Makapuku Forum

Makapuku Forum

JUMAPILI YA KWANZA 2018 NJEMA,MUNGU AONEKANE KWETU KATIKA IBADA ZOTE SIKU NJEMA MBARIKIWE.

f50a0d625cdef89f011d30afd196072f-rimg-w400-h300-gmir.jpg
[/QUOTE]
Ni baraka na mapenzi ya mwenyezi Mungu,wengi hawajaiona siku ya leo
 
Nafurahi kusikia umeamka poa.
Upande wangu niko poa kabisa, likizo imeisha sasa najiandaa na kuingia kwenye ujenzi wa taifa tu. Asante kwa kunijulia hali.

Vipi wikend ilikuwaje kwa upande wako?
Weekend ilienda poa kwani Mbeya jana kulikua na ki mvua mpaka mida ya jioni, ilikua ni fursa ya kushinda nyumbani wakati najiandaa kwenda kupigika kulijenga taifa
 
...asante kwa kutukumbusha kuhusu Jpili ya kwanza 2018. Na zaidi asante kwa ku(ni)tuweka katika maombi na sala zako za kila wakati. Amen
Ubarikiwe Obe ,tumuombe Mungu atusaidie tuwe na bidii ya kumtafuta

Ufalme wa Mungu utatekwa na wenye nguvu Mathayo 11:12b

Tumshukuru Mungu hata kutuweka mahali hapa pamoja ili kuunganisha nguvu

MATHAYO 18:20

Kwa maana popote pale wanapokusanyika wawili au watatu kwa jina langu ,mimi nipo hapo kati yao...

Ubarikiwe
 
TUOMBE
Mwenyezi Mungu Mtakatifu, Mfalme wa wafalme,Baba wa Milele,Mshauri wa Ajabu,Mungu mwenye Nguvu Asante kwa kutufikisha siku hii ya leo JU JUMAPILI YA KWANZA YA MWAKA ,7 JANUARI 2018 salama wako wengi walitamani kuiona siku ya leo hawajaweza sisi ni nani Baba Mtakatifu
Tunakushukuru kwa sababu Upendo wako ni mkuu kwetu, Kwa sababu unatulinda na kutuongoza, Kwa sababu unatupigania, Kwa sababu Unaweza yote,Unajua yote,Upo kila mahali. Mungu wetu tunaomba usinyamaze kila tukuitapo sisi peke yetu hatuwezi.
Tupiganie katika kila Jambo,Tufundishe,tushauri na kuturudi tunapokukosea. Mungu bariki Afya,Kazi,kusudi,Uchumi na Imani zetu.
Waponye wagonjwa wote Baba majumbani na mahospitalini,
fariji wafiwa wote wape faraja yako popote walipo,angalia wajane,wagane,
yatima Baba wape hitaji la mioyo yao,wasaidie wote wanaopitia changamoto mbalimbali.
Wasaidie wasafiri wote kokote waendako majini,nchi kavu na angani waende na kurudi salama..ponya mioyo yote inayotaabika kwa huzuni ,taabu na dhiki ,mateso tuongezee imani Baba tukuangalie wewe tu maana wewe Baba hukawii wala huwahi jibu lako ni ndiyo.Roho Mtakatifu kaa nasi siku zote za maisha yetu.
Ni katika Jina la Yesu tunaomba tukiamini na kushukuru Amina.


JUMAPILI YA KWANZA 2018 NJEMA,MUNGU AONEKANE KWETU KATIKA IBADA ZOTE SIKU NJEMA MBARIKIWE.
barikiwa pia mom
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom