Mfahamu nyota wa soka Cristiano Ronaldo uwanjani yumo, na kwa wanawake yumo.
Ukitaja wanasoka mahiri wawili wa kizazi cha sasa duniani, jina la Cristiano Ronaldo lazima liwepo kwenye orodha hiyo, ama litakuwa la kwanza ama la pili, inategemea na tafsiri ya anayeweka orodha hiyo kati yake na Lionel Messi.
Cristiano Ronaldo Dos Santos Aveiro alizaliwa mwaka Februari 5, mwaka 1985 huko Funchal katika visiwa vya Madeira, kwa mama Maria Doroles Dos Santos Aveiro na marehemu baba yake Jose Dinis Aveiro.
Alipozaliwa tu baba yake akampatia jina la Ronaldo akimuona kama Ronald Reagan (Rais wa Marekani) ajae.
Wakati huo baba yake hakuwa na wazo kabisa kuhusu mwanae kuwa mwanasoka, alimpenda sana Rais Reagan, ambaye wakati Ronaldo anazaliwa ndio alikuwa ametoka kuapishwa kuwa rais katika awamu yake ya pili ya uongozi.
Kama si daktari almanusura mama yake aitoe mimba yake leo soka lisingekuwa na Ronaldo na lisingekuwa na mfungaji mahiri wa aina yake.
Tafiti zinaonyesha nyota huyo wa kiataifa wa Ureno ana asili ya Afrika Magharibi