Makapuku Forum

Makapuku Forum

Tafsiri Unavyoweza: Ajira

...ajira inahusisna na kitendo cha kufanya kazi kwa ujira/malipo. Malipo/ujira yapo ya aina nyingi, fedha na ujuzi vikiwa ni moja ya malipo. Hakuna ubishi kuwa Tanzania kuna tatizo la ajira, tena likiwa kubwa miongoni mwa vijana. zipo takwimu zinazokadiria kuwa angalau watu 900,000 huingia mtaani kusaka ajira kila mwaka, wengi wao wakiwa ni vijana. Ninajiaminisha takwimu hizi zimeongezeka maana kuna uandikishaji mkubwa wa vijana shuleni na vyuoni.

Kufanya kazi ni haki ya kila mwenye uwezo wa kufanya kazi. shida inatokea pale mwenye uwezo huo wa kufanya kazi anapokosa hiyo kazi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo, mtaji, ujuzi na miundombinu inayowezesha mtu kufanya kazi. Kukosa kazi si jambo zuri si tu kwa mtu anayekosa kazi bali pia kwa serikali na jamii kwa ujumla.

Kijana asiye na mwenye nguvu za kufanya kazi asiwe na kazi ni kama bomu la muda, saa yoyote linalipuka na kama lisipolipuka lenyewe basi kuna uwezekana rahisi wa kulipukishwa na yeyote mwenye nia ovu dhidi ya jamii anayoishi kijana huyu.
Zama za serikali kuwa mwajiri mkubwa nchini zimepita, tuko kwenye zama za serikali kuweka miundombinu ikiwemo sera kamilifu za kutatua tatizo la ajira nchini. Sekta binafsi ipewe kipaumbele ili iajiri wengi, hizi habari za cherahani nne ni kiwanda ni propaganda zisizo na mashiko.
Mtazamo wangu binafsi; sekta ya kilimo inaajiri wengi lakini haijapewa mkazo mkubwa nchini, bajeti iongezwe kama azimio la Maputo lilivyosema. Mwaka jana sekta ya kilimo ilitarajiwa kupanda kwa 2.9 asilimia lakini ilifikia asilimia 2.1 tu. Fedha haikupelekwa ilivyohitajika
Vyuo vya kati viimarishwe na kuwafikia wengi zaidi
Umeme uwepo wa uhakika sio huu ambao mvua ikinyesha tu umekatika
Kufanya kazi iwe ni imani inayoanzia nyumbani, kisha waajiri kuanzia wenye mikahawa wawape kipaumbele vijana katika kuwapatia kazi.

Hii ni mada yenye mambo mengi, lakini tafasiri unavyoweza, bila kuwapatia ujuzi vijana wetu, soko la ajira ni gumu kuliko maelezo.
main-qimg-fa3872ca8d90059901d84233cf8b3750-c
 
Muziki: Laumu Ufiche Udhaifu

...saikolojia ya mtu anayeshindwa kufanya yanayomuhusu mara nyingi humtuma kufuata kuangalia wengine wanaofuata yao wanafanikiwa bila kuingilia uhuru wake. Ule msemo unaosema pambana na hali yako una maana kubwa sana. usiuchukulie poa hata kama nimeanza kipengele hiki ninachokipenda bila kukusalimia. Najua unajua kabisa salamu ndo msingi wa mawasiliano.

Nirudi kwenye ambacho ninataka kusema, nisitoke msitarini. Mara nyingi mtu anayeshindwa kufanya mambo yake hubaki na jicho la kipanga kuangalia wengine/mwingine anafanya nini. Na kwa kujifanya kuona makosa ya mwenzake basi hujifanya mwalimu wa kile ambacho mwenzake anakifanya. Kukumbusha tu ni kuwa yeye kashindwa kufanya kinachomuhusu na anajongea kwako unayemind your own business na kujifanya kukuambia namna nzuri ya kufanya unachofanya.
Huwezi kunifundisha kitu kama hujaamua kujifunza kwanza, nilisema jana.
Huna haja ya kujidai kulaumu kitu ambacho hakikuhusu ili ufiche udhaifu wako.
Muziki sasa, maisha ya kulaumu hata siku moja hayajwahi kuwa na suluhisho, yanaishia kulalamika mwanzo mwisho na lalamiko lenye lawama hata siku moja halijawahi kuwa na suluhisho, kaa ukilijua hilo. Udhaifu wako ni nguvu yako, ifanyie kazi

Asante kwa maneno mazuri ya kujenga Obe.......... hakika fuata yako kuliko kufuatilia ya watu kwanza hutayaweza maana hayakuhusu...MUNGU ATUSAIDIE TUJIPENDE NA JUSHUGHULIKIA KILA MMOJA LAKE ILI TUWABARIKI WENGINE ...Mungu akubariki KWA MUZIKI WAKO ,UMETUBARIKI UMEKUWA WETU..USIKU MWEMA
 
ZEKARIA 2

5.Mwenyezi Mungu asema kuwa yeye mwenyewe atakuwa ukuta wa moto kuulinda mji huo pande zote,naye atakaa humo kwa utukufu wake.

