TUKIO HALISI LA WIZI LILILOISHANGAZA DUNIA
sehemu ya 01:
Ilikua tarehe 24/11/1971, ktk uwanja Wa ndege Wa kimataifa Wa mji wa Portland. Jamaa mmoja alievalia suti nyeusi na koti lefu jeusi kw juu akiwa amebeba brief case nyeusi, alifika ktk counter ya KAMPUNI ya ndege ya NORTHWEST Orient Airliner na akatoa fedha dola 20 kununua tiketi ya ndege fight 305 kwenda mjini Seattle.
Safari hiyo ilikua inachukua dakika 30 tuu mpaka kufika. Jamaa huyu alijitambulisha Dan Cooper.
Baada ya kuingia akakaa kwnye siti namba 18E na baadae 15D, ilipofika mida ya SAA 8:50 mchana ndege iliruka na Mr cooper akawasha sigara na kuagiza soda.
Siti ambayo alikaa huyu kiumbe ilikua siti ya nyuma kabisaa na alikaa karibu kabisa na siti ya muhudumu Wa kike Wa ndege aliejulikana kw jina la FLORENCE SCHAFFENER.
Baada ya dakika chache cooper alitoa kikaratasi mfukoni kilichochapwa kw unadhifu mkubwa na maandishi yakiwa yameandikwa kw herufi kubwa tuu. Alimpatia yule binti kile kikaratasi.
Yule muhudumu Bi Schaffner baada ya kukipokea kile kikaratasi hakukitilia maanani maana alishawazoea abilia wengi Wa kiume kuwatongoza au kuwapa namba za simu kw lengo la kuwataka hapo baadae. (Mambo ya tamaa)
Yule muhudumu akachukulia poa na kuendelea na mambo yake lkn kile kikaratasi akiwa anacho kwenye mkoba.
Cooper baada ya kuona hivyo aliinama na kumnong'oneza " Miss you would better take a look at that note. I have a Bomb "
Maana yake alimwambia ("Bibie ni vema ungekisoma hicho kikaratasi Nina bomu."
Baada ya kueleza hivyo kimya kimya akaanza kumuamuru muhudumu Huyo akae karibu nae.
Alianza kumpa maagizo na kumtia hofu na jambajamba alitaka kumuhakikishia Kua alichokiandika ni kweli.
Alichukua briefcase yake na akaifungua kidogo tu ili muhudumu aangalie, alipoangalia kweli aliona cylinders 8, NNE zikiwa chini na NNE zikiwa juu na zote zikiwa zimeunganishwa kw nyaya nyekundu ambazo nazo zilienda kuunganika kwny Betri yenye rangi nyekundu.
Muhudumu baada ya kujionea kw macho aliamini bwana Cooper anabom. kumbuka wote walikua ndani ya ndege na ilikua inaelea mawinguni mwendo mdundo.
Cooper ambae ndie stelingi wa hadithi yetu ya leo alianza kumpa tena maagizo yule muhudumu akaongee na marubani kw kupitia intercom kuwa akaamuru wawasiliane na uwanja wa ndege wa Settle na waelezwe juu ya ndege kutekwa na yupo tayari kulipua ndege na abiria wote waende na maji na yeye akiwemo.
Hapo ikawa utata maana ndani ya ndege kulikua na marubani tegemewa wawili na injinia wa ndege nae alikua anasafili siku hiyo. jamaa hili sijui liliotea vp maana kumpoteza injinia na marubani Wa ndege tena wenyeujuzi na wawili haikua swala la mchezomchezo.
Je wajua ilikuaje?.
Usikose kujua kilichojili, hapa ndo utajua watu wanavipaji vya kuiba. akili nyingi nguvu kisoda.