Pia....

Waziri Mkuu wa Iraq, Haider al-Abadi, ametahadharisha kwamba kuna changamoto nyingi, licha ya ushindi katika mapambano ya kuurudisha mji wa Mosul kutoka katika himaya ya wapiganaji wa Kiislamu.

Leo mkutano wa dunia kuhusu uzazi wa mpango unafanyika huko jijini London nchini Uingereza, ili kujadili jinsi ya kuboresha huduma za uzazi wa mpango duniani

Tume ya uchaguzi nchini Kenya yafikisha mahakamani suala la tata la utolewaji zabuni ya karatasi za kupigia kura

Rwanda imejaliwa vipaji vya muziki lakini muziki huo umeshindwa kuvuka mipaka ya nchi hiyo changamoto ikiwa ni lugha itumikayo

Tanzania ina azma ya kuelekea katika uchumi wa viwanda ikiwa ni ajenda kubwa ya serikali ya awamu ya tano.

Uganda imepeleka kikosi cha waniriadha 13 kwenye mashindano ya dunia IAAF vijana waliochini ya umri wa miaka 18.Timu hiyo imekuwa kambini kwa zaidi ya miezi miwili huku ikikabiliwa na changamoto kadhaa

Swala la usalama limeiponza Kenya, mwenyeji wa makala ya 10 na ya mwisho ya dunia ya mbio za vijana wasiozidi umri wa miaka kumi na nane yatakayoanza kesho mjini Nairobi Kenya. Mabingwa watetezi Marekani waliongoza mataifa mengine 5 kujiondoa huku wakihofia usalama wa wanariadha wao mjini Nairobi.