Wakuu ...kitendo cha North Korea kurusha jana ICBM jana nimejikuta najiuliza maswali mengi kama hamtojali sio mbaya tukashare make nilimejitahidi kufukunyua source mbalimbali kuhusu hili jeshi la bwana mapankii ...weka kando stori za sani na kiu ...
Inaaminika kuwa hii nchi ina wanajeshi wengi tena jeshi lake lokiwa miongoni mwa majeshi yaliyo active dunianii ..

Korea kaskazini inaaminika kumiliki zaidi ya silaha 1000 zenye uwezo tofauti ikiwemo kombora la maasafa marefu ambalo linaweza kuishambulia Marekani.
Mpango wa Pyongyang umeendelea katika miongo kadhaa ya hivi karibuni kutoka mizinga mikubwa katika miaka ya tisini na sabini hadi makombora ya masafa mafupi mbali na yale ya masafa marefu katika miaka 80 na 90.
Hivi karibuni, Korea Kaskazini ilitangaza kwamba inaunda makombora ya masafa marefu yanayoweza kurushwa kutoka bara moja hadi jingine ambayo yanaweza kushambulia mataifa ya magharibi....jana wakarusha ICBM sio jambo la kitoto
Taifa la Korea Kaskazini linaaminika kutengeza kombora la masafa marefu zaidi ambalo wachunguzi wamelitaja kuwa KN-08 ama Hwasong mpaka 10-13....hivi vifaa sio vya mchezo kwenye masuala ya kijeshi mfano tu Hwasong 10 lililojaribiwa june 22 2016 ni kitu hatari sana...hii ni Ballistic missile yenye urefu mpaka 12m ... lakini sasa washafikia mpka H13 ...
Inasadikika robo tatu ya bajeti inahudumia jeshii yaani ata kama kuna majanga kiasi gani jeshi lazima lihudumiwe haswa ...
Songum ambayo ndo sera yao kuu jeshi ndo namba moja kwao ..ata bajeti inaenda takribani 15.8% mpaka 38%...

kama huku kwetu Tanzania vijana wengi wanapita jkt kujifunza uzalendo na wao hii system wanayo na 1.5m -6 watu wanakuwa trained na wapo tayari kuingia front kikinukaa ...
Inasadikika kila mwanaume korea ni mwanajeshi kule make wanapitia mafunzo ya kijeshi kwa kijikimu ..jambo jemaaa

hata kama kuna wachunga mbuzi kama Bitoz lakini mguse huoneeee dadeeekiiii....
Hawa jamaa wako vizuri haswa hata zile Banned lasers ambazo kufikia miaka ya 2010 zilikuwa zinapingwa lakini jamaa wamekomaa nazo ...
Achilia mbali hilo hata Multiple Cyber Warfare wako vizurii ...wana uwezo wa kuhack kumbuka walichomfanyia sony 2014...
Sio vidume tuu hata wanawake wako vizuri ...kazi kaziii hawarembiii make kwetu inajulikana wanawake wanaoingia jeshini tunawachukulia kama watu wa ajabu ila kwao kawaida tuu....yeeeeeeaaaaaaaah chekiii sura za kaziiiii
....ukiachilia mbalii hivyo vyote ata chemica weapons wapo

...matumizi ya Chlorine , phosgene na zile mustard gas hawapo nyumaaa ...
Vijana wadogo wadogo nao wanapata mafunzo
Twende wotee... Idara ya ulinzi nchini Marekani Pentagon inaamini kwamba Korea Kaskazini inamiliki makombora 6 aina ya KN-08, ambalo lina uwezo wa kufika hadi Marekani. Korea kaskazini inaaminika kutengeza toleo jipya la kombora hilo linalojulikana kama K14
Mnamo mwezi Januari 2017, kulikuwa na ishara ya jaribio, muda mfupi baada ya kiongozi Kim Jong un kudai kwamba taifa hilo lilikuwa katika awamu ya mwisho ya kutengeza kombora la masafa marefu linaloweza kurushwa kutoka bara moja hadi jingine.
Mpango wa kisasa wa kutengeza makombora yaa Korea Kasakzini ulianza kwa kutengeza makombora ya scud ambapo yalipitia Misri mwaka 1976. Kufikia 1984, taifa hilo lilikuwa likitengeza makombora yake kwa jina Hwasong.

Inaaminika kuwa na makombora tofauti tofauti ya masafa mafupi ambayo yanaweza kulenga taifa jirani la Korea Kusini .Uhusiano kati ya mataifa hayo mawili ya Korea umeharibika na yamekuwa yakijiandaa kukabiliana kivita.
Kombora la Hwasong 5 na Hwasong 6 ambayo pia hujulikana kama Scud B na Scud C yana uwezo wa kwenda kilomita 300 na 500 mtawalia kulingana na kituo cha Marekani kinachofanya utafiti wa kuzuia kuenea kwa nuklia.Makombora hayo yanaweza kubeba makombora ya kemikali na nyuklia....picha chini ni scud b na scud c
Scud c
....missile zao zipo katika hii range
Shukrani wadau