Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,077
- 464,004
Waziri wa Viwanda na Biashara Profesa Kitila Mkumbo akiambatana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dr. Hashil Abdallah wamekutana na Waagizaji na Wazalishaji mafuta ya kula Nchini Tanzania ili kujua kinachosababisha kupanda kwa bei ya mafuta hayo ambapo wameweka mikakati ya muda mfupi na mrefu ya kukabiliana na uhaba wake.
“Tunafahamu kutokana na upungufu wa malighafi, Viwanda vyetu vya ndani vya alizeti haviwezi kuzalisha kwa kiwango ambacho kinakidhi mahitaji ya ndani, Nchi nzima inahitaji tani 570,000 na sisi tuna uwezo wa kuzalisha tani 210,000 pekee, ili kufidia upungufu huu tunaagiza nje”
Profesa Mkumbo ametaja changamoto kubwa zinazosababisha kupanda kwa bei ya mafuta kuwa bei ya mafuta ya mawese katika soko la Dunia kupanda ambapo mwaka jana katika soko la Dunia yaliuzwa USD 600 kwa tani moja lakini kwa sasa wanauza USD 1200 kwa tani.
Sababu nyingine kwa sasa Waagizaji wanaagiza mafuta yaliyochakatwa kutoka nje sababu viwanda vitatu vikubwa vya Tanzania havifanyi kazi sababu ya mabadiliko ya kodi kipindi cha nyuma, waagizaji walikuwa wakiagiza mafuta yaliyochakatwa na wanaeeleza kuwa ni mafuta ghafi, serikali ili kudhibiti na kulinda viwanda vya ndani iliongeza kodi mpaka 35% ya uingizaji ya mafuta yaliyochakatwa.
Waziri Profesa Mkumbo ameeleza kuwa kuanzia mwezi huu wa tano hadi mwezi saba kuna mavuno makubwa ya alizeti ambayo yatasaidia kupatikana malighafi kwa viwanda vya alizeti hivyo uzalishaji wa mafuta utaongezeka na kusaidia bei ya mafuta kushuka.
Mwenyekiti wa wenye Viwanda vya mafuta ya kula Gulam Dewji ameeleza kuwa kupanda kwa bei ya mafuta Tanzania kunatokana na bei ya mafuta kwenye soko Dunia hivyo ameiomba Serikali kupunguza kodi ya uagizaji wa mafuta kwani kwa sasa kodi ya mafuta yaliyochakatwa ni 35% na kodi ya mafuta ghafi ni 25% ambayo hupitishwa kiwandani kuchakatwa hivyo kodi kubwa ya mafuta ghafi ndio imesababisha wafunge viwanda na waagize mafuta yaliyochakatwa.