Makapuku Forum

Makapuku Forum

Jasho ni moja ya njia maalumu ya mwili ya kurekebisha kiwango cha joto la mwili, ila inapofika wakati jasho hili linaanza kutoa harufu mbaya hua kero kwa mtu anaetoa harufu na kwa jamii nzima inayomzunguka.

Kwa kawaida jasho hua halina harufu, kwani jasho ni mchanganyiko wa maji na aina mbali mbali za madini chumvi yanayotolewa kama taka mwili,

Harufu mbaya ya kwapa husababishwa baada ya bakteria kumeng`enya aina flani ya protini inayozalishwa pamoja na jasho kutoka katoka tezi maalumu za jasho ziitwazo apocrine glands. Tezi hizi zinapatikana katika maeneo ya makwapa, matiti, maeneo ya sehemu za siri na katika kope za macho.

Kwa baadhi ya watu hali hii ya kunuka kwapa hua sugu sana na hivyo kua kero kwao na jamii kwa ujumla. Ili kupunguza harufu au kuimaliza kabisa yapaswa kupunguza pia kiwango cha jasho unalozalisha kwa siku kwa kufanya yafuatayo;

1; Kula mlo kamili na fanya mazoezi ili kupunguza mwili, kwa sababu watu wanene huathiriwa sana na tatizo hili kwa sababu ya mikunjo mikunjo ya ngozi yao hivyo kutoruhusu jasho kukauka mwilini.
2; Vaa nguo za pamba , nguo za aina hii husharabu jasho la mwili na kukuacha mkavu, epuka pia nguo zanazokubana sana.
 
3; Tumia manukato mbalimbali ili kupambana na harufu.. pia tumia dawa maalumu zinazoweza kupunguza kiwango cha jasho linalizalishwa kwenye makwapa (muone daktari wako kwa kupata dawa hizi)
4;Kua na tabia ya kuoga mara kwa mara.. kila unapokua umefanya shughuli yoyote ya kukutoa jasho, ni vizuri kutumia medicated soap ili kuua bakteria wanaozalisha harufu mbaya.

5;Epuka vyakula na vinywaji vinakavyokufanya utoe jasho. Vyakula kama pilipili, kahawa, pombe, vitunguu;
6;Nyoa nywele za kwapani. Kwa sababu uepo wa nywele hizi husababisha jasho kutokauka.. hivyo bacteria kuzalisha harufu kutokana na jasho hili.
7; Kula mboga mboga za majani kwa wingi husaidia kupunguza kiwango cha jasho mwilini
 
8;Kunywa maji ya kutosha kila siku.
9;Badilisha nguo kila siku.. ili kupunguza mrundikano wa jasho.
10;Punguza msongo wa mawazo kwa kufanya vitu vitakavyokupa burudani kama kusikiliza muziki na mengineyo, hali hii hupunguza kiwango cha jasho mwilini.

Muone daktari wako endapo una matatizo yafuatayo;
1; unatoka jasho kwa wingi wakati wa usiku mpaka unalowanisha nguo au shuka zako
2;unatokwa na jasho nyingi kuliko kawaida ulivyozoea
3;unatoka jasho kipindi cha baridi
4;jasho lina kunyima uhuru wa kufanya kazi zako za kila siku.
 
Watu wengi Waume kwa wanawake hukoseshwa raha na matatizo mengi ya sehemu za siri. Moja wapo ya tatizo hili ni kutokewa na vipele baada ya kunyoa nywele huotazo sehemu hizo.

Nini Umuhimu wa hizo nywele sehemu za Siri ?

● Nywele za uke na uume huzuia maambukizi ya bakteria ambao huweza kupenya kwenye vitundu vidogo vya sehemu hizo,vilevile huzuia mchubuko wa ngozi katika sehemu hizo.

Sababu hii haimaanishi usinyoe sehemu za Siri. Sehem hizi zikizidi nywele hutoa harufu mbaya. Hivyo zingatia husafi na unadhifu pia.

Nini kinasababisha vipele hvi?

