[emoji524] Pole na majukumu ya leo unapojiandaa kupumzika tafadhali imba wimbo huu kwa kuutafakari*
1. Kaa nami, ni usiku tena;
Usiniache gizani, Bwana;
Msaada wako haukomi;
Nili peke yangu, kaa
nami
2. Siku zetu hazikawii
kwisha,
Sioni la kunifurahisha;
Hakuna ambacho
hakikomi,
Usiye na mwisho kaa
nami.
3. Nina haja nawe kila saa;
Sina mwingine wa
kunifaa;
Mimi nitaongozwa na
nani
Ila Wewe?
Bwana kaa nami.
4. Sichi neno uwapo karibu;
Nipatalo lote, si taabu,
Kifo na kaburi haviumi,
Nitashinda kwako, kaa
nami.
5. Nilalapo nikuone wewe,
Gizani mwote nimulikiwe,
Nuru za mbinguni
Hazikomi,
Siku zote kaa nami.
*Usiku mwema*NAWAPENDA SANA[emoji7] [emoji7]