Husna Muba
JF-Expert Member
- Jan 28, 2017
- 14,524
- 44,585
Mi ni mmoja kati ya mamod'sNi ya kwako hii shemeji?
Mi ni mmoja kati ya mamod'sNi ya kwako hii shemeji?
Mi ni mmoja kati ya mamod's
NUKUU YA LEO
The future belongs to those who prepare for it today
Maisha ya baadaye ni ya wale wanaoweza kuyaanda leo
Haya maneno yalipatwa kutamkwa na Mwanaharakati na mmarekani mweusi Malcolm Little au Malcolm X ambaapo pia aliitwa el-Hajj Malik el-Shabazz.
Malcolm Alifariki akiwa na miaka 39 kwa mauhaji yaliyofanyika NY katika kitongoji cha Manhattan kwa kupigwa risasi 21 kifuani
Hata hivyo Malcolm X aliacha watoto 6 na mjane mmoja.
Mliopata kusoma historia ya taifa la marekani na pan-africanism mtakuwa mnamkumbuka huyu jamaa vizuri.
![]()
![]()
Wakuu:
Tuandae kesho yetu leo! Ukitakata uwe na nyumba mwakani lazima ujiandae leo! Ukitaka kuwa mtu wa namna fulani lazima ujiandae leo..!
Make your tomorror!
Transend ..
LEO KATIKA HISTORIA:
1965 - Malcolm X anauliwa kwa kupigwa risasi.
Alikuwa ni mwanaharakati kutoka Nchini Marekani.
Shikamoo binamuTafasiri Unavyoweza: Miliki Unachoamini
Ni Jumanne leo, hilo halina ubishi kwa wengi wetu na kama unaamini kuwa leo ni leo basi hii ndo mada yangu ya usiku huu. Miliki Unachoamini, hapa simaanishi tu kumiliki yanayoshikika (tangible) Bali hata mawazo, maoni na lolote unalojua unaweza kumiliki.
Tumekuwa tukisikia zaidi na zaidi kuhusu watu wasiojulikana, hawa kwangu wanabaki kuwa ni watu waoga. Kutojulikana kwa lugha rahisi ni fahari ya mtu mwoga/uoga (cowardice), muovu, mwenye hila, mshakunaku na zaidi ni mtu mwenyewe husuda aliyetawaliwa na nia ovu juu ya mwingine mmoja au kikundi.
Kutojulikana mara nyingi kunakupa nafasi ya kumchafua mtu, kuzusha na hata Kama kuna vijifaida vya kutojulikana , lakini kama unajiamini umesimama mstarini, kwanini usimiliki unachokiamini na kila mmoja akajua.
Tafasiri Unavyoweza. Usiku mwema

Nimekumis wewe mtuMi ni mmoja kati ya mamod's
Ankoooooo....wow! Hongera wangu
Muziki: Hugh Masekela
Inawezekana ukawa ndo unamsikia leo, lakini kwa wakongwe, well hata sisi vijana wa jana tunaopenda muziki wa Jazz tumemsikia na kusikiza nyimbo zake. Anitwa Hugh Masekela, nguli ambaye kama ilivyo kwa maisha ya mwanadamu yeyote aliyezaliwa, kafariki leo kwa tatizo la saratani.
Je, uliangalia World Cup iliyofanyika South Africa, kama uliangalia ufunguzi basi utakuwa ulimuona mtu mzima mmoja akiwa kashika midomo ya bata, ambayo ni chombo muhimu katika muziki wa Jazz, alikuwa akitumbuiza na mkongwe mwingine Femi Kuti. Ilikuwa poa sana. FYI, alimuoa Miriam Makeba na baadaye waliachana ila waliendelea kufanya muziki pamoja. Alijiingiza kwenye ulevi na madawa lakini alifanikiwa kuacha, inawezekana.
Muziki sasa, leo sitaki nikuchoshe kwani ninaangalia maisha yake kimuziki muda huu. Pumzika kwa amani Hugh Masekela
![]()
![]()
Tafasiri Unavyoweza: Usingizi, Dawa Kulala
Usingizi ni moja ya utajiri ambao kila mmoja wetu amejaaliwa na Muumba, hilo halina ubishi. Viumbe hai vyote husinzia kila kimoja kwa wakati na muda wake.
Tafiti zinatuonesha kuwa zaidi ya theluthi moja ya maisha yetu wanadamu tunaitumia kulala (seaward, 2015). Kulala ni kitendo kizuri na hapa ni lazima ujue kuna tofauti ya kulala na kulalana, naongelea kitendo nilichoandika kwanza.
Mfumo wa maisha ya kisasa na michakariko ya kusaka maisha yametufanya wengi wetu kuuchukulia usingizi kama kitu poa tu, hakina umuhimu sana na si ajabu mtu kuamka saa kumi na moja alfajri ilhali kalala saa nane usiku. Mtu mzima unapaswa ulale masaa kati ya 6-8 kwa usiku, lakini hatuyapati masaa haya kutokana na sababu kadha wa kadha ima kazi, starehe au imani.
Tafasiri unavyoweza, usingizi ni jibu zuri kwa uchovu unaokuwa nao kwa siku nzima, ukiukosa usingizi akili itachoka na mwili utakuwa dhaifu na hii si afya njema kwa mwili na akili. Dawa ya usingizi, kulala.
![]()

Muziki: Hisia Hazizuii Ukweli
....ninatamani kumsalimia kila mmoja ambaye ni mdau wa jukwaa hili kwa kumtaja jina, lakini rasilimuda hauniruhusu kwani nilitumika kisawasawa leo. Itoshe tu kusema kwamba, wewe uliyehapa unalifanya jukwaa hili kuwa sehemu nzuri ya kuja kila wakati, Asante sana.
Ukitegemea hisia kuwasilisha ukweli (relying on illusions to convey realism ) utakuwa unajisumbua bure. Hisia si mara zote huwa ukweli na hutofautiana sana na ukweli. Ukweli una vithibitisho, ukweli una rejea, ukweli una mashiko na zaidi ukweli utakuweka huru. Hisia hazishikiki, zinakufunga kuutazama ukweli.
Muziki sasa, kuwa na hisia husaidia ikiwa tu utajiachia sawia kuzitafutia hisia ulizonazo ukweli.
Kawaida tu ucjal....wow! Hongera wangu
