayo ndio namba yake pale Golden State Warriors

Na sasa PSG imemsaini Messi, ambae atatumia namba 30

Lionel with Stephen Curry esque
Screenshot_20210811-153058_GBInsta.jpg
 
Gomes mtu sana... mwana kulitafuta hakuwa tena na sehemu ya kwenda baada ya WANANCHI kutia ngumu kumrudisha

Ajibu anatarajiwa kuondoka kesho kwenda Morocco kuungana na msafara wa nyota wengine walioondoka jana Jumanne.
Screenshot_20210811-153321_GBInsta.jpg
 
MSAFARA WA SIMBA MOROCCO
.
Wachezaji walioondoka jana ni kipa Aishi Manula, Mohamed Hussein, Beno Kakolanya, Kennedy Juma, Mzamiru Yassin, Erasto Nyoni, Meddie Kagere, Hassan Dillunga, Gadiel Michael, Benard Morrison, Clatous Chama, Perfect Chikwende, Shomari Kapombe, Thadeo Lwanga, Rally Bwalya, Jonas Mkude, Joash Onyango na Peter Banda.
.
Msafara wa wachezaji ni 18, uliongozwa na Gomes, msaidizi wake Seleman Matola,meneja Patrick Rweyemamu uliondoka jana huku kundi lingine la wachezaji litakaloongozwa na nahodha John Bocco likiondoka kesho Alhamisi.
Screenshot_20210811-153542_GBInsta.jpg
 
Grealish aahidi taji la Uefa Etihad
.
Wahenga wanasema usitoe ahadi wakati ukiwa na furaha. Sasa Jack Grealish mwana kulitaka na mashabiki wa Manchester City watamsikilizia tu atakachokifanya msimu ujao.
.
Kiungo huyo mshambuliaji amesema ana furaha kubwa kuwa mchezaji wa kwanza kwenye Ligi Kuu England kusajiliwa kwa Pauni milioni 100, katikati ya furaha hiyo akawaambia mashabiki wa Man City atafanya kila analoweza kuhakikisha miamba hiyo ya Etihad inabeba ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.
.
Grealish, 25, amesema: "Hapana hii kitu hainipi presha. Nimetazama kwenye vyumba vyetu vya kubadilishia kuna wachezaji wengi sana wenye vipaji na uwezo, hivyo nina amini tutashinda taji hilo la Ligi ya Mabingwa."
Screenshot_20210811-153646_GBInsta.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom