Makapuku Forum

Makapuku Forum

VIDEO: Mkuu wa Wilaya ya Temeke Godwin Gondwe amempa siku saba Mwenyekiti wa Mtaa wa Azimio kusini Kata ya Azimio, Temeke Iddy Njechele kuitisha mkutano wa Wananchi katika Mtaa wake, ametoa maagizo hayo alipozuru katika Mtaa huo na kupata wasaa wa kusikiliza kero na changamoto za Wananchi.

Akiwa ameambatana na wataalamu kutoka Manispaa, DAWASA, pamoja kamati ya Ulinzi na Usalama alisikiliza kero mbalimbali za mtaa huo ikiwemo kukosekana kwa mikutano ya Wananchi ndani ya mtaa, gharama za uondoshaji taka, TASAF, changamoto ya mradi wa maji , Ulinzi shirikishi (SunguSungu) nk

Wananchi wamemueleza DC kuwa gharama ya kuzoa taka ni kubwa ambayo ni Tsh. 3000 kila chumba, Mradi wa maji ulioko unamnufaisha Mwenyekiti wa mtaa, wanatozwa malipo ya ulinzi shirikishi wakati hakuna ulinzi unaofanyika.

Gondwe ameagiza suala la taka na Sungusungu lijadiliwe katika mkutano mkuu wa mtaa na mapendekezo yawasilishwe ngazi husika na mradi wa maji uliopo utakuwa chini ya DAWASA kuanzia sasa.
20210429_144836.jpg
 
Kwenye orodha ya Nchi zenye bei kubwa za Bando Duniani ambayo imetolewa na Mtandao wa Cable wa Uingereza inayoongoza ni Equatorial Guinea ambayo GB 1 wanalipia USD 49.67 (Tsh. 115,420) ikifuatiwa na Kisiwa cha Falkland (USD 44.56), Saint Helena (USD 39.87) na São Tomé and Principle (USD 30.97).

Kutoka Afrika, Nchi ya Malawi ipo kwenye Top 5 za bei kubwa ya Bando Duniani ambapo GB 1 wanalipia USD 25.46.
20210429_145039.jpg
20210429_145108.jpg
 
Nchi ya Israel imekuwa namba moja Duniani kwa kutoa bei rahisi za Bando za Internent mwaka huu ambapo GB 1 inagharimu USD 0.05 (Tsh. 116.19) kwa mujibu wa takwimu za mtandao wa Cable wa Uingereza, Israel ilikuwa nafasi ya Pili mwaka jana.

India imeishangaza Dunia kwa kutoka kwenye nafasi ya kwanza mwaka jana kwa bei nafuu ya Bando Duniani hadi nafasi ya 28 ambapo GB 1 kwa sasa inagharimu USD 0.68.

Kwenye tano bora ya Dunia ya bei rahisi ya Bando ipo pia Sudan (USD 0.27).
20210429_145254.jpg
20210429_145313.jpg
 
Watumiaji wa Mtandao wa Twitter Tanzania wameanza kuutumia mtandao huo leo bila kuhitaji kujiunga na Virtual Private Network (VPN) ambayo wamekua wakiitumia kwa zaidi ya miezi mitano sasa, tweets mbalimbali zimeandikwa na baadhi ya Watumiaji kuonesha kufurahishwa na maamuzi hayo.
20210429_145516.jpg
 
Kwa mwaka wa pili mfululizo, Tanzania imetajwa kuwa ni Nchi ya kwanza Afrika Mashariki ambayo bei ya bando zake za internet ni nafuu kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Mtandao wa Utafiti wa Cable wa nchini Uingereza.

Kwenye ripoti hiyo yenye Takwimu za Dunia nzima ambazo zimekusanywa kuanzia December 08,2020 hadi February 25,2021 inaonesha kuwa Tanzania ina bando rahisi ambayo ni USD 0.75 (Tsh. 1,742.81) kwa GB moja ikifuatiwa na Rwanda (USD 1.25), Uganda (USD 1.56) na Burundi (USD 2.10).

Kenya ilikuwa ya pili mwaka jana ambapo bando iligharimu USD 1.04 kwa kila GB lakini kwa mwaka huu gharama zimepanda na kufikia USD 2.25 .
20210429_145604.jpg
 
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi amesema ni lazima Waajiri wote nchini waweke mifumo madhubuti ya usalama kwa Wafanyakazi wanapokua kazini———Kauli mbiu yangu "Mwajiri lipa mishahara kabla jasho la Mtumishi halijakauka"

“Ni muhimu kila Mwajiri kulipa mishahara kwa tarehe husika, haiwezekani Mfanyakazi halipwi mshahara miezi 13 wakati Mfanyakazi huyo ndiye anaelinda mitambo na shughuli nyingine kiasi cha kujikuta anaingia kwenye tamaa ya wizi, walipeni mkizingatia hili tutajenga uchumi wa Mtu, Familia na Nchi nzima”———Katambi

