Makapuku Forum

Makapuku Forum

ISAYA 49

15.Lakini Mwenyezi Mungu asema:"Je mama aweza kumsahau mwanawe anayenyonya,
asimwonee huruma mtoto wa tumbo lake?

Hata kama mama aweza kumsahau mwanawe ,mimi kamwe siwezi kukusahau.


USIKU MWEMA MUNGU AWABARIKI DAMU YA YESU ITUFUNIKE MBARIKIWE
MUNGU HATAWASAHAU
Eeeeemeeen
 
TUOMBE
Mwenyezi Mungu Mtakatifu, Mfalme wa wafalme,Baba wa Milele,Mshauri wa Ajabu,Mungu mwenye Nguvu Asante kwa kutufikisha siku hii ya leo JU JUMAPILI YA KWANZA YA MWAKA ,7 JANUARI 2018 salama wako wengi walitamani kuiona siku ya leo hawajaweza sisi ni nani Baba Mtakatifu
Tunakushukuru kwa sababu Upendo wako ni mkuu kwetu, Kwa sababu unatulinda na kutuongoza, Kwa sababu unatupigania, Kwa sababu Unaweza yote,Unajua yote,Upo kila mahali. Mungu wetu tunaomba usinyamaze kila tukuitapo sisi peke yetu hatuwezi.
Tupiganie katika kila Jambo,Tufundishe,tushauri na kuturudi tunapokukosea. Mungu bariki Afya,Kazi,kusudi,Uchumi na Imani zetu.
Waponye wagonjwa wote Baba majumbani na mahospitalini,
fariji wafiwa wote wape faraja yako popote walipo,angalia wajane,wagane,
yatima Baba wape hitaji la mioyo yao,wasaidie wote wanaopitia changamoto mbalimbali.
Wasaidie wasafiri wote kokote waendako majini,nchi kavu na angani waende na kurudi salama..ponya mioyo yote inayotaabika kwa huzuni ,taabu na dhiki ,mateso tuongezee imani Baba tukuangalie wewe tu maana wewe Baba hukawii wala huwahi jibu lako ni ndiyo.Roho Mtakatifu kaa nasi siku zote za maisha yetu.
Ni katika Jina la Yesu tunaomba tukiamini na kushukuru Amina.


JUMAPILI YA KWANZA 2018 NJEMA,MUNGU AONEKANE KWETU KATIKA IBADA ZOTE SIKU NJEMA MBARIKIWE.
Amin
 
HII NDIO TANZANIA NA HAWA NDIO WATANZANIA WANAOMKA ASUBUHI NA KUJADIL UPUPU BADALA YA NAMBA..SHAME!!
 
Kwanza kabisa, karibu sana Makapuku Forum, na Heri ya 2018!
...oh! Sikujua hili, asante sana kwa ushauri. Kwa kuwa umekuja kwenye huu uzi basi nategemea utashare mafanikio uliyoyapata kwenye 'nyuzi' tofauti na hii.

Niwie radhi pia kwa kutodadavua maana ya mafanikio. Kwa kuwa unaonekana kuwa na mafanikio hebu share basi nami ili nibadilike mzee mimi niwe kijana kama wewe
 
...interesting! sikujua kama mtu anayejua mafanikio anaweza ijua misukule ya ushirombo!
Kwa kuwa ukapuku huanzia kichwani, basi nikisema utajiri huanzia kichwani nitakuwa sijakosea, sawa!
Sasa wewe unayeona hapa hatuongelei mafanikio, unaweza kuwa na sababu ya wewe kuja na hitimisho la kunishauri mimi mzee nibadilike? Yaani uchaguzi wangu binafsi wa kuwa hapa unakuumiza roho wewe, ajabu sana.

Jipe nafasi, toka kwenye hisia usake uhalisia wa Makapuku. Usiyafanye maisha kuwa magumu sana kwa kuimba mashairi ya kina Tambalizeni na kukaririri vitabu vya nguli Topan (1971).

Mimi kama mimi nimeamua kuwa hapa na kujiita Kapuku ni hiari yangu, shida yako kwa hili inatoka wapi? Au unajiona kama nabii uliyekuja kuni'komboa'?
 
Muziki: Unataka Kukijua, Kifundishe

...u khali gani wewe Kapuku mheshimika!? Unajua kabisa ninapokuuliza hali huwa siulizi swali kwamba ujibu maana majibu yako yanatofautiana na ya kwangu na ya yule. Kila mmoja akija na jibu lake tutakesha hapa na kukesha kwetu hapa ndiko kunalifanya jukwaa hili kuwa sehemu nzuri na bora kabisa ya kuwepo. Tuko hapa kuelimishana, kubadilishana mazuri ambayo yanaendelea kati yetu iwe ya kikazi, mahusiano, shule, siasa na maisha kwa ujumla. Hapa ni sehemu nzuri kwa sababu wewe upo, usingekuwepo hapa, hakyanani tena MF ingekuwa ishapotea kitambo, ipo kwa sababu upo. Asante.

Unaweza kuniona kama mkongo kwa namna navyopenda kushout out majina, utajiumiza roho kukereka na hiki ninachofanya maana siwezi kuacha kukifanya. Nina show appreciations kwa wadau wanaolifanya jukwaa hili kuwa bora wakati wote, fyi, hakuna Jukwaa ambalo limeanzishiwa nyuzi nyingi kama hili, kwanini, mti wenye matunda ndo upopolewao. Asante sana shululu kwa magazeti, asante BlessedHope kwa nukuu zenye kujenga imani. Nikushukuru Tumosa kwa kulifanya jukwaa hili kuwa sehemu nzuri kabisa kuwepo. Karibuni sana jukwaani Te Lavista Demiss The List , hapa mtaungana na anko wangu Lyon Lee , Shunie , husna muba , Tetramelyz , Jimena , Bitoz , SHIMBA YA BUYENZE , Werrason , Mussolin5 , ABJ , moneytalk , dumejeuri , Mndali ndanyelakakomu , Sakayo , Transcend , Nyagei , makaveli10 na wadau wengi wa jukwaa hili adhimu.

Muziki sasa, kuna msemo maarufu kwenye kuta za ualimu 'if you want to lean a subject, teach it. Kufundisha sio kusimama mbele peke yake, ni kujiandaa ili kuondoa maswali utakayokutana nayo kwa wanafunzi makini. Na ninakuongezea hiki, ukitaka kupata maarifa juu ya kitu chochote, basi andika kuhusu hicho kitu. Utajua mengi kwani hutaishia kukwaruza kalamu kwenye karatasi peke yake, utatafiti na kuja na hitimisho utakalopenda kushare nasi hapa. Hii ndo tofauti yetu na wengine. Usiku mwema


Nawe pia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom