Makapuku Forum

Makapuku Forum

Mtakatifu Mtakatifu Mtakatifu Bwana Mungu wa Majeshi Asante kwa Upendo wako,fadhili zako na kutuamsha tukiwa wazima na Afya njema,wapo watu wengi walitamani kuiona siku ya leo Baba hawajaweza ,tunatoa Sifa ,Shukurani,Heshima na Utukufu kwa Neema hii.

Tunakuja Mbele zako tukikukabidhi siku ya leo ya Jumamosi 9 DESEMBA 2017 ikawe njema na ya kukupendeza.
Tunaomba toba kwa yote tuliyokosea Kwa mawazo ,kwa maneno, kwa matendo na kwa kutotimiza wajibu wetu mbalimbali Uturehemu twakusihi.
Tuimarishe ili tukupende,
tukuheshimu na kuishi maisha ya kukupendeza wewe tu.
Tunaikabidhi Nchi yetu iwe na Amani.
Tunazikabidhi Familia zetu zidumishe Upendo na Mshikamano.
Tunawakabidhi wagonjwa na wenye shida mbalimbali majumbani na mahospitalini Baba ukawaponye miili na roho pia wape tumaini lako wakushike wewe tu endelea kuwaonesha ukuu wako Mfalme wa Amani.
Baba wasafiri wote majini,nchi kavu,angani ukawe nao waende na kurudi salama.Na familia zote Baba mwema zikawe salama na Amani itawale.
Watoto wetu popote walipo makazini,majumbani na mashuleni ukawasimamie wakawe vichwa si mikia wafanye mambo yote kwa ufanisi na mafanikio.Tunaendelea kuwakabidhi watoto wetu wenye mitihani ya masomo mbalimbali onekana kwao Baba,uwepo wako utawale katika mitihani yao na wawe washindi,
Baba Mungu tunazikataa kazi zote za shetani zisipate nafasi katika maisha yetu tunazivunja kazi zote hizo katika jina la Yesu Kristo tunamwaga damu ya Yesu Kristo ikatakase kila pando na kuling'oa na kulitupa kuzimu Mfalme wa Amani.
Tunakabidhi kazi zote za mikono yetu zikapate kibali mbele yako nawale wasio na kazi na shughuli za kufanya Baba wape kazi ,waliofanya usaili mahali popote takasa njia zao waweze kupata kazi Baba na maarifa ili wauone Utukufu wako,fungua milango yote ya baraka Baba mwema..kila tuingiapo na kutoka utubariki.
Baba Asante kwa Matendo yako Makuu yasiyo na mwisho,tunauona ukuu wako siku zote za maisha yetu tunasema Asante Baba na tunaomba uzidi kutuimarisha imani zetu zipande na kuwa viwango vya juu ili tuweze kushuhudia matendo yako siku hadi siku.Roho Mtakatifu tutie nguvu tuondoe hofu na mashaka tuliyo nayo.
Nakushukuru maana utatenda yote sawa na mapenzi yako
Katika jina la Yesu Kristo naomba naamini na nashukuru Amen

SIKU NJEMA WAPENDWA MBARIKIWE
 
Amina mama ubarikiwe
 
Hahahaha Obe ,mmmh huwa nakutafakari sana..Mungu akupe maisha marefu sana

...hunishindi mimi ninavyokutafakari siku zote, tunatafakariana ila bado jambo moja tu, lile ninaloliandikaga kwa maandishi madogoooooo ili wasiopenda wasione. Huwa unalisoma lakini?

Mungu atubariki na maisha marefu pamoja kama pingu za maisha (waswahili misemo yao bhana, sasa mimi na wewe tukifunga pingu za maisha ndo inamaanisha nini kwa mfano?)
 
Ubarikiwe Obe Mungu mwenyewe anajua kuingia na kutoka kwetu kiroho ina maana kubwa sana jumamosi njema
 
ITAZAME ASUBUHI YAKO LEO KATIKA JINA LA YESU KRISTO. AMEN.
Biblia Takatifu inasema kwamba:
"...Huenda kilio huja kukaa usiku, Lakini asubuhi huwa furaha." ~ Zab 30:5
USIKU unawakilisha wakati wa TABU, SHIDA, MAHANGAIKO, DHIKI, UDHIA na MATESO. Wakati huo ndipo watu wengi huvunjika moyo na kukata tamaa. Japokuwa usiku upo (upo wakati wa udhia na dhiki); lakini si lazima dhiki hiyo iambatane na kilio!
Katika andiko hili (Zaburi 30:5) kuna jambo zuri hapa la kujifunza ambalo watu wengi bado wapo gizani; Biblia imetumia neno:
"...Huenda..." neno hilo "...Huenda..." likiwa na maana ya: Labda inaweza ikawa au isiwe hivyo! Sio lazima usiku uambatane na kilio.
Katika dhiki tegemea kukutana na watu wa namna zifuatazo wanaokuvunja moyo:
1. Wenye kukulaumu kutokana na kushindwa kwako.

