Makapuku Forum

Makapuku Forum

Tafasiri Unavyoweza: Itumie Au Ipoteze

Shule nyingi zimefungwa kwa sasa, mtaani watu wameongezeka sana. Inapendeza kuwaona vijana walioishi ndani ya shule za 'boarding' wakiziacha sare zao za kushindia na kuvaa mavazi tofautitofauti yanayowapendeza. Si lengo la kipengele hiki kuongelea kuhusu kufungwa kwa shule na mavazi ya vijana wetu. Makala haya yanaangalia namna ambavyo kama umepata maarifa au ujuzi fulani na usipoutumia basi unaweza kupoteza maarifa hayo na ujuzi ulioupata na ukawa ni mzigo kwa jamii nataifa kwa ujumla. Use it or lose it, Tafasiri unavyoweza.

Kwenye upande wa kusoma na kuandika bila kusahau kuhesabu (3 K) Unesco, taasisi inayofuatilia masuala ya elimu duniani inasema kwamba kuna hatari kubwa ya mtu ambaye alikuwa anajua kusoma (literate) kurudia ujinga (illiterate) kama hatojisumbua kujisomea baada ya kuwa amemaliza elimu iliyomlazimisha kusoma.

Maarifa yapo vitabuni, asikudanganye mtu, shukrani kwa mitandao ya kijamii, kwa sasa wengi wentu hatubebi vitabu kujisomea tena, simu yako inakuwa kitabu na majukwa kama JF yanasaidia kukuongezea maarifa maana kuna habari inabidi uzisome, usissimuliwe na kwa wewe unayeweza kupoteza muda wako kuchangia humu, hauupotezi bure, unaongezea wengine maarifa na kujiongezea maarifa pia. Hakuna unachoandika humu kisicho na faida kwa kila mwanajf hata kama hukubaliani nacho.

Kitumie au kipoteza, ni rahisi tu na ni vizuri kukumbushana kwa hili. Nikutakie wiki njema
Kinachokuzamisha sio kudondikea mtoni, ni kushindwa kupiga mbizi, ukasizi na watu tukashindwa kukuona, hapo ndio unakuwa umezama.
 
Muziki: Changamka, Usichanganyikiwe

...wiki la kwanza la mwezi wa sita ndo tunalianza, eeh, kama ulikuwa umesahau basi nakukumbusha na baada ya kumbusho hili nakusalimia Kapuku mwenzangu na kukutakia mafanikio katika mwezi huu. Mwezi wa kipekee kabisa kwa kina sie tunaolipa kodi mara mbili kwa mwaka, yaani tangu wiki imeanza nimeshangaa sana mwenye nyumba kuniandikia meseji ya kunisalimia. Akilini nikajiongeza tu sijamjibu maana nikijibu tu atanikumbusha kitu ambacho nakikumbuka sana. Mimi sio kama anko wangu ambaye yeye huwa inabidi mwenye nyumba aje na polisi jamii kuchukua kodi.

Muziki sasa, ninajiamnisha ulikuwa na wikend nzuri, kwangu ilikuwa nzuri sana asante kwa kutouliza. Changamka usichanganyikiwe mwezi wa sita huu, mwaka ushagawiwa kwa mwili, sasa ni zamu yako.

Impact!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom