

Zaburi 122:1
Nalifurahi waliponiambia,Na twende nyumbani kwa BWANA.
Kumbu *torati 12:5
Lakini mahali atakapochagua BWANA, Mungu wenu, katika kabila zenu zote, apaweke jina lake, maana, ni makao yake, elekezeni nyuso zenu hapo, nawe wende huko;
Waebrania 10:25
wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia.
Mathayo 18:20
Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.
Kumbu*2 torati 16:17
Kila mtu na atoe kama awezavyo, kwa kadiri ya baraka ya BWANA, Mungu wako, alivyokupa.
Matendo 2:42
Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali.
*Tuombe: Baba katika jina LA Yesu tunajileta mbele zako tukisema asante kwa ulinzi wa usiku kucha wa Leo na hatimae tumeiona siku mpya ambayo Bwana ameifanya sifa na utukufu kwake yeye aliyejuu tumelala wengi lakini tumeamka wachache siyo kwamba sisi ni wema kuliko wengine Bali ni upendo utulinde tuingiapo katika majukumu ya siku nzima ya Leo utuongoze kwa kila tufanyalo roho mtakatifu aishi ndani yetu kuanzia sasa nakuendelea tukinge na ajali za barabarani,mashuleni, makazini,majumbani na za roho utusamehe tulipoenda kinyume na wewe kwa mawazo maneno matendo na kutotimiza wajibu mbalimbali tutakase kwa Damu ya Yesu tuwe safi mbele za Bwana sifa na heshima ni vyako uliyeumba mbingu na nchi uliyemuumba kila mwanadamu kwa mfano wako mwenyewe Katika jina LA Yesu nimeomba Na kuamini Amen*
JUMAPILI NJEMA NA IBADA NJEMA WOTE