“Suala hilo linaenda sambamba na mafao, kumekua na ujanjaujanja kwa baadhi ya Waajiri unapofika muda wa kustaafu Mfanyakazi anasumbuliwa pesa zake za NSSF, naagiza Waajiri wote kuhakikisha wanalipa hii michango ya madai ya Wafanyakazi wao kwa wakati”———Katambi

“Waajiri nawasihi muige mfano mzuri wa ulipaji mishahara kamili na kwa wakati, Waajiri tendeni haki, faida na mitambo sawa ila kipaumbele kiwe kwa wanaozalisha faida hiyo na kuendesha mitambo yako, Serikali hatutamuonea Mtu wala kumpendelea tutatenda haki tupu”———Katambi
20210429_145736.jpg
 
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi amewaagiza Mameneja wa Mikoa NSSF, PSSF na Compliance Officers kuhakikisha hakuna madeni kwa Waajiri na Waajiri wenye madeni wachukuliwe hatua.

Katambi amesema hatua hii inakuja kufuatia kuwepo wa Waajiri ambao wamekuwa na ujanjaujanja na unapofika muda wa kustaafu Mfanyakazi anasumbuliwa pesa zake za mafao.

“Hili la Wadaiwa sugu au Waajiri sugu wasiolipa mishahara, kodi (P.A.Y.E),na michango ya Watumishi katika mifuko ya hifadhi ya jamii tutawatangaza kumi bora hadharani na kuwapa tuzo ya hati chafu ya Kutotii Sheria za Kazi”———Katambi

“Natoka shukrani za dhati kwa niaba ya Waziri Mkuu wetu Kasimu Majaliwa na Waziri wa Nchi Jenista Mhagama kwa TUCTA na ATE kwa ushirikiano wao mkubwa na kusimamia haki za Wafanyakazi wa Tanzania”———Katambi
20210429_145850.jpg
 
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi amewaagiza Mameneja wa Mikoa NSSF, PSSF na Compliance Officers kuhakikisha hakuna madeni kwa Waajiri na Waajiri wenye madeni wachukuliwe hatua.

Katambi amesema hatua hii inakuja kufuatia kuwepo wa Waajiri ambao wamekuwa na ujanjaujanja na unapofika muda wa kustaafu Mfanyakazi anasumbuliwa pesa zake za mafao.

“Hili la Wadaiwa sugu au Waajiri sugu wasiolipa mishahara, kodi (P.A.Y.E),na michango ya Watumishi katika mifuko ya hifadhi ya jamii tutawatangaza kumi bora hadharani na kuwapa tuzo ya hati chafu ya Kutotii Sheria za Kazi”———Katambi

“Natoka shukrani za dhati kwa niaba ya Waziri Mkuu wetu Kasimu Majaliwa na Waziri wa Nchi Jenista Mhagama kwa TUCTA na ATE kwa ushirikiano wao mkubwa na kusimamia haki za Wafanyakazi wa Tanzania”———KatambiView attachment 1767545
Huyu jamaa hana "haiba" ya uwaziri wala naibu waziri
 
Kabla ya uchaguzi wa rais wa Marekani wa mwaka 1860, Mwanasiasa aliyefahamika kwa jina Valentine Tapley aliapa kwamba kama Abraham Lincoln ambaye alikuwa mgombea urais, atachaguliwa kuwa Rais, basi Hatonyoa ndevu zake katika maisha yake yote hadi atakapokufa.

Baada ya uchaguzi Lincoln akatangazwa mshindi na kuwa rais, Tapley akatimiza ahadi yake hakunyoa ndevu hadi alipokufa Mwaka 1910, wakati huu ndevu zake zilifika urefu wa futi 12.

Kabla ya kuzikwa ndevu zote zikanyolewa.
20210429_161320.jpg
 
BODI ni kabila linalopatikana nchini Ethiopia, kila sherehe za mwaka mpya lina utamaduni wa kuandaa mashindano ya Wanaume kushindana kuwa na vitambi.

Maandalizi ya mashindano huanza miezi sita kabla ya siku ya sherehe za mwaka mpya. Wanaume wanaoshiriki katika mashindano hayo huwa hawaruhusiwi kutoka nje wala kushiriki tendo la ndoa hadi siku ya sherehe itakapofika.

Siku ya sherehe ikifika ndipo mshindi anachaguliwa. Yeyote atakayekua na tumbo kubwa kuzidi wengine ndiye mshindi na uchukuliwa kama shujaa wa kabila ilo.

Unaambiwa kila mtoto katika kabila la BODI katika makuzi yake anakua na ndoto ya kuwa na kitambi kikubwa ili awe shujaa.
20210429_162106.jpg
20210429_162049.jpg
 
Mwaka 1840 Malkia Victoria aliweka historia ya kuwa miongoni mwa Wanawake wa kwanza kuvaa gauni jeupe katika katika harusi.

Hii ilitokea katika harusi yake alipokuwa anaolewa na Prince Albert, Malkia Victoria alichagua kuvaa gauni jeupe rangi ambayo kiutamaduni haikua inatumika katika harusi.

Kwa kipindi hicho mavazi meupe yalikuwa yakitumika zaidi katika maombolezo.
20210429_162254.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom