Waziri wa TAMISEMI, Ummy Mwalimu ameitaka Jamii iache kuwa na dhana potofu kwamba Mtu akionekana amebeba kondomu ni muhuni bali Jamii ijifunze kujilinda na maambukizi yatokanayo na ngono zembe ambazo zimekua zikiharibu maisha ya Watu.
Ummy ameyasema hayo Dodoma alipokuwa anazindua uwekaji wa makasha ya kusambazia kondomu maeneo ya Watu na maeneo yenye mikusanyiko ambapo ameeleza kwamba takwimu zinaonesha kwa mwaka takribani Watu Elfu 72 wanaambukizwa virusi vya UKIMWI nchini Tanzania.
Waziri Ummy amewaagiza Watendaji wa TAMISEMI kwa kushirikiana na TAYOA kuhakikisha wanasambaza makasha hayo na kutoa elimu ya kujikinga na maambukizi ya UKIMWI hadi Vijijini ambapo baadhi ya jamii haina uelewa wa kutosha kuhusu ugonjwa huo.
Makasha hayo tayari yamefika kwenye Halmashauri 169 kati ya Halmashauri 184 kwa Tanzania Bara.
View attachment 1876737