Asante Mungu kwa usiku huu umetulinda mchana kutwa tunakushukuru,
sasa ni usiku tunalala..tunajua ahadi yako itatimia utakuwa ukuta wa moto katika mji huu pande zote na utakaa humu kwa utukufu wako..angalia familia zetu,watoto wetu,majirani zetu,marafiki zetu uwazingire kwa ukuta huu adui asipate nafasi asante maana tutakuwa salama usiku kucha..katika jina la Yesu tunashukuru na kuamini Amen
 
TUOMBE:

Mtakatifu Mtakatifu Mtakatifu Bwana Mungu wa majeshi Asante kwa wema na Upendo wako kwetu kwa kutupa neema hii yakuiona siku ya leo ALHAMISI 11 JANUARI 2018

Asante Baba unastahili kuabudiwa Mfalme wa Amani

Wapo wengi walitamani kuiona siku ya leo hawakuweza Baba kuamka kama tulivyo sisi leo .

Baba tunakuja mbele zako leo tukiomba toba Baba Utusamehe makosa yetu tuliyotenda kwa mawazo kwa maneno kwa matendo na kwa kutotimiza wajibu wetu kwa nafasi zetu zote tulizonazo kwa kujua au kutojua
Tunaomba pia kuwasamehe wote waliotukosea walioomba msamaha hata wasioomba msamaha

Tunakuja mbele zako tukiomba Utulinde Utuokoe katika ajali mbalimbali za kimwili na kiroho Uwalinde watu wote wa familia zetu wasaidizi majumbani wake Waume Wanandoa Wachumba watoto Ndugu Jamaa na marafiki

Baba tunaomba Roho Mtakatifu akae nasi atufundishe kukujua kukupenda kukuheshimu na kukutii wewe tu

Baba Waponye wagonjwa majumbani na mahospitali
Baba wewe ndie mponyaji wa kweli waponye wagonjwa wote watie nguvu ndugu wazazi na walezi onekana kwao waamini Uponyaji toka kwako

Baba tunaomba ponya d awa wanazotumia wagonjwa wote wabariki madaktari na manesi watie nguvu wanaoguza wasipungukiwe

Wafariji Wafiwa Wajane Wagane Yatima Wapweke Walea pekee wenye mahitaji mbalimbali

Wape utulivu na majibu Baba wanaotafuta watoto ,wenye madeni wanaotafuta kazi, wanaotafuta Ada , wanaotafuta kodi za nyumba wenye mitihani na wote wenye uchungu na kukata tamaa Waliokataliwa Wafungwa waoneshe ukuu wako Baba kuwa unawapenda siku zote za maisha yao wawe na amani wakupende na wakuone wewe katika kila pito.

Tunaomba kila tunapotoka na tunapoenda Uwe dereva na kiongozi wetu tulinde Nchi kavu Majini na Angani Damu ya Yesu itufunike tuangalie kwa wema tufike salama katika safari zote siku ya leo Mfalme wa Amani

Tunaomba uwabariki Viongozi wote wa Dini waweze kutuongoza vema kiroho na tuwe na hofu ya Mungu

Walinde viongozi wa serikali na wenye mamlaka waweze kuongoza vema na kuwa na mwenendo bora Nchi iwe na amani na utulivu.

Ponya kazi za mikono yetu Biashara Ajira Ujasiriamali uonekane Mfalme wa Amani tupate riziki kihalali

Baba tunayo mengi unayajua tunaomba uyapokee na utupatie sawasawa na mapenzi yako utupe kuvumilia katika Mapito mbalimbali kwani kwako yapo majibu huchelewi wala huwahi Mfalme wa Amani

Asante Baba kwa kuwa unatupenda na hujawahi kutuacha kila tukuombapo utatujibu sawasawa na mapenzi yako

Tunaomba Tunashukuru na kuamini katika jina la Yesu Amen.

DAMU YA YESU ITUFUNIKE,SIKU NJEMA
 
Amen
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom