Makapuku Forum

Makapuku Forum

Mbona wamejaa tele
Sema gia zao zinatofautiana
Kuna waganga feki
Madokta feki
Mafundi feki
Wafanyabiashara feki
Madadapoa,
Makakapoa n.k

Kila mtu yupo JF kwa lengo lake...wengine kutafuta pesa kwa halali,wengine umaarufu,wengine likes,wengine kutapeli,wengine kutafuta marafiki,wengine kutafuta wapenzi,wengine kutafuta maarifa,wengine kubadilishana mawazo,wengine kutukana watu,wengine wanatumikia wanasiasa
Wengine wapowapo tu hawana malengo yoyote
JF ni kichaka
.......
Duuuuuh kaz kwelikweliii
 
5fbffeae27dc136ff7d6ed419d647c59.jpg
 
Tuendelee na TETESI ZA USAJILI


Arsenal wanakaribia kutangaza usajili wa winga kutoka Algeria, Riyad Mahrez, 26 ambaye anaichezea Leicester City (Calciomercato).

Arsenal huenda wakakamilisha usajili wa Alexandre Lacazette, 26, katika saa 48 zijazo kwa mujibu wa rais wa Lyon Jena-Michel Auylas (Le Progress).

Paris Saint Germain wamemuulizia kiungo wa Liverpool Philippe Coutinho, 25, huku Liverpool wakisema mchezaji huyo kutoka Brazil ana thamani ya pauni milioni 87 (Daily Mirror).


Chelsea wana matumaini wataweza kufanikisha mpango wa kumsajili beki wa kushoto kutoka Brazil, Alex Sandro, 26, huku mazungumzo na Juventus yakitarajiwa kufanyika Jumatatu (Daily Telegraph).

Antonio Conte anakabiliwa na ushindani kutoka Manchester City katika kutaka kumsajili beki wa kati wa Roma Antonio Rudiger, 24. Barcelona pia wanataka kumsajili Leonardo Bonucci, 30, ambaye Chelsea wanamtaka, na Juventus wamempa mkataba mpya Sandro ili kumshawishi asiondoke (Daily Mirror).

Jurgen Klopp ameiambia Liverpool kuongeza bidii katika kumsajili kiungo wa RB Leipzig Naby Keita, 22, ambaye atakuwa na mazungumzo na klabu yake kuhusu mustakbali wake nchini Ujerumani (Times).


Kocha mkuu wa Monaco Leonardo Jardim ana matumaini kuwa Kylian Mbappe, 18, hataondoka, lakini amekiri kuwa wachezaji wengi huenda wakaondoka msimu huu (RMC).

Tottenham wamepanda dau kwa mara ya pili la pauni milioni 27 kumtaka kiungo wa Sporting Lisbon Adrien Silva, 28, (A Bola).

Chelsea wamemuulizia beki wa Real Madrid Danilo, 25 (Marca).

Beki wa Paris St-Germain anayenyatiwa na Manchester City, Marquinhos, 23, amesaini mkataba mpya wa mude mrefu kubakia Ufaransa (Independent).

Newcastle wanafikiria kumchukua beki wa Arsenal Kieran Gibbs (Daily Mirror).

Paris Saint-Germain wamemuulizia kiungo mshambuliaji wa Liverpool Philippe Coutinho, huku Barcelona pia wakimnyatia mchezaji jhuyo kutoka Brazil (Daily Mirror).
.....
Mie namuwazia Lacazette tuuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom