Muziki: FurahiDay Mdau Mwaminifu
...maneno machache kwa sababu ya ukimya unaoendelea kutamalaki humu jamvini. Hakijaharibika kitu maana bado wengi wetu tukipata muda tunachungulia na kusmile kisha tunaendelea tunapotaka kwenda, JF ni kama bahari, kubwa mno kuanzia jukwaa la juu hadi la chini, hapo sijaoongea vijijukwaa vya msimu. Uzuri ni kuwa Makapuku ilionekana kuwa ya msimu lakini imesimama kuliko moja. Hongera kwako unayelifanya jukwaa hili kuwa sehemu nzuri kuwepo.
Muziki sasa, sijaacha kuwakumbuka hata kidogo, mnalijua hilo. Nakutakia wikend njema mdau mwaminifu