Makapuku Forum

Makapuku Forum

EUFA SUPER CUP
8a8eea88504d10844c4f0cc6b19e0159.jpg
a70100cc8a243d309d08c401fd99ab31.jpg
.......Achana na penati ya Morata na ile ambayo sijui kipa wa chelsea alijua anaanza mpira ....anyway yalitokea na ufunguzi huo tayari ijmaa kinanuka ...sema sio dili wala kesi ila utamu ni leo....dadeeekii ebhu twende wote japo mda wako ntautumia kama wewe hutoutumia .....Marcelo na Dani Carvajal hawa ndio watu hatari sana katika kutengeneza nafasi za magoli kwa safu ya ushambuliaji ya Real Madrid...... Ubora wao sio tu Zidane anaukubali hata Mourinho anauheshimu. Pamoja na kuwa bora sana katika kuifaidisha safu ya ushambuliaji kwa mipira yao ya mwisho Bado pia wamekuwa wakiitia dosari eneo lao la ulinzi wanapokutana na timu zinazotumia mashambulizi ya kushtukiza.

Kwa bahati mbaya kwa Mourinho na bahati nzuri kwa Zinedine Zidane ni kuwa kuelekea mchezo huu, Jose Mourinho anawakosa mabeki wake watatu bora kabisa Marcos Rojo, Phil Jones na Erick Bailly. Hii inatengeneza mapungufu kiasi katika safu ile ya ulinzi ya Manchester united mbele ya safu ile ya ushambuliaji ya Real Madrid..... Kriss Smaling, Daley Blind, Victor Lindelof na Alex Tuanzebe ndio mabeki wa kati wenye uwezekano mkubwa wa kucheza katika mchezo huu.

kapuku usinichoke .......ili uweze kumzibiti Christian Ronaldo basi ni lazima Valencia na Damian wafanye kazi kuwazuia sana na kuwashambulia sana Marcelo na Dani Carvajal.... Njia pekee ya kuwakaba hawa mabeki bora kabisa wa pembeni wa Real Madrid ni kuwashambulia, Marcus Rashford, Anthony Martial, Jesse lingard, Juan Mata na Henrikh Mkhitaryan kama viungo wa pembeni watatakiwa kuwafanya Marcelo na Dani Carvajal wasipandandishe mashambulizi na kama wakipandisha basi yasiwe mara kwa mara.

Jiandae kulipia kinywaji kwaajili ya vita ya eneo la kiungo..... Toni Kroosi, Paul Pogba, lucar Mondric, Nemanja Matic, Casemiro na Andre Herrera. Hapa ndipo zilipo roho za difensive na offensive katika mchezo huu.
Baada ya ujio wa Nemanja Matic katika kiungo cha Manchester united.... Viungo wa Real Madrid wanapaswa kuwa makini sana na Paul Pogba katika eneo la juu nyuma ya Romero Lukaku. Mara zote mpira unapokuwa mguuni kwake huwa na hatari sana, hii kutokana na aina ya uchezaji wake, kuna wakati anaamua kupiga, kuna wakati anaamua kutengeneza nafasi za magoli.
Achana na Dani cellobas na Matteo Covacic alafu Fellain na Andre Pereira hawa ni wa baadae.

Mpira unapokuwa mguuni mwa eidha Mata, Mkhitaryan, martial, Rashford au Lingard.. Ramos, Nacho na Verane wanapaswa kuwa makini sana na movement za Romero Lukaku, huyu jamaa ni mzuri sana kwenye kujitengenezea nafasi wakati timu inakuja nyuma na mpira. Kama ilivyo kwa Karimu Benzema, Marco Asensio, Isco na Gareth Bale... Wamekuwa wazuri sana wanapopata nafasi huzitumia vizuri pindi mabeki tension yao inakuwa kwa Christian Ronaldo.

Kama Zinedine Zidane ataamua kumtumia Bale katika mchezo huu basi Madrid watakuwa na nguvu sana pembeni mwa uwanja, ila kama ataamua kumtumia Isco, Manchester united watapata usumbufu sana katikati ya uwanja..... Ila kama Mourinho ataamua kumtumia eidha Fellain au Matic kama destroyer basi kuna unafuu mkubwa kwa watu hawa kupunguza pressure ya mipira ya juu kutokana na size zao katika maeneo yote mipira itakapokuwa inapigwa juu.

Mchezo huu unaweza usiwe na ubora ule watu Wengi wanaoutegemea kutokana na hali ya joto katika nchi ya Macedonia katika mji wa Skopje kuwa na joto Kali linalokadiriwa kufika mpaka nyuzi joto 40 japo kwa jana ilikuwa ni nyuzi joto 38. Kama timu hazija training katika mazingira kama hayo basi wanaweza kucheza chini ya ubora ule wa kila siku.

Zinedine Zidane changa karata zako na Jose Mourinho panga kete zako... Tuikaribishe UEFA champions league....japo wenzangu na mimi pambana na hali yenu kama watoto wenu wataililia futuhi walaze mapema ili muenjoy mpira wenu .....
 
TOP TEN
Wakati kukiwa na ngonjera pamoja na kiki za kibwege za kutuzuga eti hataki kutawala zaidi ya miaka 10 kila siku wakati ni maigizo tu na kila mtu anajua Urais mwisho ni vipindi viwili sasa mbwembwe za nini sijui?
Wakenya wapo kwenye uchaguzi na ninavyowajua hawapendagi ujinga wale wanaweza kumweka mtu kando ila sijui kzma wameamua
Huko Rwanda bwana mkubwa keshageuka Rais wa maisha wakati aliyejiita hivyo (Omar Bongo} alishajifia na kuzikwa na utawala wake kuishia hapo

Sasa tuangalie marais wa Marekani waliotawala kipindi kifupi
Karibuni
.....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom