Makapuku Forum

Makapuku Forum

Bi Grace Mugabe amemtaka mumewe Rais Mugabe wa Zimbabwe kumtangaza mrithi wake ili kupunguza migawanyiko kuhusu atakayemrithi. Soma zaidi: Bi Mugabe amtaka mumewe kumtangaza mrithi wake Zimbabwe - BBC Swahili
9417312587c7926cc934b5e70d21ff4b.jpg
 
Kwa mujibu wa GPL Lucy Komba anajivunia mwanae kujua kiingereza vizuri ndani ya muda mfupi na kusahau Kiswahili, Aidha Lucy amefurahi mwanae anapata elimu nzuri nchini Denmark na kuachana na tabia za kiswazi toka Bongo...

"Kitambo nawaza malezi bora kwa mwanangu, sikupenda awe na tabia za Kibongo japo ni Mbongo, hivi sasa siyo yeye kabisa ameshasahau Kiswahili siku nyingi maana mtoto ananasa kirahisi, nimefurahi mno" alinukuliwa star huyo aliyesaidia wasanii chipukizi wengi
1a0858203014e36f353623e4a42af5f2.jpg
YAANI UNAFURAHIA MWANAO KUTOJUA LUGHA YAKO??!!!!!!




anyway kila MTU apambane na hali yake
 
HII NDIYO HISTORIA HALISI YA MANENO "SHIKAMOO" NA "MARAHABA."
kuna idadi kubwa ya watu wanatumia neno shikamoo kama sehemu ya kuonyesha heshima au salamu kwa mtu aliyekuzidi umri.
Ila ni muhimu sana tukaelewa maana na historia ya na maneno “Shikamioo” na “Marahaba”. Kama ifahamikavyo kuwa kila jambo huwa na mwanzo na mwanzo huwa na sababu za kufanya hilo jambo kuibuka. Ni hivi kabla ya miaka ya 600 BK au BM, Wabantu walikuwa wameshafika Pwani ya Afrika mashariki. Na ukweli ni kwamba Wabantu walishapata kuishi hapo na hata wageni waliofika walikiri suala hilo. Na kwa kuwa Wabantu walipata kuishi hapo walikuwa na mitindo yao wa maisha na walikuwa wakiheshimiana.
Kikubwa zaidi Wabantu walikuwa na salamu zao. Kwa mfano Wazaramo (historia yao itaandikwa) walikuwa na salamu yao kama ifuatavyo, aliyekuwa akiamkia alionyoosha mikono mbele na kusema “simbamwenee” na kisha anayeamkia huitikia “utwaaa”. Na kila mtu alikuwa akifurahia salamu hiyo, iliyokuwa nzuri kuitamka mdomoni.
Lakini mambo yalibadilika pale walipokuja Waarabu na kuanzisha biashara ya utumwa. Na hapo tukapata makundi mawili yaani “mtumwa” na “bwana” na mtumwa alipaswa kumuamkia Bwana kwa neno la “Nashika Miuu” akiwa na maana ya “Nashika Miguu”. Na kila mtumwa alipaswa kujua na kutambua salamu hii.
Na mtumwa alipaswa kutoa salamu hii hata mara 100 kwa siku moja. Lengo la salamu hii ilikuwa ni kutenganisha kati ya mtumwa na bwana wake.
Kuanzia miaka ya 600-1700, salamu hii ilikuwa ikitumika maeneo ya Pwani tu. Na kuanzia miaka ya 1700 mwishoni na 1800 mwanzoni Waarabu walianza kuingia maeneo ya ndani ya Afrika mashariki. Na kila walipofika salamu hii waliitumia na baadhi ya machifu waliipenda sana salamu hii. Na kujikuta wakiwa na matamshi tofauti juu ya salamu hiyo. Na kwa wakati wote huo ilikuwa ni salamu ilikuwa ni "Nashika Miuu" na sio "Shikamoo" kama ilivyo sasa.
Kutokana na watu tofauti kutumia salamu hii, wapo waliotamka "Shikamuu" kama neno moja. Na mpaka miaka ya 1930, kipindi ambacho Kiswahili kinafanyiwa usanifishaji ndipo tukapata neno "shikamoo."
Na kuhusu neno "Marahaba", lina maana ya "asante". Na neno hili huitikiwa na Yule anaeamkiwa (Bwana) ambaye miguu yake imeshikwa na mtumwa. Na mpaka sasa salamu hii inatumiwa sana na Watanzania wengi licha ya kuwa na salamu zao za kikabila.
Hii ndio historia fupi ya neno "Shikamoo" na "Marahaba".
- Shukrani za pakee ziwafikie "Historia ya Afrika" .
- Kambi Kuu kwa ihsani ya Habari Forums.
Asante sana mpendwa wa binamu
 
Kwa mujibu wa GPL Lucy Komba anajivunia mwanae kujua kiingereza vizuri ndani ya muda mfupi na kusahau Kiswahili, Aidha Lucy amefurahi mwanae anapata elimu nzuri nchini Denmark na kuachana na tabia za kiswazi toka Bongo...

"Kitambo nawaza malezi bora kwa mwanangu, sikupenda awe na tabia za Kibongo japo ni Mbongo, hivi sasa siyo yeye kabisa ameshasahau Kiswahili siku nyingi maana mtoto ananasa kirahisi, nimefurahi mno" alinukuliwa star huyo aliyesaidia wasanii chipukizi wengi
1a0858203014e36f353623e4a42af5f2.jpg
YAANI UNAFURAHIA MWANAO KUTOJUA LUGHA YAKO??!!!!!!




anyway kila MTU apambane na hali yake
Mtoto wake kakua
 
STAAJABIKA NA KIM JONG-UN (ALMAARUFU KWA JINA LA KIDUKU) RAIS WA KOREA KASKAZINI.

Kim Jong- un ni mtoto wa tano na wa mwisho katika uzao wa Kim jog-il (raisi wa pili wa Korea Kaskazini).

Kwa sasa ndiye kiongozi wa nchi hiyo na alichukua cheo hicho baada ya kifo cha baba yake Dec 19, 2011.

Kim jong-un anatajwa kuwa mmoja wa viongozi wenye msimamo mkali hasa kwa nchi za kimagharibi na hadi sasa ameimarisha nguvu za kinyuklia za korea kaskazini na anainyima usingizi Marekani.

[HASHTAG]#Hebu[/HASHTAG] sasa tuyajue machache yafuatayo
kumuhusu Kim jong-un:

1. Ni general pekee duniani aliyepata cheo hicho bila uzoefu wa kijeshi. Kipaji, akili na kujituma ndo vilimfanya kuwa general licha ya kutokuwa na mafunzo wala uzoefu wowote wa masuala ya kijeshi. Labda ni kwa sababu Kim ni shupavu na jasiri wa kuzaliwa na sio wa kujifunza. Na anapenda zana za kinyuklia kuliko zana nyingne za kijeshi.

2. Pamoja na kuwa kiongozi na mkuu wa nchi, Kim hakusoma shule yoyote nchini Korea kaskazini. Alipelekwa kwa siri nchini
Swirtzerland akiwa mdogo na alisoma Bern
international school ya nchini humo. Mkuu wa shule alimtambulisha darasa la sita A kama Park un na kwamba alikuwa mtoto wa mwanadiplomasia wa korea kaskazini (kwa sababu za kiusalama). Somo alilofaulu vizuri ni mziki lakini alifeli hesabu na sayansi.

3. Anaweza kuwa ndo kiongozi mkubwa wa nchi na mwenye umri mdogo zaidi dunian japo haifahamiki ni lini hasa Kim jong-un alizaliwa. Wapo wanaodai alizaliwa mwaka 1982, wengine 1983, na taarifa nyingne zinasema alizaliwa mwaka 1984.

4. Baba yake, aitwae "KIM Jong-IL" alizaliwa kimiujiza. Taarifa nchini korea kaskazin zinasema Kim jong-il alizaliwa mlima Baekdu, Huu ni mlima wa imani na huabudiwa na wakorea kaskazin.
Wakati, saa na siku aliyozaliwa, nyota mpya ilitokea na kufunika mbingu, ghafla majira yalibadilka kutoka winter kwenda spring na pinde mbili za mvua zilionekana. Japo taarifa kutoka katika kumbukumbu za kisoviet zinasema alizaliwa 1941 katika kijiji cha Vyatskoye huko nchini siberia. Huyu ni baba wa kim jong-un.

5. Alikuwa na uwezo wa kubadili
majira na hali ya hewa, hii ni kwa sababu inadaiwa alikuwa mtu wa miujiza.

6. Akiwa na miaka 27 Kim jong-un alifanyiwa plastic surgery ili kuwa na mwonekano sawa na babu yake Kim II sung. Hii ni kwa sababu Wakorea
kaskazin wengi hawamiliki vyombo vya habari na hivyo wengi hawakuwahi kumuona ila siku walipomuona walimfananisha na hayati kim II
sung na kwa hilo wakatokea kumpenda sana kwakuwa alifanana na babu yake ambaye ndo baba wa taifa wa korea kaskazin na kwao huyu ni Mungu wao na wanaamini yupo nao hadi leo Katika maisha yake ya nje ya uhai.

7. Mwaka 2012, wachina walidai Kim jong-un ni "Sexiest man alive" na kwamba jamaa ni ndoto ya kila mwanamke hapa duniani. Hii ni kutokana na mwonekano wake, ushupavu,, ukarimu, kujiamini pamoja na mvuto wa sura yake ya mviringo.

8. Baba yake alipofariki mwaka 2011 alihakikisha msiba wake unaombolezwa na wakorea kaskazini wote. Ambao hawakujua namna ya kulia, alihakikisha wanayatoa machozi. Ambao hawakushiriki kwa namna moja ama nyingne katika shughuli muhimu za msiba huo
yakiwemo mazishi walihukumiwa kufanya kazi ngumu miezi sita.

9. Alimuhukumu kifo kamanda msaidizi wa jeshi la wananchi kwa kosa la kuhudhuria msiba wa baba yake akiwa amelewa. Amri aliyoitoa ni kwamba " anyongwe na usibaki hata unywele wake".

10. Kim jong-un pia alitoa hukumu ya kifo kwa mjomba wake kwa kile kinachodaiwa kuwa kosa la ubadhilifu wa mali ya umma na harakati za kupindua nchi. Huyu alivuliwa nguo na kutupwa katika banda la mbwa wakali waliomzika katika matumbo yao.

11. Mmoja kati ya marafiki wakuba wa kim jong-un ni nyota wa zaman wa NBA Michael Jordan. Akiwa mwanafunzi, kim alitumia muda wake mwingi kuchora picha za Michael Jordan.

Huyo ndo KIM JONG-UN Rais anayewanyima amani korea kusini na mshirika wake Marekani
na anadai yupo tayari kwa lolote dhidi ya
marekani hasa kwa nguvu za kinyuklia.
Anaendeleza kile walichokiamini babu na baba yake kuwa Marekan ndo adui mkubwa wa Korea kaskazini.

Habari Forums.
55d8e61f0ff52ec72197b2e02ff4e3a9.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom