Makapuku Forum

Makapuku Forum

Tafasiri Unavyoweza: Mwalimu Andaa Raia Mwema

Tunaweza kuwa na uelewa wa nani ni raia mwema, ndiyo, wale walio magereza tunaweza kuwaona kuwa hao si raia wema na ndiyo maana wako jela. Lakini vile vile tunaweza kukubaliana au kutokubaliana kuwa walio uraiani wengi wetu tunastahili kuwa jela kwa sababu tu sheria haijatuona. Ndo uzuri wa sheria zetu, zinaona na wakati mwingine zinaacha kuona na wala hazijapofuka maana kupofuka si kutoona kwa tafasiri ngumu. Tafasiri unavyoweza. Mwalimu usifungwe, andaa raia mwema.

Raia mwema aliyekamilika ni yule anayesimama na kuhoji mamlaka juu ya hatua inazochukua bila kumtaarifu, ujue raia mwema ndo anaipa mamlaka serikali na kama inafanya kwa niaba yake bila kumtaarifu basi ni wajibu wake kufungua mdomo na kuhoji wala si kukaa na kupiga makofi kwa kitu asichoelewa. Raia mwema ni zao la mwalimu mzuri, ndiyo mwalimu wa shule na nyumbani, mwalimu anayemwandaa raia mwema kuwa mpiga kura anayetambua thamani ya kura yake, mwalimu anayemwanadaa raia mwema kujua umuhimu wa kulipa kodi na kuhoji matumizi yake, mwalimu anayemwandaa raia mwema kusaka maarifa na kuwa mhojaji (inquisitive).

Tafasiri unavyoweza, mwalimu mwandae raia mwema ambaye anaweza kubuni na kuleta maendeleo yatakayolinufaisha taifa zima na wakati huo huo faida itakayopatikana isishikiriwe na wachache bale wote tufaidike nayo (a privatized profit while the risks and failures are communalized). Mwalimu una nafasi na kama unadhani mwalimu ni yule anayekaa darasani basi unaweza kutafasiri unavyoweza maana leo ni mwalimu kumuandaa raia mwema.
 
Tafasiri Unavyoweza: Mwalimu Andaa Raia Mwema

Tunaweza kuwa na uelewa wa nani ni raia mwema, ndiyo, wale wasio magereza tunaweza kuwaona kuwa hao si raia wema na ndiyo maana wako jela. Lakini vile vile tunaweza kukubaliana au kutokubaliana kuwa walio uraiani wengi wetu tunastahili kuwa jela kwa sababu tu sheria haijatuona. Ndo uzuri wa sheria zetu, zinaona na wakati mwingine zinaacha kuona na wala hazijapofuka maana kupofuka si kutoonakwa tafasiri ngumu. Tafasiri unavyoweza. Mwalimu usifungwe, andaa raia mwema.

Raia mwema aliyekamilika ni yule anayesimama na kuhoji mamlaka juu ya hatua inazochukua bila kumtaarifu, ujue raia mwema ndo anaipa mamala serikali na kama inafanya kwa niaba yake bila kumtaarifu basi ni wajibu wake kufungua mdomo na kuhoji wala si kukaa na kupiga makofi kwa kitu asichoelewa. Raia mwema ni zao la mwalimu mzuri, ndiyo mwalimu wa shule na nyumabni, mwalimu anayemwandaa raia mwema kuwa mpiga kura anayetambua thamani ya kura yake, mwalimu anayemwanadaa raia mwema kujua umuhimu wa kulipa kodi na kuhoji matumizi yake, mwalimu anayemwandaa raia mwema kusaka maarifa na kuwa mhojaji (inquisitive).

Tafasiri unavyoweza, mwalimu mwandae raia mwema ambaye anaweza kubuni na kuleta maendeleo yatakayolinufaisha taifa zima na wakati huo huo faida itakayopatikana isishikiriwe na wachache bale wote tufaidike nayo (a privatized profit while the risks and failures are communalized). Mwalimu una nafasi na kama unadhani mwalimu ni yule anayekaa darasani basi unaweza kutafasiri unavyoweza maana leo ni mwalimu kumuandaa raia mwema.
Mkuu
Asante sana
 
Muziki: Kukana, Usizungushe Macho

...baadhi ya Makapuku wako kwenye mfungo (lent/fasting almaarufu Quadragesima- tamka Kwaresma maana hilo gumu ni neno la kilatin), hongera na nawatia moyo maana ndo kwanza bado majivu yako kwenye paji la uso kwa wale wasiopenda kuoga na kunawa uso, wanajijua. Nikusalimie Kapuku wewe ambaye Jumatano ya Majivu uliiunganishia na Valentine-siku ya wapendanao na pamoja kufanya viunganishio bado uliweza kurudisha chumba cha guest kabla ya saa nne asubuhi haijafika.

Mjomba wangu Lyon Lee kakana kabisa kuwa hakuondoka na muuza chapati baada ya gharama za ampendae kuwa shilingi milion ishirini na mbili tu bila senti. Unajua ukitaka kukana juu ya jambo fulani basi lazima macho yawe makavu, sio unakana huku unachezeshachezesha macho kama macho ya panya. Mjomba anakana huku macho anayakwepeshakwepesha kama anapigwa picha ya fulashi, kwachaaaaaa. Uzuri ni kuwa aunty yangu hayajui haya maana mjomba aliaga anaenda semina Kilombero.

Muziki sasa, macho huongea ukweli, jaribu kufuatilia yaani ukiweza kaa kwenye kioo chako halafu mikono yako idanganye, yaangalie macho ynachofanya. Burudika na muziki

Mkuu shikamoo

...mbona unasalimia huamini kama salamu inanifaa
giphy-95.gif
 
binamu niko kilombero nimepanda gari asubuh na mapema ..kurudiii tumuombe Allah

Asante kwa music mzuri
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom