Makapuku Forum

Makapuku Forum

haha Haa.loohh..hapana tubaki Humu " Humu " kwa makapuku wenzetu...huko kwengine nikikupeleka "" watanipora aiseee"" Nina mpango wakuhamishia makazi yangu katika huu Uzi rasmi" kwaajili yko""" huko pengine sinto kwenda tena """
taratibu baba
 
Tafasiri Unavyoweza: Ondoa Mashaka Uongoze

Unategemea kupata nini toka kwa wale unaowaongoza kama wewe si mwaminifu, historia yako imejaa makandokando na hajawahi na hujaonesha kutaka kubadilika? Kama unakosa kuwa mkweli (honesty) na mwenye kuaminika (moral uprightness-integrity) unategemea mafanikio gani katika kile unachokiongoza. Unapokuwa kiongozi na huwaamini unaofanya kazi nao unategemea mafanikio yatafikiwa kwa namna gani? Vitisho! Kiongozi mzuri hapayukipayuki, huongoza kwa mfano, anawaamini anofanya nao kazi, kwa sababu kagawa majukumu (delegating and empowering) na hatengenezi matukio ili aonekane kila wakati. Tafasiri unavyoweza.

Kutaka kusimamia kila kitu hakujawahi kumfanya kiongozi kuwa maarufu, kunampunguzia sifa ya kuwa kiongozi mzuri na kumjaza sifa ya udikiteta, kutaka kuonekana kila sehemu, atajwetajwe kila kukicha. Ni sifa sahihi ya kiongozi kujiamini katika analofanya kwa sababu analofanya ni la ukweli na linakubalika kwa jamii. Kiongozi bora hashindi kusisitiza kuombewa, wanaombewa wenye dhambi, wezi, majangili, mafisadi na watu wa namna hiyo, wenye mapungufu, waoneaji, waporaji na taja kingine unachopenda kiombewe.

Kiongozi kujiamini kwa kusimamia sheria, kutenda haki, kuwa na huruma, kutoonea, kuheshimu walio chini na unaowaongoza kunakupa nguvu ya kupata mafanikio zaidi. Hakuna timu ya mtu mmoja, tafasiri unavyoweza
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom