Muziki: Kama Haifungui, Sio Mlango Wako
...waswahili kwa misemo tu hawajambo, hebu ukumbuke huu msemo, bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi, ha hahaha na mingine ya aina hii mingi tu. Kwa hali ilivyo tight hapa mjini unaweza kulala mlango wazi kweli! si utakuta wamesomba hadi dodoki la kuoshea vyombo maana watu tunafunga milango na madirisha lkini kila kukicha unakutana na sambusa tu kwenye nyavu! Eeh, sio sambusa za kula, ni ile mikato wadokoaji wa simu wanayotumia kudonoa simu.
Ujumbe wangu leo ni mfupi tu, kama unaingiza funguo mlangoni na haifungui basi umekosea mlango, huo sio wako. Mantiki yangu hapa ni kutokata tamaa maana unapoaribu sehemu moja ili ufanikiwe na usipofanikiwe basi jaribu sehemu nyingine pia, huna haja ya kukata tamaa na kuanza kujilaumu au kulaumu ambao kiukweli hawana msaada kwako ila maumivu. Tunaelewana, sihitaji jibu la ndiyo au hapana, hapa nimetoa maelezo tu wala si swali.
Muziki sasa, kwa sisi tunaojidai kujua kupenda, tukumbushane tu kuwa usijaribu kumfanya mtu akupende, jiamini na utakayependana naye ataanza kukupenda yeye kwanza. Hizi ni kanuni rahisi sana. Nakupenda Kapuku na unalijua hili.