Sababu zipo nyingi. Baadhi ambazo ni sababu kwa wengi ni kama:

● Urudiaji wa kiwembe ulichokwisha kukitumia uliponyoa kabla ya siku hiyo au kutumia kiwembe butu kama njia ya kunyolea.
● Kunyoa uelekeo tofauti na nywele zako zinavyoota.

Nini nifanye baada ya kupata vipele?

Mara nyingi vipele hivi hupotea vyenyewe baada ya muda, Ila kuna vingine huwepo kwa muda mrefu na hata kuanza kuuma na kutengeneza usaha. Baadhi ya njia husaidia ni kama:

● Kutumia kitambaa safi na maji ya vuguvugu kukanda sehemu iliyo na tatizo hilo.
● Matumizi ya asali na maji ya vuguvugu pia husaidia kupunguza vimelea vya bakteria wowote katika eneo hilo na hupunguza vipele hivyo
 
Matumizi ya yai. Yai linaprotini ziitwazo albumin ambazo husaidia sana ngozi.kwahyo husaidia kuponesha ngozi yenye vidonda au vipele kwa haraka.unatumia sehemu ya nje (nyeupe) ya yai kupaka sehemu husika unaacha inakaukia hapo halafu unabandua,inatoka pamoja na kipele hasa kilichoanza kutunga usaha.
● Matumizi ya sukari kama scrub. Sukari ina glycolic acid ambayo hupenya kwenye ngozi na kusaidia kuua seli zilizokufa na kuponya ngozi iliyoharibika eneo hilo haraka. Jinsi ya kutumia?Changanya sukari na mafuta ya olive kama unayo, kama huna tumia ata ya nazi kisha paka sehemu husika na sugua taratibu kwa kuzungusha taratibu kuelekea juu kisha acha kwa muda. Alafu toa kwa maji ya vuguvugu. Rudia hivi hadi vitakavyokwisha.
Endapo njia hizi hazikusaidii, muone daktari wa ngozi kwa matibabu sahihi zaidi.

Nini nifanye kuzuia vipele hivi?
● Kwanza tumia maji ya vuguvugu ulowanishe sehemu hiyo unayonyoa, kisha tumia sabuni/shaver cream kuweka povu la kutosha ili unyoe kirahisi zaidi kwa maana nywele zinaasili ya kuota kwa kujifungafunga na ni ngumu pia, hivyo kwa kulainisha hupunguza uwezekano wa kupata vipele.
● Baada ya kulainisha nyoa kwa kutumia kiwembe/mashine ya kunyolea mpya kwa uwelekeo ambao nywele zako huota.
● Baada ya kunyoa ni vyema kutumia aftershave ambayo husaidia kuzuia bakteria ambao wanaweza kupenya kwenye vitundu vidogo baada ya kunyoa
 
Vilevile imeelezwa kuwa hupaswi kunyoa nywele zote za uke au uume na kuacha kipara, kwasababu huongeza hatari za magonjwa ya ngono wakati wa tendo la ndoa majimaji na bakteria huweza kupenya kutokana na vitundu vidogo vinavyokuwepo baada kunyoa nywele zote.

Muone daktari endapo hali hii haiishi na haswa vipele vikiendelea kutokea, vinatoa usaa, vinauma sana na vinakuwa vyekundu.
 
Kuna no imewekwa pale we tuma tu hata kwa wakala halafu screenshot text ya hela itumie hiyo no text unamwambia hiyo hela ni ya flani na flani

Aisew!kuna haja ya kutoa id kwani?

Afu naona mambo ya kuvaa vikaptula.

Hapo patanishinda mimi! I am a learned gentleman...! Kaptula hapana..
 
Vilevile imeelezwa kuwa hupaswi kunyoa nywele zote za uke au uume na kuacha kipara, kwasababu huongeza hatari za magonjwa ya ngono wakati wa tendo la ndoa majimaji na bakteria huweza kupenya kutokana na vitundu vidogo vinavyokuwepo baada kunyoa nywele zote.

Muone daktari endapo hali hii haiishi na haswa vipele vikiendelea kutokea, vinatoa usaa, vinauma sana na vinakuwa vyekundu.
nimekumbuka kitu jana kuhusu swala la kunyoa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom