Makapuku Forum

Makapuku Forum

Hahahaha yaani huwa nimemuweka kwenye mabano ila kumshukuru ni muhimu..shukuru kwa kika jambo my baby girl
68747470733a2f2f73332e616d617a6f6e6177732e636f6d2f776174747061642d6d656469612d736572766963652f53746f7279496d6167652f5f5955466e65713772524e3832413d3d2d3336303630373736362e313461336630393635386562626237633333323238303835353734332e676966
 
ZABURI 63

6.Ninapokukumbuka kitandani mwangu, Nakutafakari wewe makesha yote ya usiku

7.Maana wewe umekuwa msaada wangu ,Na uvulini mwa mbawa zako nitashangilia.

8.Nafsi yangu inakuandama sana;mkono wa kuume unanitegemeza

NAWATAKIA USIKU MWEMA DAMU YA YESU IWAFUNIKE.
 
Mtakatifu Mtakatifu Mtakatifu Bwana Mungu wa majeshi Mfalme wa Wafalme,Mungu usiyeshindwa.

Baba ni siku nyingine mpya ya Jumanne tarehe 12 Desemba 2017 Baba umetuamsha tena tukiwa ni wenye Afya njema,Amani na Furaha tunasema Asante kwa wema wako mkuu

Tunakushukuru sana Baba wa Mbinguni kwa wema wako unaotutendea siku hadi siku .

Baba wako wengi walitamani kuiona siku ya leo hawajaweza lakini sisi umetuamsha Tunakurudishia Sifa Utukufu Shukurani na Heshima Mfalme wa Amani

Baba tunakuomba Utusamehe Makosa yetu tunayotenda kwa mawazo maneno na matendo na kwa kutotimiza wajibu mbalimbali kwa nafasi tulizinazo tushike mwenendo Mpya Nasi Tunaomba utusaidie Tuwasamehe wote waliotukosea walioomba Msamaha na wasioomba msamaha
Baba walinde wote ndani ya nyuwa zetu Watoto Waume Wake Ndugu Wasaidizi wa ndani Jamaa na Marafiki zetu wajenge wakujue na wakupende wewe zaidi na zaidi

Baba Tunakuomba tuondolee dhiki taabu uchungu unafiki magomvi laumu dharau kiburi Kujikweza tujaze UPENDO wa kweli tuchukuliane mizigo kwa Upendo.

Asubuhi hii ya leo tunawaombea wagonjwa wote majumbani na mahospitalini Damu ya Yesu inene mema Baba ukawaponye gusa dawa wanazotumia gusa wanaowahudumia na wakuone wewe Mfalme wa Amani

Wabariki madaktari na manesi watoe huduma njema Baba yetu mwema

Tunakuomba Baba uwabariki na kuwalinda wamama wajawazito na wanaojifungua Mfalme wa Amani ili kazi ya uumbaji na uhai uliyoianzisha ndani ya wamama hawa ipate kibali na ikupendeze wewe wamama hawa na watoto watakaozaliwa wawe salama na wawe zao jema maana wamebeba wazo lako Baba yetu wazo hili liwe la kukupendeza Amen

Tunakuomba ubariki mipango yetu yote ya Ajira zote Ujasiriamali Biashara Kilimo Mifugo Masomo Tunakuomba ukaguse kila kazi za mikono yetu na ukaonekane Baba tukapokee kila lililo jema

Baba Waangalie kwa wema Wasafiri wote wa Majini Nchi kavu Angani ukawe dereva wa kila chombo popote waendako na warudipo Baba Damu ya Yesu iwafunike.Epusha roho zote za mauti,ajali,mauaji ,uonevu ng'oa kila pando la Shetani leta Amani katika nchi yetu zuia kila aina ya mafarakano Amani idumu Mfalme wa Amani

Mungu wetu na Baba yetu unafahamu mahitaji yetu yote kabla hata hatujatamka Baba tujaze Roho Mtakatifu ili tukutafute kwa bidii

Baba Wakumbuke Wafiwa Wajane Wagane Yatima Wenyeshida mbalimbali Wanaohitaji Watoto Wanaohitaji Wachumba Wanaotafuta kazi Wanaotafuta kuongeza vipato majumbani na makazini Wakumbuke na uwaopoe katika midomo ya Mwovu

Baba nakushukuru kwa kuwa utatenda sawasawa na mapenzi yako Amen

Tunaomba yote katika jina la Yesu Kristo Amen

DAMU YA YESU ITUFUNIKE

SIKU NJEMA MBARIKIWE
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom