MIKONO YA KIHAMU @jr_farhanjr
Duniani kote Matajiri wakiwekeza kwenye timu ni ngumu kuwapa nafasi watu wa mpira moja kwa moja kwenye utendaji haswa mambo ya kifedha
Matajiri wanajihisi huru pale ambapo anakuwepo Afisa anaesimamia mambo, akiamini hawezi kumpigisha shoti bali kumpa taarifa sahihi
Watu walishawahi kukosoa Engineer Hersi pale Yanga kuwa na nguvu kubwa licha ya kuwa ni Mjumbe tu, lakini watu wanasahau ni Mkurugenzi wa Uwekezaji pale GSM ni mtu wa Boss
Watu waliwahi kuhoji uwepo wa Barbra pale Simba, wakasema hana analojua kuhusu mpira ndio inaweza kuwa sahihi lakini Boss ndie mtu anaemuamini, atapigania maslahi ya timu na yake binafsi
Hii sio Tanzania tu bali duniani kote! Maboss wanahitaji watu wao
Mfano Manchester United ile familia ya Glazer's ilimuamini sana Ed Woodward, Mtendaji na Mwandamizi kwenye masuala ya kiuchumi, watu walisema hana analojua kuhusu mpira lakini vitabu vilibalance sana
Mfano PSG wana Nasser El Kherrafi, yule sio Mmiliki wa timu bali ni Mwenyekiti na CEO wa timu, ni mtu wa karibu na Mmiliki wa PSG anaitwa Tamim Bin Hamad Al Thani, ila Nasser anasimamia kutokana na kusimamia projects nyingi za Boss
Mfano Chelsea wana Marina Granovskaia, hakuwahi kuushi mpira alikuwa Msimamizi wa biashara za Roman Abramovich, ila Tajiri alitaka Mtu wa kulinda maslahi yake, akamleta kwenye mpira, itazame Chelsea sasa kibiashara ni hatari
Huwezi kuwekeza kwenye mpira na ukaacha utendaji kwa Mtu ambaye sio wako, utalia kilio cha mbwa meno nje! Watu wa Maboss ni watu sahihi kulinda maslahi duniani kote