Makapuku Forum

Makapuku Forum

20210510_064718.jpg
20210510_064903.jpg
 
Mchezo wa VPL Na. 259 (Simba vs Coastal Union) uliopangwa kuchezwa Mei 11, 2021 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, umeahirishwa na utapangiwa tarehe nyingine kwasababu Simba inalazimika kusafiri siku hiyo kwenda A. Kusini kwa ajili ya mchezo wa CAFCL dhidi ya Kaizer Chiefs Mei 14.
20210510_163901.jpg
 
Watu wawili ambao wametoka gerezani hivi karibuni kwa msamaha wa Rais Samia Suluhu wameuawa na Wanachi wenye hasira kali baada ya kukamatwa wakidaiwa kuiba vitu mbalimbali Kibaha mkoani Pwani.

Watu hao ni Ramadhani Mohamedi maarufu Seven au Ali (28) na Idd Hamisi maarufu Chuga (30) wote wakazi wa Kibaha na walifungwa kwa makosa ya wizi kabla ya kupata msamaha wa Rais Aprili 12 mwaka huu kutoka katika gereza la Mkuza lililopo Kibaha.

RPC wa Pwani Wankyo Nyigesa ametoa taarifa leo May 10, 2021 na kusema Watu hao wameuawa juzi May 08,2021 kwa kupigwa na mawe, mapanga na fimbo wakituhumiwa kuiba.

“Niwasihi Wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi kwa kisingizio cha hasira na badala yake watoe taarifa Polisi inapotokea tukio la wizi kwenye maeneo yao, ili watuhumiwa wakamatwe na kufikishwa katika vyombo vya sheria”———RPC Pwani
20210510_164120.jpg
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaomba Viongozi wa Dini katika mahubiri yao waweke msisitizo katika masuala ya kuwekeza kwa Vijana ikiwa ni pamoja na kukemea vitendo vyote hatarishi visivyozingatia maadili ya Mtanzania.

“Tusisahau pia kwamba UKIMWI bado upo, Vijana wengi wapo katika hatari ya kupata maambukizi, kwa msingi huo, tumieni nafasi yenu katika jamii kutoa ushauri nasaha na hatimaye kupunguza kasi ya maambukizi kwa Vijana”———MAJALIWA

Ameyasema hayo jana Jumapili, Mei 9, 2021 katika ibada ya kusimikwa kwa Askofu Dkt. Msafiri Mbilu, Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Lushoto, Waziri Mkuu ameshiriki ibada hiyo kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Amesema Serikali inatambua na kuthamini kazi na majukumu makubwa ya Viongozi wa Kanisa ambayo ni pamoja na kuwaongoza Watu kiroho na kuwapa mafundisho, ushauri na kuwajenga kiimani.

Waziri Mkuu pia ametumia fursa hiyo kuwaomba viongozi hao waendelee kutoa mafundisho yenye kuhimiza wananchi wadumishe amani na utulivu nchini kwa manufaa ya vizazi vya sasa na ya vizazi vijavyo.
20210510_164224.jpg
View attachment 1779823
 
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), imepata kibali cha ajira za walimu wa Shule ya Msingi na Sekondari 6,949 na kada mbalimbali za afya 2,726 watakaoajiriwa chini ya Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini.

Maombi ya ajira hizo yataombwa kwa njia ya mtandao kuanzia May 9 hadi 23, mwaka huu kupitia kiunganishi cha ajira.tamisemi.go.tz, Waziri wa TAMISEMI, Ummy Mwalimu, amesema ajira hizo zitajaza nafasi zilizoachwa wazi na Watumishi waliokoma utumishi kutokana na sababu mbalimbali.

“Serikali imetoa kibali, maana mara baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kueleza kwamba atatoa ajira 6000 kwa walimu tulikuwa tunapata msukumo mkubwa kutoka kwa wananchi wakihoji kwanini TAMISEMI hatutangazi, taratibu za serikali lazima tupate kibali Menejimenti ya Utumishi wa umma”———Waziri Ummy

Waziri Ummy amesema kwa Shule ya Msingi wanatakiwa Walimu wenye daraja la IIIA wenye astashahada ya elimu ya msingi, elimu ya michezo, elimu ya awali na elimu maalum, Mwalimu wa daraja la IIIB anatakiwa kuwa mhitimu wa stashahada ya ualimu wa elimu ya awali, msingi, elimu maalum na Mwalimu wa daraja la IIIC, mhitimu wa shahada ya ualimu masomo ya lugha ya kiingereza, historia na jiografia
20210510_164430.jpg
 
Jeshi la Polisi nchini limefanya operesheni maalum ijulikanayo kwa jina 'Operesheni Wami' ikishirikisha Mikoa minne ya Tanga, Pwani, Morogoro na Mkoa wa Kipolisi Kinondoni kwa muda wa siku 45, hii ni kutokana na ongezeko la matukio ya uhalifu ikiwemo wizi wa magari na pikipiki, ujangili na unyang’anyi wa kutumia silaha na matukio mengine.

Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi nchini Mihayo Msikhela ameelezea mafanikio ya operesheni hiyo na kusema wamekamata malighafi ya kutengeneza Pesa bandia, magari manne na pikipiki saba, silaha, ng’ombe 132, mbuzi 27, nyama ya nyumbu (nyara) kilo 7, dawa za kulevya, gongo n.k

Watuhumiwa waliokamatwa kwenye operesheni hiyo ni 262 na kati yao 195 waliohojiwa na kufikishwa Mahakamani.
20210510_164622.jpg
20210510_164640.jpg
20210510_164656.jpg
20210510_164728.jpg
20210510_164744.jpg
 
Watu wawili ambao wametoka gerezani hivi karibuni kwa msamaha wa Rais Samia Suluhu wameuawa na Wanachi wenye hasira kali baada ya kukamatwa wakidaiwa kuiba vitu mbalimbali Kibaha mkoani Pwani.

Watu hao ni Ramadhani Mohamedi maarufu Seven au Ali (28) na Idd Hamisi maarufu Chuga (30) wote wakazi wa Kibaha na walifungwa kwa makosa ya wizi kabla ya kupata msamaha wa Rais Aprili 12 mwaka huu kutoka katika gereza la Mkuza lililopo Kibaha.

RPC wa Pwani Wankyo Nyigesa ametoa taarifa leo May 10, 2021 na kusema Watu hao wameuawa juzi May 08,2021 kwa kupigwa na mawe, mapanga na fimbo wakituhumiwa kuiba.

“Niwasihi Wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi kwa kisingizio cha hasira na badala yake watoe taarifa Polisi inapotokea tukio la wizi kwenye maeneo yao, ili watuhumiwa wakamatwe na kufikishwa katika vyombo vya sheria”———RPC PwaniView attachment 1779821
Wangejue ni kheri wangewaacha huko jela wapumzike
 
Selemani Machele Msamati (72) amefariki wakati akitibiwa Songea, Ruvuma baada ya kunywa sumu ya kimatila ya kuulia wadudu shambani, RPC Simon Maigwa amesema bado sababu ya kujiua haijabainika lakini uchunguzi unaendelea.

RPC Maigwa amesema ———> “Wananchi msijichukulie maamuzi ya mnapopatwa na magumu, fateni ushauri na usaidizi kama wa Taasisi za kidini, Dawati la Jinsia au Ndugu na Jamaa wa karibu”
20210510_201121.jpg
 
Watu wawili wamefariki baada ya Bajaji waliyokua wamepanda kugonga Treni katika eneo la Modeko, Kata ya Mazimbu Manispaa ya Morogoro ambapo Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Morogoro Goodluck Zelote amesema Treni hiyo ilikua ikitokea Morogoro kwenda Dodoma.

Kwenye Bajaji walikuwepo Dereva na Abiria mmoja ambapo Abiria alifariki papohapo eneo la tukio huku Dereva ambae aliwaishwa Hospitali naye akifariki baadae, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Morogoro Dr. Mkumbo Daniel amesema Dereva Bajaji alifariki akiwa anapatiwa matibabu Hospitalini hapo.
20210510_201258.jpg
20210510_201315.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom