Makapuku Forum

Makapuku Forum

Mwanamke huyo alitangazwa kutoweka kwenye msafara wa Watalii uliokuwa ukitembelea eneo lenye volkano la Eldgja huko kusini mwa Iceland.

Kwa maelezo ya kuhusu mtu aliyepotea yaliyotolewa na watalii wenzie hakuweza kufahamu kama wanaemtafuta ni yeye na bila kujua alijiunga na kikundi cha kumtafuta yeye mwenyewe.

Baada ya operesheni ya usiku kucha iliyohusisha karibu watu 50, mwanamke aliyepotea mwishowe aligundua yeye ndiye anayetafutwa.

Katika maelezo ya watafutaji Mwanamke waliyekuwa wanamtafuta alikua na urefu wa 160cm na amevaa mavazi meusi. Kwa wakati huo huyo Mwanamke alikua ameshabadilisha nguo zake alizokua amevaa bila wenzie kutambua.

Katika utafutaji huo unaambiwa yeye mwenyewe nae alikuwa mstari wa mbele katika kujitafuta.
20210429_164557.jpg
 
Hii ilitokea mwaka 1996 huko Hong Kong, Jambazi mmoja aliyeitwa #Cheung Tze Keung alimteka nyara mtoto wa tajiri mkubwa wa Asia #Li Ka-shing na kumtapeli tajiri huyo Dola za kimarekani milioni 130 kama fidia ya kumuachia mwanae, baadaye Jambazi huyo alimpigia simu tajiri #Li Ka-shing na kumuomba ushauri wa jinsi ya kuwekeza pesa hizo.View attachment 1767697
😆😆😆😆
 
Jiji la Whynot huko North Carolina, lilipewa jina la "WHYNOT" kwa sababu wakazi wake walibishana sana kuhusu jina gani la kuuita mji huo.

Baada ya mabishano ya muda mrefu ya watu wengi wakitoa maoni yao na kukataliwa, na kulalamika kwa kusema, "kwanini isiwe jina ilo".. Mwishowe mtu mmoja alisimama na kusema, "Kwanini tusiite mji huo "WHY NOT" (Kwanini isiwe) kisha kila mtu arudi nyumbani?" Kila mtu alikubaliana na wazo hilo na ndivyo walivyofanya alafu kila mtu akasepa zake.
20210429_164840.jpg
 
Mwanaume mmoja wa kituruki kwa jina la Ibrahim Yucel alikifungia kichwa chake kwenye kibanda kidogo kama kofia ili kujisaidia kuacha kuvuta sigara.

Yucel alifikia uhamuzi huo baada ya majaribio yake kadhaa ya kutaka kuacha kuvuta sigara kushindikana.

Mkewe ndiye alikua anahifadhi ufunguo wa kibanda hiko na alikua anamfungulia wakati wa chakula tu.
20210429_165219.jpg
 
Mwaka 1942, Mwanaume aliyepewa jina la Phantom Barber alikua anavunja na kuvamia nyumba za watu huko Mississippi na kukata nywele zao. Alikuwa anakata nywele za wanawake hususani wasichana wadogo.

Uvamizi huo alikuwa akiufanya wakati wa Usiku pindi watu walipokuwa wamelala. Licha ya kuwepo kwa kesi nyingi za watu kukatwa nywele lakini muhusika hakuweza kutambulika ni nani.

Siku moja alivamia katika nyumba moja ambayo ilikuwa wanaishi mke na mume ambapo baada ya kushindwa kutimiza lengo lake aliwadhulu kwa kuwapiga na bomba la chuma.

Tukio hili la kuwashambulia wanandoa lilichochea hisia za watu na msako wa kumtafuta Phantom Barber uliongezeka, mwishowe mtuhumiwa alipatikana.

Mwanamume aliyeitwa William Dolan alikamatwa na kushtakiwa kufanya jaribio la mauaji. Nywele za kibinadamu pamoja na bomba la chuma lililotumika katika shambulio lilipatikana karibu na nyumba yake, lakini hakukubaliana na mashitaka hayo ambayo baada ya uchunguzi kufanyika ilikutwa hana hatia hivyo akaachiwa.
20210429_165313.jpg
 
Mwanaume mmoja wa kituruki kwa jina la Ibrahim Yucel alikifungia kichwa chake kwenye kibanda kidogo kama kofia ili kujisaidia kuacha kuvuta sigara.

Yucel alifikia uhamuzi huo baada ya majaribio yake kadhaa ya kutaka kuacha kuvuta sigara kushindikana.

Mkewe ndiye alikua anahifadhi ufunguo wa kibanda hiko na alikua anamfungulia wakati wa chakula tu.View attachment 1767709
Hahaha.. walimwengu wana mambo
 
Huko Urusi watu wawili mwanamke na mwanaume walipata ajali wakiwa na mbwa wao. Mwanamke alikufa hapo hapo na mwanaume aliwahishwa hospitali lakini baadae alikufa, mbwa pekee ndiye alipona.

Baada ya tukio lile mbwa aliendelea kukaa eneo hilo, licha ya watu kujaribu kumchukua kutaka kumrudisha nyumbani, wengine walitaka kumchukua ili wamfuge lakini mbwa huyo alikataa kutoka kwenye eneo la ajali na akakaa katika eneo hilo hadi alipokufa miaka saba baadaye.

Kutokana na kitendo hicho cha uaminifu alichokionesha mbwa huyo, lilitengenezwa sanamu kubwa la mbwa huyo na kuwekwa katika mji huo kama njia ya kuheshimu uaminifu wake.
20210429_165540.jpg
 
Mwanamume mmoja nchini India aliyefahamika kwa jina la Neelim Kumar Khaire aliweka rekodi ya dunia mwaka 1986 kwa kutumia masaa 72 kukaa katika banda moja na nyoka wa aina 72 tofauti wenye sumu kali zaidi nchini India ili kuthibitisha kwamba nyoka hawang'ati watu kama hawajachokozwa.

Katika masaa hayo 72 aliyokaa katika banda ilo lenye nyoka wakali, Khaire hakuonesha wasiwasi wowote, ndo kwanza alikua anasoma magazeti na muda mwingine kusinzia kabisaa bila uwoga.

Alitoka ndani ya banda ilo bila kuumia wala kuumwa na nyoka hata mmoja.
20210429_165649.jpg
 
Mwaka 1958, msichana wa kizungu aliwabusu wavulana wawili wamerakani weusi wa miaka 9 na 7, kwenye mashavu.
Baada ya tukio hilo wavulana hao wawili walikamatwa, wakafungwa kwa siku 6 bila taarifa yeyote kwa wazazi wao. Walipigwa sana na polisi na walifungwa kwa jumla ya miezi 3.
20210429_165932.jpg
 
Mwaka 2019, polisi nchini Brazil walimkamata kasuku aliyepewa mafunzo na wafanyabiashara wa dawa za kulevya.

Kulingana na ripoti, ndege huyo alikuwa amefundishwa kutoa tahadhari kwa wahalifu kuhusu polisi kwa kupiga kelele: "Mama, polisi!" Mara tu polisi wanapokaribia, anaanza kupiga kelele.
20210429_170012.jpg
 
Mwaka 1721, mwanamke wa Scotland, Maggie Dickson alihukumiwa kifo kwa kunyongwa. Alining'inizwa, akatangazwa amekufa, akawekwa kwenye jeneza la mbao, na kusafirishwa.

Akiwa njiani kuelekea maeneo ya kanisa alizinduka na kuonekana akiwa mzima.

Kwa mujibu wa sheria ilisema adhabu yake imetekelezwa kwaio atakama ameonekana mzima (hajafa) adhabu yake imeshaisha na aliishi miaka mingine 40 ndipo akafa.
20210429_170106.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom