Makapuku Forum

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza masharti mapya ya kupambana na Corona ambapo amesema ni marufuku kwa Watu kutembea usiku kuanzia saa moja usiku hadi 11:30 alfajiri.

“Watu wote wanapaswa kubaki Majumbani, wanaoruhusiwa kutembea usiku ni Watu wa Ulinzi na Usalama na makundi mengine yaliyopewa ruhusa”

“Baa zitaendelea kufungwa na Askari wanapaswa kuwakamata na kuwatoza faini Wamiliki wa Baa wanaokiuka agizo” ———Museveni.

“Bodaboda wanaruhusiwa kufanya kazi ila mwisho ni saa 12 Jioni na wanapaswa kubeba abiria mmoja (sio mshikaki) au mizigo” ———Museveni.
Screenshot_20210801-210847_GBInsta.jpg
 
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kesho August 2 2021 anatarajiwa kuanza ziara rasmi ya Kiserikali ya siku mbili Nchini Rwanda kwa mwaliko wa Rais wa Nchi hiyo Paul Kagame.

Akiwa Nchini humo pamoja na mambo mengine atafanya mazungumzo rasmi na Mwenyeji wake Rais Paul Kagame kisha atashuhudia utiaji saini wa hati za makubaliano na kuzungumza na vyombo vya habari, ziara hii inalenga kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano kati ya Rwanda na Tanzania.
Screenshot_20210801-211012_GBInsta.jpg
 
“Zoezi la chanjo litaanza kutolewa kesho kuna Vituo kama 550 vilivyoandaliwa, chanjo hizi hazijaleta madhara kwa waliotumia kama tulivyokuwa tunasikia na chanjo hizi zitaendelea kuletwa baada ya zile dozi milioni 1 kuna nyingine zitaendelea kuletwa”

“Kuna upotoshaji unaoenezwa mitandaoni naomba Waandishi tuoneshe weledi, tusijiingize kwenye huu upotoshaji wa kuwatisha Watanzania, Serikali imeamua chanjo iwe hiari sasa tusiwashinikize Watanzania wakahiari kutokuchanja tuwaache wenyewe waamue”

“Serikali pia inawasisitiza Wananchi kwenye suala la chanjo tujitahidi sana kuwasikiliza Wataalamu badala ya kumsikiliza kila Mtu, tatizo tulilonalo sasa hivi kila mmoja amejivisha Utaalamu, kila mmoja anaijua Corona, tuwasikilize Wataalamu”

“Msimamo wa Serikali ni kwamba shughuli ziendelee kama kawaida lakini Watu wachukue tahadhari, Wizara ya Afya imeandaa Mdahalo kesho pale Muhimbili wale wote wenye hoja waende wakatoe hoja zao watajibiwa, hoja inajibiwa kwa hoja” ——— Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania Gerson msigwa
Screenshot_20210801-211205_GBInsta.jpg
 
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kesho August 2 2021 anatarajiwa kuanza ziara rasmi ya Kiserikali ya siku mbili Nchini Rwanda kwa mwaliko wa Rais wa Nchi hiyo Paul Kagame.

Akiwa Nchini humo pamoja na mambo mengine atafanya mazungumzo rasmi na Mwenyeji wake Rais Paul Kagame kisha atashuhudia utiaji saini wa hati za makubaliano na kuzungumza na vyombo vya habari, ziara hii inalenga kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano kati ya Rwanda na Tanzania. View attachment 1876762
Safi sana
 
“Kuna kiwanda kinajengwa pale MSD ambacho kitazalisha barakoa milioni 86 kwa siku ni barakoa nyingi sana”

“Serikali inaendelea kukamilisha viwanda vya kuzalisha dawa vilivyopo Makambako kule Njombe kunajengwa viwanda vinne, kuna cha kutengeneza dawa za maji, dawa za vidole vile vya rangi mbili, vidonge vya kawaida na mipira ile ya kuvaa Serikali itaokoa Bilioni 33 ambazo tungetumia kwa kuagiza dawa ndani na nje ya Nchi”

“Nchi zote zitasaidiwa chanjo kwa idadi ya 20% ya Watu wake, kwahiyo Tanzania kupitia mpango huu wa kusaidiwa chanjo tutapata takribani chanjo milioni 11, kwahiyo zilizokuja hizi zaidi ya milioni 1 ni sehemu ya mpango wa COVAX Facility chini ya WHO” ——— Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson msigwa leo Dar es salaam, ingia youtube ya ‘millardayo’ kutazama kwa urefu zaidi.
Screenshot_20210801-211454_GBInsta.jpg
 
"Kwenye kuchonganishachonganisha mwingine jana kasambaza kabango jamani Gwajima kajiuzulu Ubunge, mlikaona kabango kale? kauongo.. ka wale wachonganishichonganishi haina uhusiano"

"Uhusiano ni kwamba mimi ni aina ya Mtu ambae nikisema hivi leo, nitasema hivyo kesho, kesho kutwa wiki ijayo, nyinyi ambae mnabadilikabadilika na nyie mmebarikiwa kwa aina yenu, mimi sina uwezo huo" ——— asema Askofu Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima ambae pia ni Mbunge wa Kawe Dar es salaam.
Screenshot_20210801-211847_GBInsta.jpg
 
Askofu Josephat Gwajima leo amewaongoza maelfu ya Waumini wa Kanisa la Ufufuo na Uzima kumuombea Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais Dr. Philiph Mpango, Waziri Mkuu Majaliwa Kassim na Viongozi wengine pamoja na Wananchi mmojammoja dhidi ya corona, maombi haya yamefanyika Kanisani kwake Ubungo Dar es salaam.
Screenshot_20210801-212915_GBInsta.jpg
 
"Corona ipo, nina-support misimamo ya afya ndio maana pale nje (Kanisani) kuna mabomba zaidi ya 50 na sabuni kabisa kabla hujaingia na ukitoka unanawa, ishu yangu tu ni kuchanjwa kwa Watu wa familia yangu hiyo hapana na hiyo hainifanyi nikawa adui wa Mtu"

"Nam-support Mwenyekiti wangu (Rais Samia Suluhu Hassan) kwa asilimia 100, kila Mtu anayependa kuchanja atachanjwa na wasiotaka kuchanjwa waheshimiwe kwa sababu kamati imependekeza hivyo hata hapa ukijisikia kwenda kuchanjwa kachanjwe sikuzuii” ——— Askofu Gwajima.

"Msimamo wa Rais Samia aliouchukua ni msimamo wa Kiongozi wa Nchi ambao Rais yeyote duniani lazima auchukue, Watu waache kumshambulia kwa maneno”——— Askofu Gwajima.
Screenshot_20210801-213101_GBInsta.jpg
 
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema kimepokea kwa masikitiko barua ya kujiuzulu kwa Mbunge Mteule wa CCM Jimbo la Konde Sheha Mpeka Faki leo August 02, 2021.

“Katika barua ya Sheha ameeleza kwamba amefikia uamuzi huo kutokana na changamoto za kifamilia jambo ambalo Chama hakina uwezo wa kumzuia hasa ikizingatiwa kwamba ni haki yake ya msingi kama ilivyo kwa haki ya kuomba ridhaa ya kugombea nafasi ndani ya CCM” ———Shaka Hamdu Shaka, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.

Sheha Faki amejiuzulu siku chache tu baada ya kutangazwa Mbunge mpya na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) baada ya kushinda uchaguzi uliofanyika Jumapili 18 Julai 2021.
Screenshot_20210802-132028_GBInsta.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom