Kampuni za kutengeneza chanjo ya COVID-19 za Pfizer na Moderna zimepandisha bei ya chanjo katika mikataba yake mipya ya mauzo na Umoja wa Ulaya ambapo Ripoti mpya iliyochapishwa na gazeti la Financial Times iliyotolewa leo Jumapili imenukuu sehemu ya makubaliano hayo ikisema bei mpya ya chanjo ya Pfizer imepanda hadi euro 19.50 (Tsh. 52,288) kutoka euro 15.50 za awali (Tsh. 41,280).
Gazeti hilo limeripoti kuwa dozi ya chanjo ya Mordena iliyokuwa ikiuzwa dola 25.50 (Tsh. 59,117) itauzwa dola 28.50 (Tsh. 66,078) kwenye makubaliano hayo mapya na hii ni kutokana na ongezeko la mahitaji ambapo baada ya bei hizi kupanda juhudi za shirika la habari la Reuters za kupata tamko kutoka kwa kampuni ya Pfizer na Moderna hazikufanikiwa.
View attachment 1877265