2. Wenye kukushutumu kuwa wewe ni chanzo au umehusika kusababisha tatizo.
3. Wenye kukucheka wakikudhihaki kutokana na kuanguka kwako; wakikwambia "kama kweli wewe ni mtumishi wa Mungu, iponye nafsi yako!"
4. Wenye kukudharau kutokana na udhaifu wako wa nje wakidhani kuwa hautasimama tena.
Tambua tu hayo ni mawazo na maneno ya wanadamu; tena hayatokani na Mungu bali yanatoka kwa Shetani. Katika wakati wa dhiki, sio lazima kilio na huzuni zitawale nafsi yako, bali unaweza kuikataa hiyo hali. Huzuni (kilio) chanzo chake ni namna jinsi ulivyoiruhusu akili yako kupokea mambo. Unaweza kuizuia huzuni na ukajaza ujasiri akilini mwako. Ujasiri unaleta faida zifuatazo:
1. Tumaini la ushindi dhidi ya tatizo lako.
2. Faraja inayoondoa uchungu wote, kwa maana Mungu aliye ndani yako ni Mkuu kuliko hiyo dhiki yako.
3. Namna ya kutafakari juu ya utatuzi wa dhiki hiyo.
Wenye huzuni (kilio) hukata tamaa, lakini wenye ujasiri hutafuta namna ya kutatua tatizo.
Katika maisha jifunze yafuatayo:
1. Usilaumu watu kwa kushindwa kwako hata kama wao ndio wamehusika kuchangia kuanguka kwako; kwa sababu lawama na kilio vitakukumbusha uchungu wako na vitakufanya ubongo wako ushindwe kutafakari namna ya kutatua dhiki yako.
2. Tambua wewe mwenyewe ndiwe mhusika wa kwanza katika kuileta furaha yako. Jifunze kujifariji mwenyewe hata kama hauna mtu wa kukufariji; ukifanya hivyo utajenga afya ya ubongo wako. Kila jambo linaanzia katika fikra! Kile unachokipanda akilini mwako ndicho kitakacholeta matokeo katika maisha yako.
3. Usijihukumu kwa makosa uliyoyatenda awali, wala usiwahukumu waliokusababisha kuanguka; bali jifunze kusamehe. Tazama mbele na utaiona siku mpya njema mbele yako (You will discover a new person today and a better today!) Samehe ila nawe upate kibali mbele za Mungu. Wasaidie hata hao waliokuudhi; kwa maana Biblia inasema:
"Lakini, Adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake.
Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema." ~ Warumi 12:20-21
4. Mungu ndiye mnenaji wa mwisho juu ya hatima yako. Mungu amekwisha kubariki wewe; Mungu amekupatia kibali; Mungu amekufanya mwana wa ufalme wa mbinguni. Hata kama unapitia magumu kiasi gani; tambua kuwa WEWE NI MBARIKIWA WA BWANA. Wewe ni mteule wa Mungu. Jitambue, tambua mamlaka uliyopewa ndani ya Kristo Yesu, na uyatumie mamlaka hayo kumwangusha na kumwaibisha Shetani.
Kwa kumalizia napenda kukukumbusha tena andiko hili:
"...Huenda kilio huja kukaa usiku, Lakini asubuhi huwa furaha." ~ Zab 30:5
Kumbuka hicho kilio HUENDA kikaja wakati wa usiku (wakati wa dhiki); sio lazima kilio kije, bali HUENDA kikaja; na kuja huko kunatokana na wewe mwenyewe kuiruhusu hiyo dhiki itawale fikra zako; lakini endapo Yesu akiitawala hiyo dhiki yako, hapo utakuwa na tumaini na utashinda zaidi ya kushinda katika Yeye atutiaye nguvu.
Jitahidi uwe sehemu ya kutatua tatizo, wala usiwe mtu wa kulalamika. Endapo ukiona mlango umefungwa, basi tambua Mungu atafungua dirisha; na ikiwa madirisha yamefungwa, basi Mungu atang'oa paa la nyumba na kukupatia njia ya kutokea; na ikiwa paa likizibwa, basi Mungu atafunja ngome zote za nyumba na kuta zote zitabomoka kama jinsi alivyofanywa wakati wa Yoshua kwenye mji wa Yeriko.
Mungu wetu ni Mkuu sana; hafungwi kwa wakati wala kwa mipaka yoyote ile. Hiyo mipaka uionayo inatokana na wewe mwenyewe kuiweka katika akili zako mwenyewe. Ukitaka ubarikiwe, hebu iondoe kwanza hiyo mipaka akilini mwako. Je, mipaka hiyo ni ipi?
1. Haijalishi madaktari wamesemaje juu ya afya yako. Pokea uponyaji katika jina la Yesu Kristo. Uwe mzima sasa.
2. Haijalishi elimu yako ni ndogo kiasi gani. Pokea ajira sasa katika jina la Yesu Kristo. Upate maarifa ya kutafuta riziki halali kwako.aibu na dhiki zote ziondoke kwako sasa.
3. Haijarishi shughuli zako zimeyumba kiasi gani. Pokea mafanikio sasa katika jina la Yesu Kristo. Kila silaha ya adui iliyoinuka dhidi yako na imwangamize yeye mwenyewe.
JITAHIDI KILA WAKATI UWE NA MAWAZO CHANYA JUU YAKO. Kile unachokipanda akilini mwako ndicho hicho icho kinaleta matokeo katika maisha yako! Panda mbegu njema akilini mwako.
Pokea uzima katika ndoa yako; pokea uzima katika afya yako; pokea uzima katika maisha yako. Pokea baraka na mafanikio maishani mwako. Yote hayo yatimie katika jina la Yesu Kristo. Amen.
ITAZAME ASUBUHI YAKO LEO KATIKA JINA LA YESU KRISTO. AMEN
 
...hunishindi mimi ninavyokutafakari siku zote, tunatafakariana ila bado jambo moja tu, lile ninaloliandikaga kwa maandishi madogoooooo ili wasiopenda wasione. Huwa unalisoma lakini?

Mungu atubariki na maisha marefu pamoja kama pingu za maisha (waswahili misemo yao bhana, sasa mimi na wewe tukifunga pingu za maisha ndo inamaanisha nini kwa mfano?)
......
 
Na huku tulipo tunasumbuliwa sana na hawa jamaa
cfa8e21a5ff28a941bcc051e07c97884.jpg
na hawa
725c08a36c6d90eeb754358f1874c389.jpg
mkuu imekuwa kero kwa kweli, lakini hakuna jinsi inatulazimu kuyazoea mazingira
Mie bora mjomba simba nishamzoea, hata msimbazi yupo, ila nyoka hapana, nikimuona hata kwa tv amani yote inapotea, ninabaki na risasi, uwazi na ijumaa..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom