Makapuku Forum

Makapuku Forum

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Simon Sirro akichoma chanjo ya corona leo IKULU Dar es salaam.
Screenshot_20210728-181408_GBInsta.jpg
 
Ameandika Haji Manara:

Kila tunapomaliza Mechi yoyote ile ya Simba,neno langu la kwanza baada ya matokeo yoyote yale ni Alhamdulillah

Kwa wanaofuatilia page hii wanatambua hilo.

Kwangu neno hili ndio Msamiati nnauotumia mara nyingi zaidi na hufanya hivi kwa kila jambo, liwe jema au baya

Yes neno langu ni moja tu

AL-HAMDULILLAH
Screenshot_20210728-181547_GBInsta.jpg
 
Mtoto wa Mtangazaji Masoud Kipanya aitwae Malcom Ally amefariki leo Dar es salaam, msiba utakuwa Mlimani City pembeni ya jengo la Mwenge Tower na maziko yanatarajiwa kufanyika kesho makaburi ya Kisutu DSM saa saba mchana.
RIPMalcom
Screenshot_20210728-193832_GBInsta.jpg
Screenshot_20210728-193850_GBInsta.jpg
 
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (CDF) Jenerali Venance Mabeyo, Jaji Mkuu, Shaka, Dr. Abbas na Viongozi wengine ni miongoni mwa waliochoma chanjo ya corona leo IKULU Dar es salaam.
Screenshot_20210728-194516_GBInsta.jpg
Screenshot_20210728-194809_GBInsta.jpg
Screenshot_20210728-194828_GBInsta.jpg
Screenshot_20210728-194847_GBInsta.jpg
 
Club ya Yanga SC imetangaza kuachana na beki wake wa kati wa kimataifa Ghana na nahodha wao Lamine Moro baada ya kuwatumikia katika kipindi cha miaka miwili, Lamine anakuwa staa wa pili wa kimataifa Yanga kuondoka baada ya Haruna Niyonzima kutokea Rwanda…. “kwa pamoja pande zote mbili tumekubaliana kusitisha mkataba wake”
Screenshot_20210729-131638_GBInsta.jpg
Screenshot_20210729-131720_GBInsta.jpg
 
Kamanda wa Kamandi ya Afrika ya Jeshi la Marekani (AFRICOM) Jenerali Stephen Townsend, alikuwa na ziara ya siku mbili nchini Tanzania, tarehe 27 na 28 Julai, ambapo alikutana na Maafisa Waandamizi wa Jeshi na kufungua mazoezi ya kwanza ya pamoja ya kijeshi ya Nchi hizi mbili tangu mwaka 2017.

“Tanzania imeendelea kuwa Nchi kiongozi Barani Afrika katika nyanja ya usalama na mbia muhimu sana wa Kamandi ya Afrika ya Jeshi la Marekani, Majeshi yetu ya ulinzi yana historia ndefu ya kufanya kazi bega kwa bega, na ziara hii ni kielelezo cha nia yetu ya kuimarisha zaidi ubia huo”———- Jenerali Townsend.

July 28,2021 Jenerali Townsend aliungana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo katika hafla ya ufunguzi ya mafunzo ya pamoja ya kijeshi (Joint Combined Exchange Training – JCET) kati ya Askari wa Vikosi Maalumu vya Jeshi la Marekani na Askari wa Jeshi la Wanamaji la Tanzania katika Chuo cha Ulinzi wa Amani kilichopo Kunduchi.

Mazoezi hayo ya kijeshi ya wiki sita ni ya kwanza ya aina yake kwa Majeshi ya Tanzania na Marekani toka mwaka 2017, Askari wa Kimarekani na wa Kitanzania watakuwa bega kwa bega wakishiriki mafunzo haya ili kuimarisha ujuzi wao katika mbinu za medani kwa kikosi kidogo, ulengaji shabaha, utoaji matibabu, mbinu za kimapambano za kikosi kulingana na maeneo tofauti tofauti(unit maneuver), mafunzo kuhusu sheria za kivita au migogoro ya kivita (Law of Armed Conflict) na jinsi ya kulinda haki za binadamu wakati wa mapambano.
Screenshot_20210729-132248_GBInsta.jpg
Screenshot_20210729-132306_GBInsta.jpg
Screenshot_20210729-132322_GBInsta.jpg
 
Mbunge wa Segerea Bonnah Kamoli amemshukuru Rais Samia Suluhu kwa kutoa Milioni 500 kwa kila Jimbo na kusema kwenye Jimbo la Segerea yeye milioni 500 hizo amezipeleka Kata ya Kipawa kwenye Barabara ya Airport mkabala na Uwanja wa Ndege.

“Nimekagua Barabara hii kwenye Kata ya Kipawa na kiukweli namshukuru sana Rais kwa hizi pesa maana kilio cha Wananchi kuhusu hiyo Barabara ni cha muda mrefu, hatimaye leo tumepata suluhisho” ——— Bonnah Kamoli
Screenshot_20210729-132618_GBInsta.jpg
 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu ametoa siku 7 kwa vyombo vya Ulinzi na Usalama kuchunguza vifo vya wanafunzi 3 waliofariki kwa kufunikwa na kifusi katika Shule ya Msingi Mbori, Kata ya Motondo Wilayani Mpwapwa.

Wakati huo huo Ummy amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kuwaondoa Walimu wote wa shule ya Msingi Mbori kupisha uchunguzi unaondelea.

Waziri Ummy ametoa kauli hiyo wakati aliposhiriki kuaga Miili ya Wanafunzi watatu waliofariki kwenye ajali ya kufukiwa na mchanga katika shule ya Msingi Mbori 27.07.2021 wakibeba mchanga kwa ajili ya kujenga choo.

Akiwa shuleni hapo Waziri Ummy amelaani vikali vitendo vya Walimu kuwafanyisha kazi siziso stahili tofauti na ilivyoelekezwa kwenye Waraka wa Elimu bila malipo No. 3 wa mwaka 2016.

“Hatukatazi Mwanafunzi kufanya kazi zinazomjenga kama vile stadi za kazi lakini sio kumfanya Mwanafunzi kama Kibarua unawezaje kumwambia mtoto akachimbe mchanga wa kujengea au akaponde kokoto tena bila uangalizi wa Walimu??” ——— Waziri Ummy.

“Katika Shule ya Msingi Mbori tumeleta shilingi milioni 12 kwa ajili ya ujenzi wa choo na fedha za mchanga zimejumlishwa humo inakuwaje Waalimu watume Watoto kwenda kuchimba mchanga wa mtoni, kuna uzembe hapa umefanyika na tutachukua hatua”
Screenshot_20210729-133035_GBInsta.jpg
 
“Uchambuzi wa ufanisi wa Halmashauri katika ukusanyaji wa mapato ya ndani, unaonesha Halmashauri 57 zimekusanya kwa 100% au zaidi ya makisio yake ya mwaka,Halmashauri 90 zimekusanya kati ya 80% hadi 99 na Halmashauri 37 zimekusanya kati ya 50% hadi 70”

“Ulinganisho wa ufanisi wa ukusanyaji wa mapato unaonesha kuwa Halmashauri ya Nyang’hwale imeongoza katika Halmashauri zote 184 kwa kukusanya 163% ya makisio yake ya mwaka, ikifuatiwa na Halmashauri ya Mpimbwe 136% na Halmashauri ya Morogoro 133%”

“Halmashauri ya Wilaya ya Mtama imekusanya asilimia 51, Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti asilimia 51 na Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli asilimia 52, Halmashauri hizi zimekuwa za mwisho katika Ukusanyaji wa Mapato ya Ndani”

“Halmashauri 37 zimetumia 100% au zaidi ya kiasi kilichopaswa kutumika, Halmashauri 131 zimetumia kati ya 50% na 99 ya kiasi kilichopaswa kutumika na Halmashauri 16 zimetumia chini ya 50% ya kiasi kilichopaswa kutumika“———Waziri wa TAMISEMI, Ummy Mwalimu akisoma taarifa ya ukusanyi wa mapato na matumizi kwenye Halmashauri 2020/2021, Dodoma
Screenshot_20210730-051045_GBInsta.jpg
 
Kutoka Makaburi ya Kisuti DSM shughuli ya maziko wa mwili wa mtoto wa Masoud Kipanya, Malcom Kipanya makaburi ya Kisutu Dar es salaam.

Katika mazishi haya yamehudhuriwa na watu mbali mbali wakiwemo CEO wa GSM Ghalib Said Mohamed, Mwigizaji Steve Nyerere, Msanii Ommy Dimpoz, Mtangazaji Millard Ayo, Wafanyakazi wa Clouds Media na wengine.
Screenshot_20210730-051637_GBInsta.jpg
 
“Kwa mwaka 2020/2021 Jiji la Mbeya limeongoza kwa kukusanya mapato kwa 102% ya makisio ikifuatiwa na Jiji la Dar es Salaam 99% kisha Jiji la Mwanza 92%, Jiji la Arusha limekuwa la mwisho katika kundi hili ambapo limekusanya 80% ikifuatiwa Jiji la Dodoma 82% na Jiji la Tanga 88%”

“Katika kuzipima Halmashauri zote kwa kigezo cha wingi wa mapato (pato ghafi),Jiji la Dar es Salaam limekusanya mapato mengi zaidi kuliko Halmashauri zote kwa kukusanya Sh.bil 67.09 ikifuatiwa na Manispaa ya Kinondoni bil. 40.7 na Jiji la Dodoma bil.38”

“Kwa mwaka wa fedha 2020/21 Halmashauri zilipanga kukusanya Shilingi bil.814.9 kutoka kwenye vyanzo vyake vya ndani, hadi kufikia Juni, 30 2021 Halmashauri zimekusanya jumla ya Sh. bilioni 757 ambayo ni asilimia 93 ya makisio ya mwaka”———Ummy Mwalimu

“Mapato halisi kwa mwaka wa fedha yameongezeka kwa Shilingi bilioni 40 sawa na asilimia 6 ikilinganishwa na mapato yaliyokusanywa mwaka wa fedha 2019/20 ambayo yalikua Shilingi bilioni 717 kati ya bajeti ya Shilingi bilioni 765.5”———-Waziri wa TAMISEMI, Ummy Mwalimu Dodoma
Screenshot_20210730-051742_GBInsta.jpg
 
“Halmashauri ya Manispaa ya Kahama imeongoza kwa kukusanya mapato kwa 109% ya makisio ikifuatiwa na Manispaa ya Kigamboni 106% kisha Manispaa ya Temeke 105%, Manispaa ya Lindi imekuwa ya mwisho ambapo imekusanya 58% ikifuatiwa na Manispaa ya Tabora 76% kisha Manispaa ya Kigoma 78%”

“Upande wa Miji Halmashauri ya Mji wa Njombe imeongoza kwa kukusanya 131% ya makisio yake ya mwaka ikifuatiwa na Mji wa Kibaha 116% na Halmashauri ya Mji wa Mafinga 108%, Halmashauri ya Mji wa Ifakara imekuwa ya mwisho kwa kukusanya 64% ikifuatiwa na Halmashauri ya Miji wa Korogwe 66%”

“Matumizi katika Miradi ya Maendeleo Taarifa zinaonesha kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa imeongoza kwa kuchangia asilimia 192.3 ikifuatiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru asilimia 166 na Halmashauri ya Wilaya ya Newala asilimia 155 “

“Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu imekua ya mwisho kwa kuchangia asilimia 25.47 ikifuatiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe asilimia 28 na Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli asilimia 28”———-Waziri wa TAMISEMI Ummy Mwalimu Dodoma
Screenshot_20210730-052752_GBInsta.jpg
 
“Makusanyo Ki-Mikoa, Mkoa wa Njombe umeongoza kwa kukusanya asilimia 113 ikifuatiwa na Mkoa wa Geita 107%, Mkoa wa Songwe asilimia 107 na Mkoa wa Lindi umekua wa mwisho kwa kukusanya asilimia 78 ukifuatiwa na Mkoa wa Simiyu 81% na Mkoa wa Singida 82%”

“Matumizi katika Miradi ya Maendeleo Taarifa zinaonesha kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa imeongoza kwa kuchangia asilimia 192.3 ikifuatiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru asilimia 166 na Halmashauri ya Wilaya ya Newala asilimia 155”

“Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu imekua ya mwisho kwa kuchangia asilimia 25.47 ikifuatiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe asilimia 28 na Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli asilimia 28”

“Uchambuzi wa ufanisi wa Halmashauri katuka ukusanyaji wa mapato ya ndani, unaonesha Halmashauri 57 zimekusanya kwa 100% au zaidi ya makisio yake ya mwaka,Halmashauri 90 zimekusanya kati ya 80% hadi 99 na Halmashauri 37 zimekusanya kati ya 50% hadi 70” ———-Waziri wa TAMISEMI, Ummy Mwalimu Dodoma
Screenshot_20210730-052953_GBInsta.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom