Muziki: Wasiliana Ufanikiwe
...kesho ni Ijumaa kama ulikuwa hujui na sio mbaya ukisema asante kwa kukumbusha kuhusiku siku hii nzuri kabisa. Na ujue siku za mwezi wa 12 zina nyodo sana, huwa zinajidai kutembea haraka haraka kama unawahi muda wa kulipa deni. Ninakufurahia sana wewe kapuku unayekuwa hapa na kulifanya jukwaa hili kuwa la kipekee. Asante,
shululu ,
Tumosa ,
makaveli10 ,
Shunie ,
Lyon Lee , Mimi,
BlessedHope ,
husna muba mpenzi wangu mwenyewe,
moneytalk hoping the papers are over and ready to work yur butt off during the break,
SHIMBA YA BUYENZE ,
Tetramelyz ,
Mndali ndanyelakakomu ,
koncho77 ,
Transcend ,
Sakayo ,
Nyagei ,
Mtu wa Green ,
dumejeuri ,
mzeewakungoa ,
Gentries ,
Werrason ,
Mussolin5 ,
ABJ ,
moudgulf na wewe Kapuku unayekuwa hapa na unasoma kipengele hiki sasa.
Mawasiliano ni muhimu katika kufanikisha haja zetu za kimaisha na kimwili, ndo maana sijui bila mawasiliano tungeweza kufahamiana vipi na wewe kapuku mheshimika, tungeweza kupata michongo yetu ya kifedha kinamna gani bila mawasiliano na zaidi ingewezekana vipi bila mawasiliano kutongozana kukawa rahisi na kukataliwa kukawa rahisi zaidi. usikae kimya, fanya mawasiliano iwe ni kwenye kutafuta kazi, mchumba, mtaji, masomo na marafiki au tumia mbinu za anko wangu ambaye yeye mawasiliano yanakuwa rahisi pale anapohakikisha kutongoza kumerahisishwa kwa uwepo wa sheria mpya kule Kenya inayoruhusu mume kuoa mke mwingine bila ruhusa ya mke, anko wangu anahamia Kenya, fyi.
Muziki sasa, nimesikiza huu muziki hapa nikakumbuka zamani, si mnajua mimi ni mhenga, mkongwe ila sio babu wala mzee sana. Enzi za muzki wa raggamuffin, siku hizo nilikuwa nayrudi mareggaemuffin na nikatengeneza jina nikishindanishwa na watu wa bongo kina Digadiga. Muziki wenyewe ni wa Chaka Demus na Pliers Bam bam, ila huu sasa ni mpya hawajui hata kucheza