
Nikasema moyoni mwangu, Mungu atawahukumu wenye haki na wasio na haki kwa kuwa kuna wakati huko kwa kila kusudi na kwa kila kazi
Nikasema moyoni ni kwa sababu ya wanadamu ili Mungu awajaribu nao waone ya kuwa wao wenyewe wafanana na wanyama
Kwa maana linalowatukia wanadamu linawatukia wanyama jambo moja lawatukia anavyokufa huyu ndivyo anavyokufa huyu naam wote wanayo pumzi moja wala mwanadamu hana kitu cha kumpita mnyama kwa maana yote ni ubatili
Wote huendea mahali pamoja wote hutoka katika mavumbi na hata mavumbini hurudi tena
MUHUBIRI 3:17:20
Niwatakie usiku mwema mlindwe na damu ya Yesu