Muziki: Hata Mimi Sielewi
...unaweza kusema chochote unachotaka, nchi huru hii na ndiyo maana mimi kwa kutumia uhuru wangu usio na mipaka wala mbwa Hobby ninakusalimia wewe Kapuku ambaye unalifanya jukwaa hili kuwa sehemu znuri kuwepo. Inawezekana narudiarudia sana haya maneno, vumilia tu na una uhuru wa kuchukia kama yanakuudhi na ikiwa ni tofauti basi furahia maana wewe ni mtu bora sana hapa.
Leo ni Jumatano, kama ulikuwa hujui ninakujulisha sasa na kukutakia wakati mzuri ulionao wakati unaburudika na huu muziki ninaoupenda zaidi.