Makapuku Forum

Makapuku Forum

Udakuu na umbea . .
67b77a4bdc79b53fabafa1c22251141f.jpg
 
Tuwe na siku njema ...

Na mimi leo nimeamua kufata mawazo ya binamu wangu Obe ...make kanambia mfano ujitoe ufahamu Valentine' flower ukijibana 30,000...Valentine dinner kitu cha kuanzia 50,000
UEFA CHAMPIONS LEAGUE mechi kubwa kwenye vibanda vyetu ni buku aka elfu 1 ...cha kufia nini nawatakia mpira mwema ....
 
Muziki: Jana Sio Zamani

Hata huwa sijui zamani inaanzia lini lakini nina uhakika kabisa jana au juzi haiwezi kuwa zamani maana unaweza kukimbia na ukaifikia jana. Kama huamini hilo sio tatizo langu na kuonesha kuwa hili si tatizo langu ninakusalimia kapuku mwenzangu na kukuambia kuwa nilikuwa na siku njema.
Asante sana anko Lyon Lee kwa magazeti, unalifanya jukwaa hili kuwa zuri sana tunapoamka. Nikushukuru husna muba kwa kuja tena, nilikumiss sana. Simu yangu alikuwa nayo anko kwa hiyo kwa yale utakayoyasoma kuhusu lolote jua kabisa sikuwa mimi.

Muziki sasa, ninafurahi sana kukuona hapa Transcend , BlessedHope , Tumosa , Shunie mama wa Biko, Mkushi wa kusi , mzeewakungoa , Mndali ndanyelakakomu SHIMBA YA BUYENZE na wewe kapuku unayenifanya nije hapa kila wakati

Ahsante kwa mziki mzuri Obe
 
Magazetiii soon ...kwa udhamini mnono wa binamu wangu jamaa langu la faida lenye busara sema shida yake moja kubwa hapendii kupitwa na chochote kizuriiiii ....

...asante mjomba kwa magazeti, sasa kweli mtu unaweza kupingana na mambo ya sili au ukoo. Mimi mwenyewe nimefuata mkondo tu wa ukoo wenu
 
Tuwe na siku njema ...

Na mimi leo nimeamua kufata mawazo ya binamu wangu Obe ...make kanambia mfano ujitoe ufahamu Valentine' flower ukijibana 30,000...Valentine dinner kitu cha kuanzia 50,000
UEFA CHAMPIONS LEAGUE mechi kubwa kwenye vibanda vyetu ni buku aka elfu 1 ...cha kufia nini nawatakia mpira mwema ....

...akili za mjomba wangu zinajijua zenyewe, wala mimi sijawaza alivyowaza. Mimi nimewaza mengine kabisa kwenda kutafuta single bar tufanye kolabo
 
Tafasiri Unavyoweza: Love Is Love

Mambo ya Valentine leo. Itoshe tu kusema leo ni siku ya wapendanao na kama unaifuata au kutoifuata basi haizuii siku hii kuwepo na kusheherekewa na wengi duniani. Usipoisheherekea hautokuwa wa kwanza kutoisheherekea maana wapo wengi wasioisheherekea kama walivyo wengi wanaoisheherekea. Tafasiri Unavyoweza.

Siku zote kijiwe hiki ni kigumu, hivi ndivyo ninavyojionea mwenyewe, kama wewe unakiona ni rahii basi ndo maana kikaitwa tafasiri unavyoweza. Wengi wanakiona mambo yake magumu na wengine wanakiona mambo mepesi kabisa haya yanayoandikwa hapa. Tofauti zetu ndo umoja wetu.

Kila mmoja ana tafasiri yake ya siku ya wapendanao, wengine huichukulia kama siku ya familia, wengine siku ya wapenzi na kupenzishana, wengine siku ya jamii na kujamiiana. Ilamradi tu kila mmoja anakuwa na tafasiri yake basi itoshe tu kukwambia Love is Love na tafasiri unavyoweza. Happy Valentine's Day. Na kukukumbusha tu, kwa wale wenye siku hii (Waroma) leo imeangukia kwenye siku ya majivu. Kumbuka tu kuangukia kwa siku hii leo kuna maana kubwa sana, Mungu yupo nasi kwenye mahusiano tuliyonayo iwe kifamilia, kijamii bila kujamiiana na kitaifa bila kuhitilifiana.

Happy-Valentines-Day.png
 
Muziki: Jamii na Kujamiiana

...nianze kwa kukutakia Jumatano nzuri ya majivu, kwa sasa kuna watu watatulia kwa kaucha kunywa pombe na kuamsha tamaa zao za mwili wakazihamishia kwa wengine, sio mmoja kama inavyotakikana bali kupunguzia tamaa za mwli kwa wengine hata kama hamko pamoja ila mmekubaliana. Nakusalimia Kapuku mwenzangu na kukutakia Valentine's day njema pia ambayo ndo inaishiria kwa sasa na ninaamini kabisa upo panapostahili kuwepo muda huu, chumbani.

Nilikuwa naongea na mjomba wangu na baada ya kuona sasa anataka damu nyeupe akaingia zinapopatikana na akawka miadi na ili kuikamilisha ikabidi apate upembuzi yakinifu wa gharama zitakavyokuwa. Kununua ua, kulipia meza maalum na kulipia malzi (hakupanga kurudi kwake), gharama ikawa ni milioni 22 tu, pesa za kitanzania. Hamad, kuona hivyo mjomba wangu akakumbuka kuwa leo kuna mechi za uefa akazima simu na kuamua kwenda kwenye banda umiza kuangalia mpira. Hili banda analipenda maana pembeni yake yupo Zuena mpika chapati mwenye uzuri unaompendeza. Na anko akaagiza afungiwe chapati atakuja kuzichukua game likiisha, maana yake anambeba mwenye chapati na chapati

Muziki sasa, nikutakie kwaresma njema na muendelezo mzuri wa siku ya Wapendanao. Unajua nakupenda

Asante Obe
 
Kumekuchaa na makuchaa yakeee.. .

Taarifa kwa umma: usku wa jana binamu Obe kaletewa zawadii ya ua japo ni jeusiii tiiii kutoka kwa mama ashura naona penzi lao limechipuka tena ...

Kwa waliomua kuitumia siku ya jana kwenye vibanda umiza kama mimi tulifaidii ...achana na story eti nilipitia kwa muuza chapati ni nongwa tu za binamu...

Soon magazeti
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom