Muziki: Changamka, Usichanganyikiwe
...wiki la kwanza la mwezi wa sita ndo tunalianza, eeh, kama ulikuwa umesahau basi nakukumbusha na baada ya kumbusho hili nakusalimia Kapuku mwenzangu na kukutakia mafanikio katika mwezi huu. Mwezi wa kipekee kabisa kwa kina sie tunaolipa kodi mara mbili kwa mwaka, yaani tangu wiki imeanza nimeshangaa sana mwenye nyumba kuniandikia meseji ya kunisalimia. Akilini nikajiongeza tu sijamjibu maana nikijibu tu atanikumbusha kitu ambacho nakikumbuka sana. Mimi sio kama anko wangu ambaye yeye huwa inabidi mwenye nyumba aje na polisi jamii kuchukua kodi.
Muziki sasa, ninajiamnisha ulikuwa na wikend nzuri, kwangu ilikuwa nzuri sana asante kwa kutouliza. Changamka usichanganyikiwe mwezi wa sita huu, mwaka ushagawiwa kwa mwili, sasa ni zamu yako.