Makapuku Forum

Makapuku Forum

Muziki: Changa Karata

Mchezo wa karata ni akili, kila kitu unacho wewe na unakiangalia mwenzako hakioni, usijidai kumuonesha mpinzani wako, utashindwa au utakuwa na wakati mgumu kutoboa, Najua unajua namaanisha nini na ndiyo maana sichoki kukusalimia Kapuku mwenzangu na kukushukuru kwa kuwa hapa maana bila wewe jukwaa hili si sehemu nzuri kuwepo.

Asante Tumosa mama JJ, sweetlee kwa kuweka nukuu nzuri za kuvutia (ukiweza weka kila siku). ABJ ni nzuri kukuona hapa kila wakati, Transcend karibu bruh, hearly na wewwe kapuku unayelifanya jukwaa hili kuwa sehemu nzuri
Muziki sasa, furahia sasa

Tafasiri Unavyoweza: Ondoa Mashaka Uongoze

Unategemea kupata nini toka kwa wale unaowaongoza kama wewe si mwaminifu, historia yako imejaa makandokando na hajawahi na hujaonesha kutaka kubadilika? Kama unakosa kuwa mkweli (honesty) na mwenye kuaminika (moral uprightness-integrity) unategemea mafanikio gani katika kile unachokiongoza. Unapokuwa kiongozi na huwaamini unaofanya kazi nao unategemea mafanikio yatafikiwa kwa namna gani? Vitisho! Kiongozi mzuri hapayukipayuki, huongoza kwa mfano, anawaamini anofanya nao kazi, kwa sababu kagawa majukumu (delegating and empowering) na hatengenezi matukio ili aonekane kila wakati. Tafasiri unavyoweza.

Kutaka kusimamia kila kitu hakujawahi kumfanya kiongozi kuwa maarufu, kunampunguzia sifa ya kuwa kiongozi mzuri na kumjaza sifa ya udikiteta, kutaka kuonekana kila sehemu, atajwetajwe kila kukicha. Ni sifa sahihi ya kiongozi kujiamini katika analofanya kwa sababu analofanya ni la ukweli na linakubalika kwa jamii. Kiongozi bora hashindi kusisitiza kuombewa, wanaombewa wenye dhambi, wezi, majangili, mafisadi na watu wa namna hiyo, wenye mapungufu, waoneaji, waporaji na taja kingine unachopenda kiombewe.

Kiongozi kujiamini kwa kusimamia sheria, kutenda haki, kuwa na huruma, kutoonea, kuheshimu walio chini na unaowaongoza kunakupa nguvu ya kupata mafanikio zaidi. Hakuna timu ya mtu mmoja, tafasiri unavyoweza
duuhh""" [HASHTAG]#Jiwe[/HASHTAG] ..hii essay inakuhusu aisee.."""
 
Muziki: Changa Karata

Mchezo wa karata ni akili, kila kitu unacho wewe na unakiangalia mwenzako hakioni, usijidai kumuonesha mpinzani wako, utashindwa au utakuwa na wakati mgumu kutoboa, Najua unajua namaanisha nini na ndiyo maana sichoki kukusalimia Kapuku mwenzangu na kukushukuru kwa kuwa hapa maana bila wewe jukwaa hili si sehemu nzuri kuwepo.

Asante Tumosa mama JJ, sweetlee kwa kuweka nukuu nzuri za kuvutia (ukiweza weka kila siku). ABJ ni nzuri kukuona hapa kila wakati, Transcend karibu bruh, hearly na wewwe kapuku unayelifanya jukwaa hili kuwa sehemu nzuri
Muziki sasa, furahia sasa

Asante Mkuu" natambua uwepo wako na mchango wako pia """..endelea kutufunza na kutuburudisha ""
 
Muziki: Changa Karata

Mchezo wa karata ni akili, kila kitu unacho wewe na unakiangalia mwenzako hakioni, usijidai kumuonesha mpinzani wako, utashindwa au utakuwa na wakati mgumu kutoboa, Najua unajua namaanisha nini na ndiyo maana sichoki kukusalimia Kapuku mwenzangu na kukushukuru kwa kuwa hapa maana bila wewe jukwaa hili si sehemu nzuri kuwepo.

Asante Tumosa mama JJ, sweetlee kwa kuweka nukuu nzuri za kuvutia (ukiweza weka kila siku). ABJ ni nzuri kukuona hapa kila wakati, Transcend karibu bruh, hearly na wewwe kapuku unayelifanya jukwaa hili kuwa sehemu nzuri
Muziki sasa, furahia sasa

Asante binamu Obe..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom