Wakuu wapenda kabumbu ....japo mkuu Nyagei amekuwa bize kutuhabarisha yanayojiri kule Russia lakini mambo yanazidi kuwa mambo ...kila timu inavuna ilichoingia nachooo .....ewaaaaaaaah matokeo ukwajuu kabisa kabisaaaa na kushangaaa kupoo ...
Juzi Chile walikuwa wa kwanza kutinga fainali ..wanastahilii haswaa ...ila huyu jamaa huyuu Alexis Sanchez ...ndo huyu kipenzi wa shululu na clkey wapenzi wa Arsenal ...
Mshahara kuanzia £270,000 mpaka £300,000 kwa wiki ni halali kabisa kwa Alexis Sanchez....... Kinachomfanya aishi chini ya hapo ni Imani ya kumpenda Mungu aliyonayo sambamba na kumuogopa babu Wenger tu.
Huyu jamaa ni mchezaji bora kabisa anayeishi maisha ya kawaida sana..... Amekuwa na kiwango kile kile akiwa na jezi ya Chile lakini pia amekuwa na kiwango kile kile akiwa na jezi ya Arsenal.
Huyu jamaa ana upepo wa hatari... Imani yake na uoga wake mwache aendelee kuishi maisha ya kawaida tu.
Ila na wewe Bravo kweliii bravooo kweli kweliiiii
....
Kutolewa kwa Ureno yawezekana ilikushangaza lakini mpira ndo ulivo ...mpira unadundaaa ila ndo hivo ureno na C7 waoo bye bye japo Huyu usiku ulikuwa wa furaha kwakee ....
Twende sawa usichoke kapuku mwenzangu hii wala sio ngumu kumezaa ila time consuming ....ila yote sawa leo ni furahiiiisikuuuuu ....
Ninamuelewa sana Ronaldo ndani ya uwanja kama CR7 ila Bado sijabahatika kumuelewa nje ya uwanja kabisa kama Baba wa watoto watatu.
Kinachonifanya nimuelewe ndicho kilicho kufanya na wewe uelewe akiwa na jezi nambari 7 mgongoni na kuipeleka mipira nyavuni.
Kinachonifanya nisimwelewe ni namna au njia anazotumia kupata watoto..... Mpaka sasa ana watoto watatu, Christian Jr au Christianinho na hawa Mapacha wa sasa hivi Eva na Matteo...... Tangu kuzaliwa kwa mtoto wa kwanza Christian Ronaldo Jr mpaka Leo hajulikani Mama yake ila aliyehusika kubeba mimba sio Mama wa mtoto, yeye alilipwa tu kwaajili ya kubeba vitengeneza mimba vya wenzie (surrogate mother)...... Hawa Mapacha nao hali imekuwa vivyo hivyo Mama yao pia hajulikani baada ya Mama aliebeba mimba kujifungua na kulipwa fedha kwaajili ya kazi aliyopewa.
Situation hiyo ndiyo imeniacha na maswali mengi sana juu ya CR7 huyu huyu japo mpenzi wake wa sasa Georgina Rodriguez inasemekana ni mjamzito.
Wacha niendelee na research yangu labda ipo siku nitakuja kumwelewa kwanini anatumia wamama wa kukodi ili kubeba virutubisho vyao.... Christian vipi au haupigi kazi mzee ?.... Moja ya maswali ninayojiuliza kimya kimya.
Rafiki zangu madaktari najua kuna kitu mtaweza kuniweka sawa hapo kwa surrogate mother......
Tuachane na hayo ....
Usiku wa kuamkia leoo mpira ukadunda kama kawaida yake ...wengii wapeew ewaaaaaaah ikala kwaooo make Mexico promo alizopewaaa ziliwaingiza mapema fainali mapema kumbe wale vijana wa mjerumani wanawaza jumapili kuliko alhamis...
Aiseeeeehhh, mtoto wa nyoka ni nyoka tu...... Wale wahenga sijui walijifunzia wapi misemo hii. Wajerumani walikuwa bora kuanzia kwa Ter Stegen, emri Can mpaka kwa Leon Goretzka. Mexico walikuwa wanacheza na mtoto wa nyoka tu nikawaza kama wangekuwa wanacheza na joka lenyewe sijui ingekuwaje.
Muller, Ozil, Boateng, Gotze, Neur, Khedira, Kroos, Reus, Gundogan, Sane, belarabi........
German 4-1 Mexico.
Tuwe na siku njemaa