Makapuku Forum

Makapuku Forum

Tafsiri Unavyoweza: Maua

Dunia yetu inapambwa na vitu vingi vya kuvutia, vingi sana na ukiweza kuvitaja vyote itachukua muda kuvimaliza. Kuanzia ndege wanaokuamsha asubuhi hadi wale wanaokutisha usiku. Wanyama tuwafugao na wale tunaoenda 'kutalii' mbugani kuwafurahia. Samaki majini na wadudu watambaao na warukao. Ni mengi yanayoupamba ulimwengu na dunia yetu. Kuna yale unayopenda kuyaona, kuyaangalia na kuyafurahia, yapo usiyopenda kuyaona au kuyaangalia kwa sababu unayachukia. Mengine una hofu nayo maana unayahusisha na matokeo mabaya. Mimi nayaangalia maua leo, tafsiri unavyoweza!

Tangu enzi na enzi, watu tumekuwa tukipenda maua. Mfalme Sulaiman (Solomon) aliyechukua madaraka baada ya mfalme Daud alipenda maua na alisema yanapendeza kuona. Kila mmoja anatafasiri yake ya maua, nawe tafasiri unavyoweza.
Maua ni mapambo yenye harufu nzuri, yanavutia na yanapendeza kuona.
Dhana ya kuhusianisha maua na jinsi ya kike sitaianzisha mimi, imekuwepo tangu zama za kale, mwanamke ni pambo la nyumba. Maana yake nyumba isiyo na ua linaloipamba haijakamilika. Utaugua ukilikosa ua ndani ya nyumba yako. Ua ni tiba, linaleta kujiamini na mara zote ukilitunza likapendeza linakupa tabasamu na nguvu ya kuamka kila siku.
Usisahau kulimwagilia maji ua, litapendeza sana vinginevyo litakauka na kusinyaa, lisivutie tena na utamani kulitupa nje ya macho yako maana moyo haupendi kuona kitu kilichosinyaa.
Tafasiri unavyoweza, mimi nimeangalia maua, maana nayapenda
Beautiful-green-600x399.jpg

flowers.gif
 
Ubarikiwe Obe asante kwa ushauri wa kumwagilia maua

Sent from my TECNO H6 using JamiiForums mobile app
 
Muziki: Unataka Kukijua, Kifundishe

...u khali gani wewe Kapuku mheshimika!? Unajua kabisa ninapokuuliza hali huwa siulizi swali kwamba ujibu maana majibu yako yanatofautiana na ya kwangu na ya yule. Kila mmoja akija na jibu lake tutakesha hapa na kukesha kwetu hapa ndiko kunalifanya jukwaa hili kuwa sehemu nzuri na bora kabisa ya kuwepo. Tuko hapa kuelimishana, kubadilishana mazuri ambayo yanaendelea kati yetu iwe ya kikazi, mahusiano, shule, siasa na maisha kwa ujumla. Hapa ni sehemu nzuri kwa sababu wewe upo, usingekuwepo hapa, hakyanani tena MF ingekuwa ishapotea kitambo, ipo kwa sababu upo. Asante.

Unaweza kuniona kama mkongo kwa namna navyopenda kushout out majina, utajiumiza roho kukereka na hiki ninachofanya maana siwezi kuacha kukifanya. Nina show appreciations kwa wadau wanaolifanya jukwaa hili kuwa bora wakati wote, fyi, hakuna Jukwaa ambalo limeanzishiwa nyuzi nyingi kama hili, kwanini, mti wenye matunda ndo upopolewao. Asante sana shululu kwa magazeti, asante BlessedHope kwa nukuu zenye kujenga imani. Nikushukuru Tumosa kwa kulifanya jukwaa hili kuwa sehemu nzuri kabisa kuwepo. Karibuni sana jukwaani Te Lavista Demiss The List , hapa mtaungana na anko wangu Lyon Lee , Shunie , husna muba , Tetramelyz , Jimena , Bitoz , SHIMBA YA BUYENZE , Werrason , Mussolin5 , ABJ , moneytalk , dumejeuri , Mndali ndanyelakakomu , Sakayo , Transcend , Nyagei , makaveli10 na wadau wengi wa jukwaa hili adhimu.

Muziki sasa, kuna msemo maarufu kwenye kuta za ualimu 'if you want to lean a subject, teach it. Kufundisha sio kusimama mbele peke yake, ni kujiandaa ili kuondoa maswali utakayokutana nayo kwa wanafunzi makini. Na ninakuongezea hiki, ukitaka kupata maarifa juu ya kitu chochote, basi andika kuhusu hicho kitu. Utajua mengi kwani hutaishia kukwaruza kalamu kwenye karatasi peke yake, utatafiti na kuja na hitimisho utakalopenda kushare nasi hapa. Hii ndo tofauti yetu na wengine. Usiku mwema

AYUBU 35

10.Lakini hakuna asemaye ,"Yuko wapi Mungu,Muumba wangu ,mwenye kunifanya niwe mchangamfu usiku..

DAMU YA YESU ITUFUNIKE USIKU HUU NA TUCHANGAMKE KULETA MAOMBI NA SHUKURANI KWA MUUMBA WETU.
 
Muziki: Unataka Kukijua, Kifundishe

...u khali gani wewe Kapuku mheshimika!? Unajua kabisa ninapokuuliza hali huwa siulizi swali kwamba ujibu maana majibu yako yanatofautiana na ya kwangu na ya yule. Kila mmoja akija na jibu lake tutakesha hapa na kukesha kwetu hapa ndiko kunalifanya jukwaa hili kuwa sehemu nzuri na bora kabisa ya kuwepo. Tuko hapa kuelimishana, kubadilishana mazuri ambayo yanaendelea kati yetu iwe ya kikazi, mahusiano, shule, siasa na maisha kwa ujumla. Hapa ni sehemu nzuri kwa sababu wewe upo, usingekuwepo hapa, hakyanani tena MF ingekuwa ishapotea kitambo, ipo kwa sababu upo. Asante.

Unaweza kuniona kama mkongo kwa namna navyopenda kushout out majina, utajiumiza roho kukereka na hiki ninachofanya maana siwezi kuacha kukifanya. Nina show appreciations kwa wadau wanaolifanya jukwaa hili kuwa bora wakati wote, fyi, hakuna Jukwaa ambalo limeanzishiwa nyuzi nyingi kama hili, kwanini, mti wenye matunda ndo upopolewao. Asante sana shululu kwa magazeti, asante BlessedHope kwa nukuu zenye kujenga imani. Nikushukuru Tumosa kwa kulifanya jukwaa hili kuwa sehemu nzuri kabisa kuwepo. Karibuni sana jukwaani Te Lavista Demiss The List , hapa mtaungana na anko wangu Lyon Lee , Shunie , husna muba , Tetramelyz , Jimena , Bitoz , SHIMBA YA BUYENZE , Werrason , Mussolin5 , ABJ , moneytalk , dumejeuri , Mndali ndanyelakakomu , Sakayo , Transcend , Nyagei , makaveli10 na wadau wengi wa jukwaa hili adhimu.

Muziki sasa, kuna msemo maarufu kwenye kuta za ualimu 'if you want to lean a subject, teach it. Kufundisha sio kusimama mbele peke yake, ni kujiandaa ili kuondoa maswali utakayokutana nayo kwa wanafunzi makini. Na ninakuongezea hiki, ukitaka kupata maarifa juu ya kitu chochote, basi andika kuhusu hicho kitu. Utajua mengi kwani hutaishia kukwaruza kalamu kwenye karatasi peke yake, utatafiti na kuja na hitimisho utakalopenda kushare nasi hapa. Hii ndo tofauti yetu na wengine. Usiku mwema

Lala salama Obe ubarikiwe asante kwa wimbo
 
Muziki: Likizo Imeisha

Nimekaa wakati nataka kuanza kuandika kipengele hiki leo, nilitaka nibadili style yangu ya kuandika lakini nikasita kidogo. Ieleweke kwanza kabla sijakusalimia na kukuambia namna nilivyoimaliza likizo yangu vizuri huku kijijini. Kubadili kitu si jambo baya na ndiyo maana wengine tunapouanza mwaka huwa tunaamua kubadili baadhi ya vitu vyetu vya ndani na vya nje. Naamini unanielewa na kama kunielewa ni ngumu basi usikonde maana frahiday si siku unayotakiwa kuifanya kuwa ngumu sana.

Mara ya mwisho naandika hapa hadi unaponisoma leo zimepita text 611, na nimezisoma zote na sikuweza kuchangia kutokana na changamoto ya mtandao na mambo kama hayo na nikiungana na mdau uliyeshangaa kuwepo kwa post 11 tu kwa siku basi Makapuku hebu tutoke tulipo, turudi tulisongeshe group letu. Asante kwa wote mnaozidi kulisongesha.
Muziki sasa, leo narudi zamani na zamani kwangu naliangalia gitaa na 'utamu' linaoleta kwenye muziki. Nikutakie wikend njema na nikukumbushe tu, likizo imeisha

Similar Discussions

Back
Top Bottom