Makapuku Forum

Makapuku Forum

MATHAYO 5

38.Mmesikia imenenwa jicho kwa jicho,na jino kwa jino.

39.Lakini mimi nawaambia,Msishindane na mtu mwovu,lakini mtu akupigaye shavu la kuume,mgeuzie na la pili.

40.Na mtu atakaye kukushitaki kuitwaa kanzu yako,mwachie na joho pia.

41.Na mtu atakayekulazimisha mwendo wa maili moja,nenda naye mbili.

42.Akuombaye mpe,naye atakayekukopa kwako usimpe kisogo.

43.Mmesikia imenenwa kwamba mpende jirani yako,na umchukie adui yako.

44.Lakini mimi nawaambia ,Wapendeni adui zenu,waombeeni wanaowaudhi.

45.Ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliyembinguni,maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema,huwanyeshea mvua wenye haki na wasio na haki.

46.Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani?hata watoza ushuru ,je!nao hawafanyi yayo hayo?

47.Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu,mnatenda tendo gani la ziada?Hata watu wa mataifa je!Nao hawafanyi kama hayo?

48.Basi ninyi mtakuwa wakamilifu ,kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.


BABA SIKIA KUOMBA KWETU,TUNAJUA UNAFAHAMU HAJA ZA MIOYO YETU HATA KABLA HATUJATAMKA..TWAKUOMBA UTUSIKIE..NAWATAKIA USIKU MWEMA MALAIKA WALINZI WATUZINGIRE,DAMU YA YESU ITUFUNIKE MBARIKIWE
Amen
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom