Makapuku Forum

Makapuku Forum

Tafasiri Unavyoweza: Mapuuza

Nimesoma shule nyingi nyingi sana hadi namaliza elimu ya sekondari, tafasiri unavyoweza. Sio wote wenye tulikuwa na uwezo wa kuanza kidato cha kwanza hadi cha nne katika shule moja tu. Mikasa ya kibinafsi na ya kiujumla inasababisha uhame hame, shule moja kwenda nyingine lakini kutokana na ukweli kuwa kichwani nilikuwa timamu nilimaliza na kufaulu kuendelea na elimu ya juu ya sekondary.

Katika michakato yote hii nilijifunza mengi, ya darasani nitayaacha maana wote mliomaliza sekondari si mlikuwaga wa kwanza kila muhula. Nitaeleza ambayo nilijifunza nje ya darasa na hasa kupitia kwa mwalimu mmoja na mwanafunzi mwenzangu wote walikuwa wakikerwa na upuuzi, mmoja akikerwa na upuuzi unaofanywa na wanafunzi kiasi kwamba tukambatiza/silimisha na kumuita mwalimu mapuuza. Mwanafunzi yeye alikerwa na upuuzi wa walimu na utawala wa shule, huyu hakubatizwa wala kusilimishwa alipewa adhabu ya kung'oa visiki.

Tafasiri unavyoweza, hakuna kitu kibaya kama kupuuzia vitu ambavyo ni muhimu, masuala ya msingi. Wengi tumekuwa tukipuuzia masuala kwa sababu tu hayatuhusu, sio ya kwetu. Kuna vingi tunapuuzia kama taifa, uonevu wa wazi wa raia, kupotea kwa raia, ukosefu wa ajira, siasa isiyohimiza utangamano (harmony), siasa ya kujiona m-bwana na mwingine m-twana, kisa tofauti ya itikadi. Hatufiki kwa sababu hayajatufika. Simama uhesabiwa na kataa upuuzi wa kuweka mipaka katika taifa endelevu. Matukio ya wasiojulikana tunapuuzia, subiri wasiojulikana wakija kukujulia hali wakiwa wamevaa gwanda ulizolipia kodi.
Tafasiri unavyoweza, mapuuza huzaa ajali na hauwi salama kwa kukaa kupuuzia masuala kisa yako kwa mwenzako, kwako yanakuja FYI.
 
Wana-KF habari zenu Kwa jumla.... Shemeji yangu Lee, mtani wangu Obe &Muba... Wajukuu zangu Shunie na Tumosa... Marafiki zangu shimba wa buyenze ,Sakayo & Transcend, Shedede, Mama mchungaji Madame S and all fellow kapuku...... I wish you all a happy and prosperous New Year
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom