Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,077
- 464,004
“Nakupongeza Mzee Mwinyi kwa kuandika kitabu chako kwa lugha ya Kiswahili, nimekisoma mara mbili, mara ya kwanza nilishtuka nikapata uoga nikasema Mzee Mwinyi yamempata yote haya Mimi je!?, baadaye nikasoma tena uoga ukaniisha nikasema kazi iendelee”———Rais Samia kwenye uzinduzi wa kitabu cha Mzee Mwinyi Dar es salaam leo
“Kikubwa zaidi nilichojifunza kwenye kitabu cha Mzee Mwinyi ni kwamba Mzee Mwinyi ni Baba wa Mageuzi, alipoingia madarakani Nchi yetu ilikuwa vibaya kiuchumi lakini alipoingia akafanya mageuzi, alianzisha ubinafsishaji wa Mashirika ya Umma ikiwemo Kiwanda cha Bia”———Rais Samia
“Mzee Mwinyi anasema alibinafsisha Kiwanda cha Bia Tanzania kwasababu kilikuwa kinaendeshwa kwa hasara, kabla ulikuwa ukitaka bia kwa ajili ya harusi ilikulazimu kupata kibali cha kununua bia kutoka kiwandani au kwa Wakala tena kwa kuonesha kadi za mialiko ya harusi”———Rais Samia
“Mzee Mwinyi ndiye aliyesimamia kuanzishwa kwa Mfumo wa Vyama Vingi nchini kwahiyo ni sahihi kusema yeye ni Baba wa Mageuzi, pia Mzee Mwinyi ametufundisha kwamba Uongozi wa Nchi hautafutwi ila unakutafuta, alikuwa Rais bila kumuhonga Mtu wala kutumia nguvu”———Rais Samia

mtoto mlito