Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20210722-105320_AppLock.jpg
Screenshot_20210722-105349_Opera%20Mini.jpg
 
Anna Mghwira ambae aliwahi kuwa Mgombea Urais kwa ticket ya ACT Wazalendo mwaka 2015 na baadae kuteuliwa kuwa RC Kilimanjaro amefariki, mmoja wa Ndugu zake ameiambia AyoTV kwamba amefia Mount Meru Hospitali Arusha na kwa siku 5 amekua akiingizwa ICU na kutolewa.
RIPMamaAnnaMghwira
Screenshot_20210722-151216_GBInsta.jpg
 
Vyombo vya Usalama nchini Magascar vimesema vimefanikiwa kuzima jaribio la mauji ya Rais wa Nchi hiyo, Andry Rajoelina .

Watu zaidi ya sita wakiwemo Raia wawili wa Ufaransa wamekamatwa wakihisiwa kuhusika kupanga njama za mauaji ya Rais huyo.

Kumekuwa na ripoti kadhaa za Marais wa Mataifa mbalimbali kushambuliwa siku za hivi karibuni, mapema Mwezi huu Rais wa Haiti Jovenel Moise aliuawa akiwa kwenye makazi yake na pia juzi Rais wa Mpito wa Mali, Assim Goita alishambuliwa na Wanaume wawili mmoja akiwa amebeba kisu baada ya kumaliza Ibada ya Sikukuu ya Eid Al-Adha Msikitini, Bamako.
Screenshot_20210722-151353_GBInsta.jpg
 
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi(CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amepata chanjo ya kwanza ya kujikinga na ugonjwa wa Corona leo Jumatano July 22,2021 katika Clinic ya Umoja wa Mataifa iliyopo Masaki.

Lipumba amesema amepata nafasi hiyo kupitia kwa Mke wake Gojina Mtenga anayefanya kazi Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na Watoto Duniani( UNICEF), Cox Bazaar nchini Bangladesh.

“Wenzetu wa Mashirika ya Kimataifa wameruhusiwa kuanza kupata chanjo hizi pamoja na Familia zao na Mimi kupitia kwa Mke wangu ndio imeniwezesha leo kuja kupata chanjo hii hapa na nilipata taarifa usiku wa jana ikinitaka nifike hapa leo saa tano asubuhi nashukuru kwa kulikamisha hili”

“Baada ya chanjo hii ya kwanza nanatakiwa kurudi tena baada ya wiki sita mpaka nane kupata chanjo ya pili ili kukamilisha chanjo nzima ya kujikinga ya kujikinga na Corona, niwaombe Wananchi wachangamkie chanjo hii ili wawe salama” ——— Lipumba.
Screenshot_20210722-151519_GBInsta.jpg
 
China imesema haitowaruhusu Maafisa wa Shirika la Afya Ulimwenguni, WHO kufanya awamu ya pili ya uchunguzi kuhusu chanzo cha maradhi ya COVID-19 kwenye maabara za China, Naibu Mkuu wa Tume ya kitaifa ya afya nchini China Zeng Yixin amesema hayo hii leo na kuongeza kuwa mpango wa WHO umejaa lugha ambayo haiheshimu misingi ya sayansi.

Zeng amepuuzia mbali pia nadharia kwamba virusi hivyo vilitokea kwenye maabara za Wuhan Mji ambako viligunduliwa kwa mara ya kwanza na kuongeza kusema kwamba Maabara hizo hazina virusi vinavyoweza kumuathiri Mwanadamu moja kwa moja.
Screenshot_20210722-192914_GBInsta.jpg
 
"Mkoa wetu wa Mwanza ulipiga marufuku mikusanyiko isiyo ya lazima mpaka Watu wawe na vibali maalum cha mikusanyiko hiyo, bahati mbaya Viongozi na Wanachama wa CHADEMA walikua wameandaa kongamano la kile kinachoitwa madai ya kudai Katiba mpya, walizuiliwa wasikusanyike bila kibali na hawakutaka kufata kibali hicho hivyo Polisi lilizuia kusanyiko hilo na wengi wao kweli hawakufika isipokua kulikua na wachache walijaribu kufika na wenyewe walikamatwa na kuja kuhojiwa"

"Jumla ya Watu 15 walikamatwa pale Hotelini na sasa hivi tunawashikilia kwa mahojiano zaidi, mwanzoni Jeshi la Polisi lilipata taarifa kwamba mkusanyiko ule ungeleta vurugu na uvunjifu wa amani kwasababu baadhi yao walipanga kufanya vitendo vya uhalifu zaidi ya kukusanyika pia kulikua na katazo la maambukizi ya covid-19 vilevile kulikua na taarifa kwamba kulikua na vitendo vya uvunjifu wa amani tukalazimika kuvunja mkutano ule usifanyike na bahati nzuri wengi wengi kabisa walituelewa"

Jeshi la Polisi linafanya kazi zake kwa mujibu wa sheria ambazo zimewekwa na hatuna upendeleo kwa Mtu, Chama au Taasisi yoyote kwahiyo madai kwamba kuna Chama chochote cha kisiasa tunakibeba hakuna au kuna Chama tunakionea hakuna, yeyote anaetaka kufanya shughuli za kisiasa afate taratibu za Nchi hii na ataruhusiwa, kama hawezi kufata taratibu sheria itachukua nafasi yake” ——— RPC Ng’azi akiongea leo Mwanza baada ya Viongozi wa CHADEMA na Wafuasi jumla 15 kukamatwa jana.
Screenshot_20210722-193323_GBInsta.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom