
BABA MUNGU wa mbinguni asante kutuamsha salama tutakase ,tuongoze,tufundishe Ee Roho Mtakatifu siku ya leo ibarikiwe,tunakuomba tuepushe na mabaya yote tuepushe na dhambi za aina yoyote kwa kunena ,kutenda hata kutotimiza wajibu..tunaomba tuwe wanyenyekevu miongoni mwetu na mbele yako kila mtu akamhesabu mwenzake kuwa ni bora na muhimu katika safari hii ya Kurudi kwako BABA,Safari ambayo inahitaji mshikamano na kutiana moyo,safari ambayo inahitaji nguvu ya Roho Mtakatifu ili tusirudi nyuma katika kumtumikia Mungu wetu.
BABA tunaomba ponya wagonjwa,fariji wafiwa ,wajane na yatima watie moyo waliopondeka na kukata tamaa wale waliorudi nyuma wainuke tena na wafahamu bado unatupenda na unatusamehe na kutufutia makosa yetu kila iitwapo leo.
Wabariki watoto wetu majumbani na mashuleni wawe na hofu ya MUNGU na kuishi maisha ya kumpendeza Mungu.waimarishe katika masomo yao wawe vichwa na si mikia.
Ponya ndoa,ponya mahusiano,ponya familia na imarisha upendo kati yetu MAKAPUKU
Tuimarishe katika kazi zetu na mipango yetu ikafanikiwe BABA kila mmoja wetu akafaidi matunda ya kazi za mikono yake.
Asante Baba kwakuwa unatupenda na utatenda sawa na mapenzi yako.
Katika jina la Yesu naomba na kushukuru
Amen,Asante.
NAWATAKIA SIKU NJEMA YENYE BARAKA
Sent from my TECNO H6 using JamiiForums mobile app