Makapuku Forum

Makapuku Forum

Mwenyezi Mungu nakuomba Linda wazazi wangu, ndugu zangu, rafiki zangu, mume uliyeniandalia, watoto wetu utakaotupa, yatima wote, wajane wote, wagonjwa walio nyumbani na mahospitalini, wasafiri wote, wenye shida mbalimbali lakini zaidi Bwana linda Taifa letu la Tanzania..
 
Baba warehema wewe ujuaye mahitaji yetu kabla hatujakuomba, nakuomba uwafunike na uwalinde watoto wa Taifa hili Mfalme, malaika wako akatembee pamoja na watoto hawa katika kipindi hiki ambacho Taifa linapita kwenye changamoto ya ugonjwa, kwa nguvu zetu hatutaweza Mfalme wa amani, tawala njia zao, akili zao lakini zaidi mfalme wafunike kwa Damu yako!
 
Mfalme wa amani, nawaweka mikononi mwako wanaume wa Taifa hili Mfalme, wapo wanaopitia kwenye changamoto mbalimbali, kawaonekanie Mfalme, wape ujasiri wa kusimama na kuendelea mbele! Wape ujasiri wa kuyashinda majaribu Baba wa Rehema, tangulia mawazo yao, maamuzi yao na akili zao!
 
Kristo wa Nazareth, nasimama na wanawake wa Taifa hili, nikiomba rehema yako na upendo wako ukawe pamoja nao katika kusimamia malezi ya watoto, jamii na Taifa kwa ujumla, nakataa roho za kukata tamaa kwa wanawake wa Taifa hili katika Jina la Yesu, tupe moyo wa kusali, moyo wa kuendelea kusimama na familia zetu, moyo wa kutokata tamaa katika jina la Yesu!!

Asante Yesu kwa kuwa utasimama pamoja nasi, ni katika jina la Yesu nimeomba na kuamini, Amen.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom